@bushlander_@Aruatani Kwa sababu watu wakipata pesa wanasahau kadi. Mtu akishachukua pesa anaacha kadi anaondoka. So chukua kadi weka kisha chukua pesa ondoka.
Karibuni Tanzania.
Karibuni Nyumbani.
Leo nimejumuika na Marais wa nchi na Wawakilishi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha.
Miaka 26 tangu kurejeshwa kwa umoja huu, umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha nguvu za nchi zetu kama ndugu, kuongeza sauti ya pamoja katika masuala mbalimbali, na kujenga mustakabali wenye mafanikio kwa wananchi wa Afrika Mashariki.
Ninawapongeza na kuwatakia kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Siku hii inatupa fursa ya kipekee ya kutambua, kujivunia na kusherehekea mafanikio tuliyopata, hasa katika elimu, afya, uchumi na uongozi.
Siku hii inatukumbusha pia wajibu wetu wa msingi kwa waasisi wetu na kwa vizazi vya sasa na vijavyo; wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke, ikiwa ni sehemu muhimu ya kazi ya kukomboa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Watu wengi hufikiri kuwa mwanaume ni nguvu au umri. Lakini ukweli ni huu:
Mwanaume halisi ni yule anayewajibika.
Anayeheshimu wengine.
Anayelinda na kujali familia yake.
Na anayesimama kwenye maamuzi yake hata wakati mambo ni magumu.
Uanaume sio kelele, ni tabia.
....
#fyp#mi