Wanasiasa na viongozi wanapoamua kutunushiana misuli inayoumia ni demokrasia na sisi wananchi. Tujifunze kuachiana nafasi kila mtu afanye yake. Sisi watanzania, hatutaki kurudi kule tulikotoka. Tunatamani, tuishi kwa amani na uhuru wa kufanya yale tuliyo na haki nayo.