Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revocatus Chipando (Babalevo) amesema kuwa yeye haamini kuwa yote yanayosemwa na wapinzani ni ya uongo au ya hovyo.
Ameeleza hayo kwenye mahojiano katika kipindi cha Jana na Leo akibainisha kuwa hata mawazo mengi yaliyokuwa yakitolewa na mpinzani wake katika jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe @zittokabwe ameyachukua yale yanayofaa na anayafanyia kazi.
👉Hivi ndani ya JESHI la polisi kuna chipikiz siku hizi?? kama vile ilivyo ndani ya ccm??
👉au huyo mtoto tayari ni polisi? kama ni polisi alisoma lini na muda gani?hebu lifafanueni hili.
👉Sasahivi mpaka polisi mnakazi ya kuwekana nyie kwa nyie watoto wa masikini hata wawe na sifa hawapati ajira hizo kumbe michezo ndo hii.
#KUMBUKIZI‼️ Picha ya Askofu Mwanamapinduzi akiwa na rafiki yake, Alphonce Mawazo, aliyefariki baada ya kuuawa katika Serikali ya Awamu ya Tano, tukio lililoibua simanzi kwa Watanzania na kuleta mjadala mkubwa nchini. Mawazo alifahamika kwa misimamo yake thabiti na kwa kupaza sauti kuhusu masuala ya haki na siasa.
Tutazame kule mbele Asubuhi imekaribia @askofu_mwanamapinduzi
Haya maandamano ni ya muhimu sana na lazma yasukumwe sana na watu ambao mna access na wananchi both online and on the ground.
Watanzania no one is coming to save us. Lazma tujipiganie wenyewe. We have to fight for a new constitution, Tundu Lissu’s freedom, accountability for October 29 massacre. and we have to fight for new free and fair election.
International pressure itasaidia mauwaji kuogopa kuua tena ila the rest of the work Lazma tufaye wenyewe.
Mnaua watu kwa maelfu, Mnateka watu na kuwapoteza. Mnaiba uchaguzi kwa nguvu..
Alafu mnasema kuna watu wanawaonea wivu kwasababu ya rasimali!!!!
Hivi mnawaona Watanzania ni wajinga?
Kwamba Mataifa ya nje ndio yaliwatuma kuiba uchaguzi ambao hamjashinda!!!!
Watu sio sisimizi mmeua lazima muwajibike.
VIDEO:
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametoa hotuba nzito ya kidini inayojikita kwenye imani kwamba ustawi wa kweli wa taifa unategemea msingi wake wa kiroho.
Akifananisha na kile alichokiita asili ya kimungu ya nchi ya Marekani, Gwajima ametoa wito wa kubomolewa kabisa kwa ngome zisizoonekana na maagano ya kale ambayo yanaweza kuwa yanazuia maendeleo ya Tanzania. Lengo kuu ni kubomoa kimfumo madhabahu za kiroho na 'mazindiko' (dawa au kinga za kiasili/kijadi) kupitia nguvu ya imani ili kuhakikisha mustakabali wa haki na wenye ufanisi kwa kizazi kijacho.
Askofu Gwajima amezungumza hayo usiku wa kuamkia leo kanisani kwake mkoani Dar es Salaam katika kile alichokiita siku 40 za upenyo.
ASK RWEYONGEZA "TAFAKARI KAMA TAIFA LETU LINGEKUWA NA VIONGOZI WAAMINIFU, WATU WANGEUSEMA UKWELI BLA KUOGOPA MTU, TAFAKARI VYOMBO VYA HABARI NA WANANCHI WANGESEMA UKWELI TAIFA LINGEKUWA WAPI"
#TAFAKARI
Hivi lini tuliacha mfumo wa Uongozi wa Jamhuri na kuwa wa na uongozi wa kifalme?
Nimeangalia ziara inayoendelea huko Urusi ofcourse tayari najua yanayopangwa huko lakini bado najiuliza maswali mengi sana:-
1. Hivi Abdul, mtoto wa Samia amesafiri kama nani?
2. Anamuwakilisha nani?
3. Anatumia gharama za nani na kwa utaratibu gani?
4. Nani alimpangia protocol ya kuonana na rais wa Urusi?
5. Anawajibika kwa nani na katika mfumo gani?
6. Au hii ni ziara ni ya kifamilia lakini inafadhiliwa na pesa za walipa kodi?
Hili tukio limenifanya niyakumbuke maneno ya Rais mstaafu wa awamu ya pili, hayati Ali Hassan Mwinyi, aliwahi kutoa kauli maarufu mwaka 1993 iliyoeleza kuwa Tanzania ni "kichwa cha mwendawazimu ambapo kila anayejifunza kunyoa hujaribia hapo", najua alikuwa anaongelea michezo kufanya vibaya ila kwa sasa kauli hii inaweza kutumika kwenye siasa kufanya vibaya.
"Hii holelaholela ipo siku itatugharimu".Ndio maana @ChademaTZ2 tunasema Katiba mpya ipatikane kabla ya 2027 kuisha.
#katibaMpyaFreeTunduALissu
#TunawatuTutashinda
Kila nikifikiria kwamba umekaa kwenye kiti cha Umakamu wakati kikiwa kimetapakaa damu za Watanzania wasio na hatia, na unaonekana completely comfortable, nguvu zinaniishia.
Lakini historia inatufundisha mengi. Hata Samia, ambaye leo ameua ma elfu ya watanzania kwa ajili ya Madaraka, aliwahi kupitia manyanyaso makubwa chini ya JPM.
Inasemekana hata camera zilifungwa nyumbani kwake kwa ajili ya kumfuatilia. Kilichotokea baada ya JPM kufariki na yeye kurithi kiti kinapaswa kutukumbusha kwamba tusijisahau sana tukaanza kukuhurumia. Power and privilege can be very intoxicating, madaraka yanalevya.
Hata hivyo, jambo la msingi si nani wa kumhurumia au kumlaumu zaidi. Kikubwa ni kwamba sisi na wewe, iwe sirini au hadharani, tusaidiane kubadili mifumo mibovu inayoendesha nchi yetu ili safety, dignity, na haki za kila raia ziwe guaranteed, bila kujali nani yuko madarakani. Mfumo bora unapaswa kulinda wananchi, si kutegemea wema wa mtu mmoja.