Tumefanya jitihada nyingi kuwasiliana na @tanpol mkoa wa Mwanza ili waleze ni sababu za kumkamata @AdvocateSailenc na ni kituo gani wamempeleka lakini hadi Sasa hakuna anayetoa majibu. Polisi waliomkamata walikuwa na gari namba T 113 DVU toyota hilux.
Usiku huu RCO Mwanza amedhibitisha @AdvocateSailenc Mwenyekiti CHASO Mwanza anashikiliwa Mwanza Central Police station na anatuhumiwa kwa kuhamasisha maandamano ya July 7, kesho asuubuhi Mawakili wetu watafika kutoa msaada wa kisheria. BAVICHA tutaongea kwa hatua zitakazofuata.
Cc. @FeliusFesto .
Nimepokea taarifa ya kukamatwa kwa SAILENCE MWAKASALA Mwenyekiti wa CHADEMA Student Organization mkoa wa Mwanza mchana huu, Polisi 5 mmoja tu ndiye aliyevalia sare wakiwa na mitutu ya bunduki wamevamia nyumbani kwake na kumchukua kwa nguvu. Tunaendelea kufuatilia kila hatua.
Usiku huu RCO Mwanza amedhibitisha @AdvocateSailenc Mwenyekiti CHASO Mwanza anashikiliwa Mwanza central Police station na anatuhumiwa kwa kuhamasisha maandamano ya July 7, kesho ahsubuhi Mawakili wetu watafika kutoa msaada wa kisheria. BAVICHA tutaongea kwa hatua zitakazofuata.
Nimepokea taarifa ya kukamatwa kwa SAILENCE MWAKASALA Mwenyekiti wa CHADEMA Student Organization mkoa wa Mwanza mchana huu, Polisi 5 mmoja tu ndiye aliyevalia sare wakiwa na mitutu ya bunduki wamevamia nyumbani kwake na kumchukua kwa nguvu. Tunaendelea kufuatilia kila hatua.
REPOST 200
#FreeMwakasala
Serikali iache kuwazuia vijana kuikosoa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa kuwasingizia kuwa wanaleta taharuki. Kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mwananchi ana haki ya kuwa na maoni, kutafuta, kupokea na..
Pamoja na kuwa Tanzania ina haki ya kuwa na mahusiano ya kirafiki na nchi yoyote duniani kwa kadri inavyowezekana, kwa maoni yangu safari ya kuelekea Moscow imefanyika katika wakati ambao si muafaka kisiasa na kidiplomasia.
Katika kipindi ambacho Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini Tanzania, hususan baada ya matukio ya Oktoba 2025, malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wa upinzani, jambo la mwisho ambalo Tanzania ilihitaji ni kutuma ujumbe unaoweza kutafsiriwa kama kuhamisha mwelekeo wake wa kimkakati kutoka kwa washirika wake wakuu wa maendeleo kwenda Moscow.
Tatizo si kwenda Moscow.
Tatizo ni kwenda Moscow wakati Washington na Brussels wanaanza kuhoji mwelekeo wa kisiasa wa Tanzania.
Diplomasia sio suala la hisia; ni suala la muda, mazingira na maslahi ya taifa.
Ukweli ambao hatupaswi kuuficha ni kwamba kwa sasa Russia haiwezi kuchukua nafasi ya Marekani na Umoja wa Ulaya katika maendeleo ya Tanzania.
Takwimu zinaonyesha wazi:
Marekani imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika kipindi cha 2020–2025.
Umoja wa Ulaya umechangia takribani dola bilioni 3.2.
Russia imechangia karibu sifuri katika Official Development Assistance (ODA).
Haya si maoni. Hizi ni takwimu.
Wakati mwingine katika siasa tunajidanganya kwamba washirika wanaweza kubadilishwa kwa urahisi. Historia inaonyesha sivyo.
Marekani na Umoja wa Ulaya hawatoi fedha pekee.
Wamekuwa nguzo muhimu katika:
mapambano dhidi ya UKIMWI na malaria,
chanjo na mifumo ya afya,
elimu,
maji safi,
kilimo,
uwekezaji wa sekta binafsi,
teknolojia,
mafunzo ya wataalamu,
na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.
Pengo litakalotokana na kupungua kwa ushirikiano huo haliwezi kuzibwa kwa picha za viongozi kukutana au mikataba michache ya kisiasa.
Mataifa hayajengwi kwa alama za kidiplomasia; yanajengwa kwa maslahi halisi ya wananchi.
Swali ambalo viongozi wanapaswa kujiuliza si kama tunaweza kuwa marafiki wa Russia.
Swali ni:
Je, Russia inaweza kuchukua mzigo wa afya, elimu, uwekezaji, biashara na maendeleo ambao Marekani na Umoja wa Ulaya wameubeba kwa miongo kadhaa?
Mpaka sasa, jibu la ukweli ni hapana.
Hatari kubwa zaidi si kupoteza misaada.
Hatari kubwa ni kupoteza imani.
Mataifa yanaweza kuishi bila misaada kwa muda fulani.
Lakini ni vigumu kuishi bila imani ya wawekezaji, masoko ya kimataifa, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo.
Fedha za dunia zina tabia moja:
Hukimbilia kwenye utulivu, uwazi wa kisiasa na taasisi zinazoaminika.
Ndiyo maana nchi yenye busara haiharibu madaraja kabla haijajenga mengine.
Na hata kama imeamua kujenga daraja jipya kuelekea Moscow, ni hatari kubomoa madaraja yaliyoiunganisha na Washington na Brussels kwa zaidi ya nusu karne.
Kwa sababu katika siasa za kimataifa, si kila rafiki mpya ana uwezo wa kuchukua nafasi ya rafiki wa zamani.
Na katika wakati ambao Tanzania inahitaji uwekezaji zaidi, ajira zaidi, teknolojia zaidi na masoko zaidi, taifa linapaswa kuwa makini sana lisije likachanganya uhuru wa kidiplomasia na kujitenga kidiplomasia.
Uzalendo wa kweli si kupiga picha na mataifa makubwa; uzalendo wa kweli ni kuhakikisha maamuzi ya leo hayaleti gharama ambazo wananchi wa kawaida watazilipa kesho.
Tunaishi katika zama ambazo watawala weusi hawana hofu ya Mungu tena. Madaraka yamepofusha macho yao. Hawaogopi kutenda dhambi. Wao wanamuogopa mzungu tu. Wanaogopa wakikutoa uhai kikatili wazungu watakata misaada ya kifedha. Wanajua wakimwaga damu ya raia kikatili, benki za mabeberu zinaweza kufunga mdomo wa fedha. Mwananchi wa kawaida? Ni takataka tu machoni kwao. Hawamuogopi mwananchi. Ndiyo maana wanaiba uchaguzi bila hata kuona aibu. Hawategemei kura, wanategemea nguvu, ulaghai na bunduki. Bila mzungu na shinikizo lake la fedha, hawa watawala wengi wangefanya dhuluma za wazi mchana kweupe — wangeua raia bila hofu yoyote. Bila kuwepo kwa jicho hilo la mataifa ya nje, ni wazi kwamba ukatili na unyama unaoshuhudiwa kwa siri ungegeuka kuwa mtindo wa maisha wa mchana kweupe.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inafanya kazi ya kuchochea machafuko.
Sisty Nyahoza aliekwenda kwa marehemu mama Komu na kumshawishi kusaini karatasi ya kufungua kesi ambayo ilifungia chama chetu kufanya kazi siku 309..
Madhara mengine walitaka kukifuta chama kupitia kesi hiyo ya Said Issa.. kwa uwezo wa Mungu tumeshinda..
Sasa Sisty huyo huyo na ofisi hiyo hiyo ambayo inafanya kazi ya kuhujumu chadema usiku na mchana tena wazi kabisa. Inatuandikia barua kila baada ya mkutano na kila neno tunalosema… Maneno pekee tunayoweza kusema tusiandikiwe barua na Sisty ni kumsifia Samia na serikali yake dhalimu ambayo haikuchaguliwa.
Kwa kifupi ofisi ya msajili itaingiza Nchi hii kwenye machafuko ya kisiasa..
Chadema ni taasisi ya Watanzania na Watanzania watailinda dhidi ya hujuma zote.
Leo 29 Mei 2026, ni siku 212 zimepita tangu damu ya watanzania wasio na hatia imwagike kwa risasi za moto 29 Oktoba 2025. Serikali ya CCM inaweza kudhani labda muda umefuta machozi yetu, na ndio maana wanacheka na kupongezana badala ya kuwajibishana. Lakini wamefeli. Jeraha hili liko hai, na mioyo ya wananchi haitasahau kamwe. Hatupigani kwa nguvu zetu wenyewe; tunasimama na haki thabiti ya Mungu ambayo haijawahi kushindwa. Jasho na damu ya raia wenzetu inaililia dunia, na amini nawaambia, dhoruba ya haki inakuja. Kila mkono uliomwaga damu utawajibika. Dunia imesimama nasi, na sauti ya wanyonge haitanyamazishwa tena! #MO29