Dunia inafahamu ukweli. Ndiyo maana Tundu Lissu anasema akipatikana na hatia, anyongwe hadi kufa. CCM wanasema adhabu siyo kunyongwa pekee
Tundu Lissu anaeleza Mahakama kwamba adhabu ya uhaini ni kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa. CCM wanasema Mahakama iamue kwa hisia tu
Anyways, tuachane na huo ujinga wa CCM
EPP Group (European People’s Party Group). Ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kati-kulia (centre-right) katika Bunge la Ulaya.
EPP Group (European People’s Party Group) ndilo kundi kubwa zaidi na lenye ushawishi mkubwa zaidi katika Bunge la Ulaya (European Parliament).
EPP GROUP (European People’s Party Group) wamempendekeza Tundu Lissu kugombea Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought)
Pia, ECR GROUP (European Conservatives and Reformists Group) wameungana na EPP GROUP kumpendekeza Tundu Lissu kuwa mgombea wao
ECR GROUP ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kulia/kihafidhina (right-wing/conservative) katika Bunge la Ulaya (European Parliament)
Kumpendekeza Tundu Lissu kunamaanisha wanamuona ni alama ya ujasiri na kielelezo cha watetezi wa demokrasia wanaopitia vizuizi
Kupendekezwa kwa Tundu Lissu ni tamko kwamba mapambano ya miaka mingi, yametambuliwa katika ngazi ya juu kabisa ya kitaasisi Barani Ulaya
Uteuzi huu TAL akiwa gerezani kwa mashtaka ya uhaini unaiweka diplomasia ya Tanzania na mazingira ya kisiasa ya ndani katika jicho la kimataifa;
Unaiwekea serikali na taasisi za kisheria ‘presha’ ya kuendelea kuheshimu misingi ya demokrasia, uwazi, na haki za kisiasa na michakato ya kiuchaguzi
Mchakato wa kumchagua mshindi wa Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) unafuata hatua zilizowekwa na Bunge la Ulaya
Kupendekezwa ni hatua ya kwanza katika mchakato mrefu wa utoaji wa tuzo hii. Siyo kwamba Tundu Lissu kupendekezwa ndiyo ameteuliwa mshindi
Ili mteule aingie katika kinyanganyiro, anapaswa kupendekezwa na: Kila kundi au kundi la wabunge linaweza kupendekeza jina moja pekee
Wagombea waliopendekezwa huwasilishwa katika mkutano wa pamoja wa kamati kadhaa za Bunge la Ulaya kwa ajili ya mchujo wa wagombea
Kamati ya Mambo ya Nje, Kamati ya Mandeleo, na Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu. Hapa, maelezo ya kila mgombea husomwa mbele ya wabunge
Kamati mbili kuu za Bunge la Ulaya; Kamati ya Mambo ya Nje (AFET) na Kamati ya Mandeleo (DEVE), hufanya zoezi la kura ya pamoja kwa njia ya siri
Kutokana na kura hizo, wanachagua wagombea watatu wenye kura nyingi zaidi ili kuunda orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Uamuzi wa mwisho wa kumchagua na kumpata mshindi haufanywi na kamati, bali unafanywa na Mkutano wa Marais (Conference of Presidents)
Kundi hili hukutana faragha, kujadili finalists watatu, na kumtangaza mshindi mmoja rasmi kutoka katika orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Mshindi hualikwa katika ukumbi wa Bunge la
Ulaya mjini Strasbourg, France, wakati wa kikao cha pekee cha Bunge la Ulaya, mwezi Desemba
Huko, mshindi hutunukiwa cheti rasmi cha ushindi pamoja na zawadi ya kifedha ya £50,000. Hii kwa sasa ni sawa na takribani TZS 174,262,600
Tuzo ya Sakharov ni kitu gani?
Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) ndiyo tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya
Sakharov Prize for Freedom of Thought iIlianzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya mwanasayansi na mpinzani wa Kisovieti Andrei Sakharov
Tuzo hizi wamewahi kushinda watu wazito sana Duniani wakiwepo; Nelson Mandela (1988), Kofi Annan (2003), na Malala Yousafzai (2013)
Sakharov Prize for Freedom of Thought hutolewa pia kwa watu au mashirika yanayojitolea kutetea uhuru wa mawazo na haki za binadamu Duniani
Wakati Serikali Katili ya CCM inataka kuaminisha Dunia Tundu Lissu ni mhaini, Dunia inakataa kwa vitendo uongo na ghiliba za serikali ya CCM
Dunia inampendekeza Tundu Lissu kuwa mshindi wa tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya. Kwa heshimaaaa.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Africa democracy honours:
Tanzania’s Tundu Lissu and Uganda’s Kizza Besigye recognized. The two crowned as champions of democracy in Africa. Honours presented at the Democracy Union of Africa conference. Lissu’s award comes as Tanzania heads to the polls
#CitizenExplainer
Chunga, tamaa mbaya!
Picha hii nzuri sana, ilipigwa siku ya Jumatatu, 17.08.2020 mbele lango kuingia katika ofisi za Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bunda.
Hii ni siku ambayo Ester Bulaya alikuwa amekwenda kurejesha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Bunda Mjini. Ubunge ambao hakika, tulishinda.
Naonekana hapo nyuma. Uso wenye tabasamu. Nilikuwa Meneja (Campaign Manager) katika kampeni za Ester Amos Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa 2020
Timu yetu ya kampeni ilifanya kampeni za kisasa sana katika mitaa yote 88 ya Jimbo la Bunda Mjini. Mikutano ya hadhara na kampeni ya nyumba kwa nyumba.
Mchakato wote wa uchaguzi uliporwa na DOLA katili la CCM. Fomu za matokeo Na.24 wasimamizi walijaza usiku wa siku ya kupiga kura, ukumbi wa halmashauri.
Mawakala wote wa CDM wakaondolewa katika vituo vya kupiga kura. Saini wakajaza wasimamizi wenyewe. Mgombea, Esther Bulaya alikataliwa kukagua fomu.
Katika ngome yetu ya majumuisho, iliyokuwa katika Hoteli ya De Light, mawakala wetu walikuwa wanakuja bila matokeo, waliokuja na matokeo hayana saini.
Kwa majumuisho yetu, mgombe wangu, Esther Amos Bulaya alipata kura 31,129. Lakini, kura za mgombea wa CCM 13,258 akapewa mgombea wangu, Ester Bulaya.
Wakati wa kampeni, ngome yetu ya uchaguzi ilivamiwa usiku na OC-CID Bunda, na kuanza upekuzi bila kibali, majira ya saa 9 usiku. Walimkuta mgombea siku hiyo.
Wakatuhoji kila aliyekuwa ndani siku hiyo kwa kuonesha vitambulisho vyetu. Ambaye hakuwa na kitambulisho, walitaka kuondoka naye. Tukaleta noma sana.
Vijana wetu wa ulinzi na matangazo wakiwa katika matangazo ya mkutano wa kufunga kampeni, walivamiwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya.
Wengine walifanikiwa kukimbia mlimani. Wakalala huko kwa siku tatu. Vijana wetu 13, walikamatwa, wakapewa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery).
Gari ya matangazo iliendelea kushikiliwa hadi baada ya uchaguzi. Siku ya kufunga kampeni tulitafuta vifaa vingine vya matangazo. Vilivyopo, vipo polisi Bunda.
Baada ya uchaguzi, siku ya matokeo, Ester Bulaya akakimbilia kujificha Musoma Mjini. Kwa kuwa kulikuwa na sekeseke la kuwakamata viongozi wa CHADEMA.
Ni wakati huo Polisi walimkamata Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob, Dar es Salaam, kwamba wanaratibu maandamano kupinga matokeo
Mimi nilibaki Bunda kwa miezi mitatu nikishughulika hao vijana wetu 13 wa ulinzi watoke gerezani. Nisingeweza kuwaacha. Walikuwa ndugu zangu wakati wa kampeni.
Bunda siyo kwetu na siyo kwangu. Hapo ilibidi kuishi hotelini kwa muda wote huo. Kesi inamalizika, nikashughulikia gari na vifaa vya muziki Polisi.
Siku moja tukiwa Mahakamani Bunda, tukishughulika na kesi ya vijana wale 13, tunamuona Ester Bulaya akiwa gereji chini ya tenti anaapishwa kuwa mbunge.
Hakuwahi hata kunishirikisha kwamba anao mpango wa kuwa mbunge wa viti maalum. Nilishangaa tu ameibuka bungeni, Job Ndugai anamuapisha kuwa mbunge.
Nikaendelea kubaki Bunda. Baada ya siku 62, vijana wetu wote waliwaachia huru baada ya DPP kuleta ombi mahakamani hana nia ya kuendelea na kesi.
Polisi wakaachia gari. Vijana wetu wakashukuru. Kila mmoja akarejea kwao baada ya kusota kwa miezi miwilo na siku kadhaa gerezani wakimpambania Bulaya.
Wakakumbuka ile siku ambayo msafara wa CHADEMA ukikutana msafara wa CCM jioni baada ya mkutano na vita ya mawe na mapanga kuibuka. Watu walichanika.
Ester Bulaya amesahau, anajiunga na MaCCM, kutafuta ubunge ambao MaCCM yalitupora kwa watu wetu kuumizwa? Ni jambo baya. Lakini amerejea kwao.
Watu wetu walipigwa mapanga na kujeruhiwa, walipewa kesi zisizo na dhamana, wakaishi gerezani kwa muda mrefu ili awe mbunge, leo anajiunga na mbogamboga?
Haina noma #NoReformsNoElection
JE UASI NI KOSA KISHERIA HAPA TANZANIA?
Ni muhimu kutambua kua Kuna tofauti kati ya kuasi dola na kuasi mifumo kandamizi.
Kimsingi kuasi dola ni uhaini,
lakini kuasi mifumo kandamizi ni uzalendo."
KUASI DOLA
Kuasi dola ni kuchukua hatua za vurugu au mapinduzi dhidi ya mamlaka halali ya nchi—kitu kinachotafsiriwa kama uhaini katika sheria nyingi duniani, ikiwemo Tanzania.Hii inaweza kujumuisha matendo ya kudhutu viongozi wakuu wa nchi mf.Rais au Spika wa Bunge
KUASI MIFUMO KANDAMIZI.
Kuasi mifumo kandamizi, kwa upande mwingine, ni kusimama dhidi ya sheria, sera, au vitendo vinavyokiuka haki za binadamu, uhuru wa watu, au misingi ya utawala bora.kuasi na kukataa sjetia na kanuni zenye kuchochea maadili mabovu,wizi wa kura na matumizi mabaya katika vyombo vya umma. Hii ni hatua ya uzalendo, kwani inalenga kurekebisha kasoro ndani ya mfumo kwa ajili ya haki, usawa, na ustawi wa wananchi.
Katika Taifa lenye watu timamu kuasi na kupinga mifumo kandamizi ya kisera,kidemokrasia na kiuwakilishi siyo uhai ni wala uhalifu.
BAK Mwabukusi.
HILI LA ZAMBIA KAMA SI FUNZO, NI KENGELE.
Rais Mstaafu wa sita wa Zambia Edgar Lungu, amefariki tarehe 5/6/2025 akiwa matibabu huko Afrika ya Kusini. Atazikwa Afrika Kusini 25/6/2025 na misa itaongozwa na Askofu Mkuu wa Lusaka Alick Banda.
Wakati huo huo, serikali ya Zambia imefungua kesi ya kuzuia Rais Lungu asizikwe Afrika Kusini. Kesi hiyo itasikilizwa asubuhi saa 2 asubuhi, wakati ibada ya mazishi itaanza saa 4 asubuhi mjini Pretoria.
Rais wa saba, Hekainde Hichilema (HH) ndiye yuko madarakani. Familia ya hayati Lungu imekataa kukubaliana na serikali ya Zambia kuhusu taratibu za mazishi kwa kusema marehemu aliacha wosia kuwa akifa, Rais Hichilema asisogelee wala kuhudhuria mazishi yake.
Alipokuwa madarakani, Rais Lungu alimweka ndani Rais wa sasa mara 15 kwa tuhuma mbalimbali. Naye Rais Hichilema alipomshinda Lungu na kuingia madarakani, amemuweka katika kifungo cha ndani na kumnyima uhuru wa kutembea, kwenda kanisani na hata kugombea katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2026.
Yote haya yanatia aibu pande zote. Lakini kwetu Tanzania, haya kama si mafunzo kwetu, basi ni kengele ya kutuamsha tuweke mambo yetu vizuri.
1. Wale tulio madarakani kama mimi tujue ipo siku madaraka haya yataondoka, kwa njia nzuri au mbaya. Kutambua tu kuwa yataondoka, kutufanye kunyenyekea na kutenda wema na haki.
2. Wale wanaotafuta madaraka ni vema kutambua kuwa “mapenzi ya kuposea, siyo ya kuolea na kutunza ndoa”. Ni rahisi kulalamika kuliko kulalamikiwa. Mkiingia madarakani msitumie sheria mbaya zilizoachwa na watangulizi wenu kuwatesa wapinzani wenu wa kisiasa. Unyenyekevu si udhaifu bali unahifadhi nguvu na raslimali.
3. Ukiwa madarakani una uwezo wote wa kukataa ushauri unaopewa. Lakini, huna uwezo wala madaraka ya kukataa madhara ya ukaidi wako wa kukataa ushauri. Machozi yako wakati wa majuto ni kama yale ya samaki. Utazomewa hata na uliowasaidia. Nimeyaona kwa Lungu.
4. Kila aliye madarakani hutoa hotuba nzuri na maelekezo sahihi. Hotuba za Hichilema ni tamu na zinavutia, lakini zinaficha wingi wa kisasi na uchungu. Wasaidizi hawasikilizi hotuba zake; wanakumbuka aliyotendewa. Kiongozi mzuri ni mwenye uwezo wa kudhibiti chawa wake.
5. Familia za viongozi humwangusha kiongozi kabla hajaangushwa na wapinzani wake. Kiongozi anayelaumiwa na familia yake kwa “kutowasaidia”, anaweza kuwa kiongozi bora kuliko “anayebeba” familia nzima. Kiongozi “akiwasahau” ndugu zake, anakuwa amewaepusha na mateso baada ya yeye kuondoka. “Akiwabeba” anaondoka na kuzama nao. Nimeliona kwa Lungu.
6. Madaraka makubwa mikononi mwa mtu mmoja ni hatari kwake, marafiki na adui zake. Kwa kuwa ndugu na marafiki hawana kinga, ni hekima wakijitenga na mwenye madaraka. Kipimo halisi cha maadili ya mwenye madaraka makubwa, ni pale hata maadui na wapinzani wake wanapojiona wako salama mikononi mwake. Yaani adui yako usimwonee wala kumpendelea.
7. Kwa viwango vya siasa za Afrika, maisha mazuri baada ya kustaafu yanaweza kuwa yale ya “hukuharibu kitu na hukutenda la maana”. Kama ulionea, utasutwa. Kama ulitenda mazuri, yataharibiwa ukiona, ufe kwa kihoro. Kila kiongozi anakuja na mambo yake. Kwa hiyo? Sikiliza watu, usisikilize washauri wanaolipwa ili kukushauri. Ukistaafu utaishi na watu, siyo washauri.
Hichilema, Uchaguzi Mkuu ni mwaka kesho 2026.
Jumatano kama Leo mwaka jana ilikuwa 26.6.2024 ndio siku niliyopokea KIPIGO kutoka kwa WATEKAJI nusu KUFA.
Majina ya BONI YAI & MARTIN MARANJA MASESE ndio yaliokoa uhai wangu. Sijawahi acha kusema hili Loud & clear japo inasound kama USNICH ila ndio ukweli.
Siku ilianza poa, niliamshwa na ADHANA, MBU & BARIDI kali lililokuwa likipiga kwenye Cello yangu. Siku ile sikuletewa chakula kabisa. Nilikuwa mpweke ambae sijui hatima yangu. Nilikuwa mtu wa KUOMBA kimya kimya kila wakati nikizunguka ile Cello.
Ilipofika saa SABA MCHANA nikaona watu wawili mlangoni wakifungua CELLO yangu huku wakiwa wamevalia vinyago usoni (BOSHORI). Mionekano yao. Ni watu ambao wana miili mikubwa na miili ya MAZOEZI.
Mmoja alivalia CHENI nzito ya silva, ila wote walikuwa na MAPETE mengi mikononi yale ya silver kama ya WAGANGA. Kila mmoja alikuwa nazo sio chini ya TANO kwenye vidole vyake.
Wakafika na kuongea na mimi. “SATIVA Tumetoka kwenye kikao kizito KUKUJADILI wewe. Je UPO TAYARI KUTOA USHIRIKIANO?”
Nikajibu kwa SHAUKU “Ndio nipo tayari” basi wakaniambia tunaondoka hapa. Vipi ulipewa chakula? Nikawaambia leo sijapewa ila siku mbili nyuma nilipewa. Wakasema SAFI. Wakanivalisha BOSHORI usoni na kukaza pingu mikononi mwangu.
Wakanitoa huku mmoja akiwa upande wa kushoto na mwingine kulia. Wakawa wanaondoka na mimi kwa kuniongoza. Tukawa tunatoka pale kituoni tunashuka ngazi mdogo mdogo nikihesabu kuhakiki idadi kama nilivyoingia. Zilikuwa mikanyago mitatu.
Kisha nikaingizwa kwenye GARI. Gari lilikuwa lile lile HILUX 4X4. Ila round hii aliongezeka mtu ambae wao walikuwa wanamuita “MJOMBA”. Huyu aliingia na kukaa mbele ya Gari kushoto. Kisha mimi nikawekwa katikati siti ya nyuma. Pembeni mtu na kulia mtu. Wale waliokuja kunitoa Pale kituoni.
Wakaniambia “Sativa leo tumeongezeka, tunae MJOMBA msalimie”, nikasema “ShikamoooL” jamaa akaitikia MARAHABA. Waakaanza kama kuchekesha. Huyu ndio mjomba wetu na blah blah nyingi huku safari ikiwa imepamba moto.
Baada ya masaa kama matatu hivi, gari ikasimama kwenye msitu kisha wakashuka watu wote nikabaki kwenye gari na mmoja. Baada ya dakika kadhaa nikaambiwa nishuke. Na wakati huo nikavuliwa
BOSHORI KICHWANI. Nikawa naona. Nikiwa na PINGU MIKONONI kama kawaida.
Mazingira yalikuwa ya PORI na gari ilikuwa imesimama kama kati kati ya msitu. Hali ya HEWA kulikuwa na jua fulani kama la SAA KUMI jioni. Miti mingi. Basi nikaambiwa nikae chini. Hapo nilizungushwa NYUMA ya gari ambapo walifungua BUTI la ile gari ambayo nadhani ndio ilibeba VIPE VIFAA VYA UTESWAJI.
Walikuwa watu wanne MBAVU isipokuwa “MJOMBA” huyu alikuwa na mwili wa kawaida na muonekano kama MTUMISHI wa umma maana hata ongea yake ilikuwa official sana hakuwa mtu wa matusi kama WATEKAJI. Ni kama alikuwa ndio BOSS wao, nadhani ndiomaana alikaa mbele kwenye gari.
Walisimama kwa kunizunguka. Mm nikiwa nimekaa chini nimenyoosha miguu. Mbele yangu kulikuwa na MAFIMBO, MACHUMA, Mapanga na mavitu mengi ya kutisha ya KUTESEA. Moyoni nikajua hapa sasa ndio Mwisho wangu.
Aliesimama mbele yangu alikuwa ameshika simu na kuwa ananirekodi na kuniuliza maswali. “kwanini unaisumbua SERIKALI?, Nani anakutuma uisumbue serikali?” Nikajibu mimi situmwi na mtu na hayupo anae nituma nafanya kwa mapenzi.
OYAAA..!! nikiwa nimeconcetrate na jule jamaa anaeniuliza maswali huku nyuma kuna jamaa alinipiga na UBAPA WA PANGA kwenye uti wa MGONGO nilipiga kelele ya maumivu makali na kuanza kulia. Wakaanza kunishambulia wote kwa pamoja. Aliekuwa anarekodi akaacha kila mtu akachukua ZANA yake pale chini na kuanza kunishambulia.
Nilikula KIPIGO kama cha dakika 50. Nilipigwa kila aina ya STYLE YA MATESO unayoijua wewe. Unyao ulipigwa sana, ENKA za miguu zilipigwa sana kiasi cha kushindwa kabisa kuzikanyagia. Magoti yalipigwa sana, mabega yalipigwa sana. Mgongo wote ulivilia ALAMA ZA MABAPA YA MAPANGA.
Zilikuwa dakika 50 mpaka saa moja La MOTO sana. Sikupigwa KICHWANI TUU.
Thread👇🏾
Wiki hii, baada ya jitihada za kumtafuta kamishina wa ardhi mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Shukrani Kyando bila mafanikio, tulifanikiwa kuonana ana kwa ana
Nilimtafuta anipe majibu kwa nini anasita kutekeleza umilikishaji wa ardhi ya yule mzee wa miaka 85 kwa amri ya mahakama?
TUJIEPUSHE NA ROHO YA KAINI KWA ABEL
Ni kanuni ya haki kwamba kama wananchi wana uhalali wa kukosoa maamuzi yasiyoridhisha ya mahakama, basi wana haki hiyo hiyo ya kuyapongeza maamuzi bora yanayolinda misingi ya utawala wa sheria.
Kwa mantiki hiyo, ni jambo lisilokubalika kwa Bunge—au Spika wa Bunge—kubeza shangwe halali za wananchi na wadau wa haki wanapoukaribisha uamuzi makini wa Mahakama ya Rufani. Badala ya kauli za dharau, hili liwe fundisho na changamoto kwa Bunge kujipambanua kwa kutunga sheria bora, zinazojibu mahitaji halisi ya wananchi, na hivyo kulifanya liendelee kuwa chombo muhimu na husika (relevant) katika maisha yao ya kila siku.
Ni kosa kuu na tishio kwa misingi ya mgawanyo wa madaraka pale mhimili mmoja unapotoa kauli inayoashiria kwamba unaweza kutunga sheria zinazofuta au kudhoofisha maamuzi ya mhimili mwingine. Tabia hii haisaidii kukuza utulivu wa kikatiba, bali hudhoofisha imani ya umma katika taasisi zetu nyeti.
Kwa sababu hiyo, ninaunga mkono kikamilifu wale wote wanaousherehekea uamuzi huu muhimu wa Mahakama ya Rufani. Ni maamuzi ya msingi yatakayokumbukwa kwa kuimarisha haki, usawa, na uhuru wa mahakama. Tunatarajia kwamba uamuzi huu utaheshimiwa na kila mtu mwenye utimamu wa fikra na anayejali hatma ya taifa linaloongozwa kwa misingi ya sheria.
Kauli ya Mheshimiwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, ni ya kusikitisha na haistahili kutolewa tena. Ni vyema Spika atafakari uzito wa madaraka yake na kuepuka matamshi yanayopandikiza chuki dhidi ya mhimili mwingine. Kuendelea kwa kauli kama hizi kunaweza kumomonyoa misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, na heshima ya taasisi zetu.
Tuilinde mamlaka ya mahakama, tuienzi katiba, na tusonge mbele tukiwa na moyo wa ujenzi na si wa mafarakano—tukiepuka “roho ya Kaini kwa Abel.”
BAK Mwabukusi
President-TLS
VIDEO:
Jeshi la limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya waumini wa wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory Of Christ Tanzania Church).
Waumini hao walikuwa wanaandamana kwenye njia ya Morogoro Road wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali.
Tukio hili lingekuwa limetokea Tanzania halafu Hospital watoe ushaidi wa CCTV footage kama hivi ambao unaikaba Serikali koromeo then Media zirushe.
Muda huu Idd Amin Mama angekuwa keshaifungia hiyo Hospitali pamoja na media.
Kenya wametuacha mbali sana.
@zittokabwe
Kiujumla pendekezo la kutoza WHT ya 10% kwenye mapato yaliyobaki (retained earnings ) linaweza kuwa na athari kubwa kwa kampuni ambazo zilikuwa na malengo ya muda mrefu ya uwekezaji.
Nami nashauri liondolewe pamoja na
Kukubaliana na Waziri sio double taxation "kiufundi" lakini sera ina ukakasi kwani inalenga walipakodi walewale ndani ya kampuni yao. Ni high au excessive taxation.
Kwa kuwa tafsiri ya Mapato Yaliyobaki ni faida ambayo kampuni imepata baada ya kulipa kodi ya mapato (corporate income tax kwa sasa 30%), lakini haijagawiwa kwa wanahisa kama gawio (dividends), fedha hizi huwekwa kwa ajili ya kuendeleza shughuli au uwekezaji wa kampuni. Kwa hiyo ukizitoza kodi ya zuio ya 10% kana kwamba ni gawio Athari Zinazowezekana kwa Makampuni ni pamoja na
1.Uwezo wa Uwekezaji Kupungua na motisha ya kampuni kuwekeza faida yake katika kupanua biashara au miradi mipya kutoweka.
2 Kampuni Kuweza Kulazimika Kutoa Gawio Mapema ili kuepuka kodi hii na kuacha ilipwe na mwanahisa, hata kama haikuwa kwenye mpango wao wa kimkakati.
3 Mzigo kwa Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) nyingi zinamilikiwa na vijana na wanawake hutegemea retained earnings kwa ukuaji wao. Kodi hii inaweza kuwabana kifedha na kudhoofisha ukuaji wao. Wakawa Wanagawana kila kitu badala ya kuweka akiba na kukuza mtaji.
3 Uwekezaji wa Ndani na wa Kigeni unaweza kuathiriwa ikiwa wawekezaji wataona kuwa faida hazihifadhiwi kwa maendeleo ya kampuni na kukuza mtaji bali zinapunguzwa kwa kodi zaidi ndani ya kampuni.
Kwa kuwa gawio linatozwa kodi ya zuio ya 10% hakuna madhara kulinda uwekezaji ukakua na ukasubiri mwanahisa kulipa kodi hiyo mara tu gawio likifanyika.
Sera nzuri ya kodi sharti kulenga matakwa ya muda mfupi kwa kuongeza makusanyo (mfano kutoza WHTkwenye gawio) huku ikilea ukuaji wa mtaji wa biashara na uzalishaji (kwa kutotoza WHT kwenye retained earnings) .
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania leo imeagiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta vifungu vinne vya sheria vilivyokuwa vikiweka vikwazo mashauri ya kikatiba yenye maslahi ya umma.
Mwaka 2020 bunge lilifanya merekebisho ya sheria mbalimbali pamoja na zile utekelezaji wa Haki za msingi na wajibu (sura ya 3) kwa kuongeza vifungu vya 4(2), 4(3), 4(4), na 4(5). Vifungu hivyo ni mwiba kwa mashauri yenye maslahi ya umma ambayo vilikuwa vilazimisha muambajio awe na muathirika wa moja kwa moja na jambo liliomfanya afungue shauri pia mashauri yote yanayowahusu viongozi wakuu kama vile Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mku, Spika, Naibu Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, yafunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu na sio kuwahusisha viongozi hao.
Uamuzi huo umesomwa jana tarehe 13 Juni 2025, na Joseph Fovo, Naibu Msajili wa mahakama hiyo ambaye aliusoma kwa njia ya mtandao.
Uamuzi huo uliobatilisha vifungo vyote vinne vilivyolalamikiwa aliyefungua shauri hilo Wakili Onesmo Olengurumwa, mwanaharakati wa haki za binadamu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Rufaa hiyo Na. 134 ya Mwaka 2022 iliyosikiliza mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa: Jaji Rehema Levira, Jaji Wilfred Rumanyika na Jaji Gerald Ngwembe. Wakili Olengurumwa aliwakilishwa na jopo la mawakili maarufu likiongozwa na Prof. Issa Shivji pamoja na Dk. Rugemeleza Nshala, Mpale Mpoki na Wakili John Seka.
Uamuzi huo ulisema kuwa:- Kifungu cha 4(2) kinavunja dhana ya mashauri ya maslahi kwa umma kwa kuhitaji waathirika binafsi pekee, hali inayokinzana na Ibara ya 26(2) ya Katiba.
Kifungu cha 4(3) ni batili kwa kuwa kinachanganya masharti ya Ibara ya 30(3) (maslahi binafsi) na haki za maslahi kwa umma zinazolindwa chini ya Ibara ya 26(2).
Kifungu cha 4(4) ni batili kwa kuwa Mwanasheria Mkuu hana mamlaka ya kikatiba kuwakilisha mihimili mingine, hasa Mahakama au viongozi wa kisiasa walio huru kikatiba kama Jaji Mkuu.
Kifungu cha 4(5) pia ni batili kwa kuwa hakuna sheria nyingine zinazotoa nafuu ya moja kwa moja kwa mashauri ya maslahi ya umma.
KIlicholalamikiwa awali
Kifungu cha 4(2): Kilihitaji mtu anayetaka kufungua kesi ya kikatiba kuambatanisha kiapo kinachoeleza namna alivyoathirika binafsi na ukiukwaji huo.
Kifungu cha 4(3): Kiliongeza kizuizi kwa mashauri ya maslahi ya umma kwa kutaka mlalamikaji aonyeshe maslahi binafsi sawa na Ibara ya 30(3) ya Katiba.
Kifungu cha 4(4): Kiliweka sharti kuwa kesi dhidi ya viongozi waandamizi serikalini – Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Naibu Spika na Jaji Mkuu – zifunguliwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya wahusika hao moja kwa moja.
Kifungu cha 4(5): Kilimtaka mtu anayepanga kufungua kesi kutafuta kwanza nafuu kupitia sheria nyingine zilizopo kabla ya kufungua kesi chini ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi.
Awali, Mahakama Kuu ya Tanzania iliitupilia mbali kesi hiyo mnamo Februari 15, 2022, kwa maelezo kuwa vifungu hivyo havivunji Katiba wala mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Mahakama Kuu ilisisitiza kuwa vifungu hivyo vinakamilisha Ibara ya 26(2) na 30(3) ya Katiba, na vinaakisi misingi ya utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka, na mfumo wa kimataifa wa haki.
Hata hivyo, Wakili Olengurumwa hakuridhika na uamuzi huo na kukata rufaa Mahakama ya Rufaa mwaka huo huo wa 2022.
Profes Issa Shivji Mwanazuoni mkongwe nchini Tanzania ambaye pia ni mmoja wa mawakili waliomwakilisha Olengurumwa kwenye shauri hilo amesema kuwa uamuzi huo ni umetoa faraja kwenye duru za haki “ni uamuzi wa kijasiri imepita takibani miaka 10 mahakama haijawahi kufanya uamuzi kama huu.”
@bunge_tz JE DENI LA TAIFA NI STAHIMILIVU KWELI? Kuna vigezo viwili vya kuangalia. 1. Kwanza ni Mtazamo wa Mapato ya Serikali yanayotumika Kulipia Deni. Hapa tumelemewa kwani hadi Juni 2024, Tanzania ilitumia asilimia 44.3 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kulipia deni la umma ikivuka kabisa kiwango cha juu kilichopendekezwa na IMF na Benki ya Dunia ambacho ni asilimia 18 kwa nchi zenye uwezo wa kati wa kubeba deni na hivyo kuathiri uwezo na uwekezaji wa serikali katika huduma muhimu kama elimu, afya na miundombinu. Barabara nyingi ziko hali mbaya na Makandarasi wengi hawajalipwa na baadhi wamefirisika. Vijana waliojiajiri kama makandarasi hawawezi kuimarika ikiwa hawalipwi katika muda kwa huduma wanazotoa.
2. Kigezo cha pili ni Uwiano wa deni kwa Pato la Taifa (GDP).
Kufikia Juni 30, 2024, deni la taifa lilifikia Shilingi Trilioni 97.35, ongezeko la asilimia 18.36 kutoka mwaka uliopita. Na katika bajeti mpya limefikia Trilioni 107.
Hata hivyo, uwiano wa deni kwa Pato la Taifa (GDP) ulikuwa asilimia 30.8 – chini ya kiwango cha hatari cha asilimia 55 kinachotumiwa na IMF kwa nchi zenye uwezo wa kati wa kubeba deni.
Hii ina maana kuwa, kwa sasa, ukubwa wa deni ukilinganishwa na uchumi bado uko katika viwango vinavyokubalika na wakopeshaji hasa kwa maslahi yao.
Tathmini ya Hatari na Uendelevu wa Deni
Kwa mujibu wa uchambuzi wa pamoja wa IMF na Benki ya Dunia, Tanzania bado iko katika hatari ya kati ya kushindwa kulipa deni la nje (moderate risk of debt distress).
Ingawa uwiano wa deni kwa GDP uko chini, ongezeko kubwa la sehemu ya mapato ya serikali linalotumika kulipia deni linaashiria ongezeko la mzigo wa deni kwa muda mfupi.
Kiujumla ni kweli Tanzania bado ina nafasi ya kudhibiti deni lake kwa mujibu wa viwango vya kimataifa, hasa ikizingatiwa uwiano wa deni kwa GDP.
Hata hivyo, ongezeko la kasi ya sehemu ya mapato ya serikali inayotumika kulipia deni linaashiria hitaji la kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kutumia mikopo kwa tija zaidi.
Uwazi, nidhamu ya bajeti, na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha uendelevu wa deni na kulinda huduma za msingi kwa wananchi na kuepuka kuwabebesha mzigo wa kodi na tozo za viwango vya juu jambo ambalo litaathiri uchumi wa kaya na jamii na kuongeza umaskini.