ZILE CANDLES ZENYE UNAONA KWA MT5 It works na zitakupa ugali lakini, unahitaji
1. GOD
2. HIGH SKILLS
3. DISCIPLINE
4. GOOD RISK MANAGEMENT
5. TIME
6. PATIENCE
If you are ready for that, THEN PUT EFFORTS!
TUNAONDOKA!
Ukitaka uimudu vizuri Trading, sheria ya kwanza IPENDE, Sheria ya pili ni kwamba haijalishi inakuumiza namna gani Usiikatie tamaa, Sheria ya tatu tumia nguvu zako zote kujifunza na kujilimbikizia maarifa, Sheria ya nne Usiache kusali na kumuomba Mungu akufanyie wepesi.
HAPPY NEW YEAR MY BROTHERS AND SISTERS IN TRADING.
Haya, iko hivi...
Angalia hizi scenario mbili then u'll realize where the toughness of forex trading always starts...
1. Unaanalyze soko. Unatega. Then baada ya kuingia trade unaona price ina move direct to your Stoploss then baada ya hapo ikishaa kula kichwa, inageuka inaelekea ilipo Target yako..
2. Unaanalyze soko, then unapata trade lets say ya ku-"Buy" Na unajiamini kuwa uko right, unaweka SL, then price inachapa SL alafu ina-Sell vibaya mno.
Umeona hizi Scenario mbili? Najua, hakuna ambayo unaweza kui-Miss kati ya Losses zako zote. Lazima zina fall kwenye hizi two categories...
Sasa bana, kuna baadhi ya watu watakwambia "USIWEKE SL KWASABABU INSTITUTION ZITAONA NA KUIWINDA SL YAKO, SO IF U NEED TO WIN THE GAME ACHANA NA STOPLOSS, ITS A SCAM"
Hapa ndo tunapata nadharia inayoitwa "STOPLOSS HUNTING"
Kwanza kabisa, unatakiwa kuelewa hivi, watu wenye uwezo wa kulisogeza soko na kuifanya price i-move TECHNICALY ni SMC traders (Hapa nazungumzia Institutions) hawa ni kama Hedge funds, mabenki makubwa, Makampuni ya uwekezaji na kadhalika...
Sasa unatakiwa kuelewa zaidi ya kuwa, hawa watu wana Mitaji mikubwa mno, wana uwezo mkubwa wa kusogeza Bei lakini pia wana Data nyingi kuliko wewe hapo unayesoma huu uzi. Hawa jamaa wanaweza kufanya maamuzi YOYOTE kulingana na taarifa za ndani (Insider information) na factors zingine zinazohusisha uchambuzi wa kimsingi (Fundamental analysis). Na uchambuzi thabiti wa Technical (Sijui niiwekeje kwa kibongo).
SMC traders wanaamini kuwa "The best trades always happening after the retail traders have been taken out from the market" (Nimejaribu kuiweka kizungu ili ipendeze sasa kama kinge kimepinda utajua wewe, kikubwa mzigo ufike). Kwahiyo, ili Institutions ziingie sokoni kupiga hela retail traders wanapaswa kuliwa kwanza vichwa ndio maana kuna msemo unasema "Where retail traders put Stoploss is where smart money makes money".
Sasa nataka nikukumbushe kuwa, institution ndio zina power ya kuku induce, ku fake movement na kukuundia structure uzame ukidhani uko sahihi kumbe ni mtego ili uprovide liquidity kwaajili ya Orders zao!.
Kwahiyo, muogope sana mtu anayekwambia "USIWEKE SL KWASABABU WASHKAJI WANAIONA THEN WANAI-HUNT WAKUTOE SOKONI". Narudia, MUOGOPE SANA MTU WA NAMNA HIYO, kwasababu SMC traders hawawindi SL yako peke yako, wao wanawinda LIQUIDITY POOL ili wai-wipe it out kwaajili ya kuprovide liquidity kwaajili ya Order zao (kwahiyo hata usipoweka Hutaizuia price kuamua ilichotaka kuamua). Liquidity pool ni collection ya SL na Orders nyingi (SIO SL YAKO PEKE YAKO). Kwahiyo, hii inachora picha kuwa, Institutions always knows ni wapi mmeweka Stoploss kwasababu ni Obvious inajulikana. Ulipoweka wewe SL na wenzio (emotional traders) wameweka same place. Maana yake ni kuwa, unapoweka order ukaachana na SL utachoma account kwasababu kwenye SMC kuna nadharia inasema "Price doesn't moves randomly: it moves to Liquidity". Na ili iendelee na Movement, ni lazima itosheke na Liquidity iliyokusanywa. Isipotosheka mpaka ikatafuna account yako yote ndio UMEPOTEZA ACCOUNT!! (Wewe ni Looser na hii game utaikimbia kwasababu hutakuwa na hela za kuchoma kila unapo-loose).
So jifunze ni namna gani Institution zinatrade (wakati sahihi wa kuingia trade baada ya wengine kutolewa sokoni na unaingilia wapi), ukijua utaelewa ni sehemu gani ni lazima uhakikishe umeiva (TECHNICAL HAIJAACHA KITU) vizuri ili kupunguza idadi ya mikando, na ku provide liquidity sokoni. The reason is, Soko halijaundwa ili wewe u-win, kwahiyo unapaswa kuwa smart zaidi ku tackle na kukwepa miba na ndio maana kwenye institutional trading kuna msemo unasema "If the moves looks obvious, its PROBABLY WRONG๐"
Hii ina maana ya kuwa, NI LAZIMA UJIFUNZE KUWA TOFAUTI SOKONI, UNLESS OTHERWISE WASHKAJI WATAKU-HUMBLE MPAKA UIKIMBIE GAME.
Learn how to trade like Institution kwasababu nyie hata mjikusanye myatano na mitaji yenu ya dola myambili-mbili hamtaweza kusogeza hata candle moja. Wao ndo wanali move soko, USISHINDANE NAO. UNGANA NAO!
Huwa nna series ya Setups zangu za GOLD (ZA KUSCALP) ambazo zinaprint kila siku (Kwa kujirudia rudia), Nna seti tofauti ila hapa nataka niwawekee SETUPS NNE (Na mifano yake), ambazo ni Common na huwa zinajirudia mara nyingi zaidi (Huwa naziita Utajiri wangu๐).
Hii ni mifano ya Bactesting. Kwa ambazo nimeforward Test zipo kwenye series ya Charts zangu ambazo nimeshaa wahi kushare na ninyi kwenye huu ukurasa wangu. Huwa nna Notebooks na Counter books zina maelezo mengi (ambayo nimeandika mara nyingi zaidi nilipokuwa nikitrade au nikiwa nabacktest), lakini hapa nitashare Summary ya Notebook yangu!
Chimbuko la Hizi setups ni kujibobeza katika kujifunza Technical, kusoma tabia za namna Gold ina react katika maeneo Tofauti (Maeneo korofi), mwenendo wa mfanano wa idadi ya Pips price inavyotembea, na tofauti ya mjongeo wa Gold kulingana na Mabadiliko ya Soko. Nimebactest sana.. Na nimetrade sana kiasi cha kunifanya niamini na Kujiamini zaidi kwenye hiki ninacho kifanya. KWENYE KILA SETUP HAPO, HAKUNA SL INAYOZIDI PIPS 25 NA HAKUNA TP INAYOPUNGUA PIPS 100.
NB: MSIJADILI KUHUSU MWANDIKO WANGU, UKISHINDWA KUSOMA JITAHIDI KUELEWA LUGHA YA PICHA (Hata hivyo sijaweka maelezo ya Kina)๐.
SETUP NAMBA 1 NA MIFANO YAKE
Soko huwa linaprovide Opportunities nyingi. Ni chaguo lako kuamua Uiendeshe nidhamu, au nidhamu Ikuendeshe.
I got another trade at 2am. I've closed the Deal with 390 Pips for today!
Am done...
#CertifiedProScalper!
#BlessedMonday