Tumetokea katika mazingira tofauti na kulelewa kwa malezi tofauti. Kuna vitu unaweza kuwa ulipata bahati ya kuelekezwa na wazazi ama walezi wako kuna wenzako hawakupata bahati hiyo. Aidha walipoteza wazazi wakiwa na umri mdogo au wazazi/walezi wao hawakuwa na muda wa kuwaelekeza. Inapofika ukubwani huku ukaanza kuwahukumu na kuwalaumu kwa vitu ambavyo hata sio kosa lao ni kuwaonea tu. Tuna nafasi ya kuelekezana na kufundishana na huko ndio kukamilishana kwenyewe.