ADO: KWA MIAKA 5 RAIS SAMIA KAKOPA SH TRILIONI 52.6
"Kwa miaka mitano sasa ya uongozi wa Rais Samia, serikali imekopa jumla ya Sh. trilioni 52.6 kati ya hizo Sh. trilioni 28.7 ni mikopo ya msingi na Sh. trilioni 24.56 ni riba. Hii ina maana taifa linaingia kwenye mzunguko wa kukopa ili kulipa madeni ya zamani, badala ya kuwekeza kwa tija kwa wananchi."
Katibu Mkuu wa @ACTwazalendo@AdoShaibu
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Leo katika Uwanja wa Ndege wa @KigomaUjijiMC nimepata fursa ya kuungana na viongozi mbalimbali kumsindikiza Gavana wa Mkoa wa Tanganyika, DRC, Mh. @ChrisKitungwa mara baada ya kukamilisha ziara yake hapa kwetu Kigoma.
Kigoma inaendelea kufunguka kiuchumi na kujidhihirisha kama kitovu muhimu cha biashara ya kikanda.
@mirumbani tupo tayari kuchangia ukuaji huu kwa kutoa huduma bora za usafirishaji, kurahisisha michakato ya forodha, na kuunganisha biashara za ndani na masoko ya kimataifa.
Uongozi (Meya) ni falsafa ya ukaribu ambapo mamlaka yanageuka kuwa huduma, Siasa zinageuka kuwa matendo kuleta maendeleo karibu na wananchi.
Ni njia ya kujenga jamii yenye mshikamano na usawa kwa kila raia hongera #MussaMaulid kwa kuaminiwa kuwa Meya @KigomaUjijiMC
Safari ya mtu ina mwisho, lakini urithi wake hauna mwisho milele, Kesho haitengenezwi na hatua pekee tu, bali na alama tunazoziacha kwa wengine.
Ustahimilivu wenu kwa yale mliyoyapitia katika madhila haya ni shule tosha kwa vizazi vya leo na kesho.
Maisha ni safari yenye utulivu na dhoruba, Yenye njia Laini na Milima vyote ni shule ya uvumilivu.
Maumivu tunayoyapitia maishani hupima imani ya ndoto, Changamoto tunazozipitia pia hufichua thamani ya matumaini, Usikubali kuua ndoto maana kila pumzi uliyonayo ni nguvu ya kesho.
Niliposimama kutazama mawimbi, nimejifunza kuwa maisha ni kama bahari yenye mawimbi na utulivu, ikibeba giza na mwangaza.
Kupitia changamoto tunakua, na kupitia mapumziko tunapata nguvu na kurudi kama awali.
Tumekuwa kama waigizaji kwenye sinema #TheLongWalkMovie tunaumizwa mchana, tunakutana usiku tunaambiwa tusameheane “#Maridhiano”.
Ukweli ni kwamba maridhiano bila uwajibikaji ni kejeli, tuache maigizo.
Natoa shukurani zangu za dhati kwa wanachama @ACTwazalendo na Chama @TanganyikaLaw. Uwepo wenu Mahakamani kufuatilia shauri hili umetupa nguvu, tumaini na faraja kubwa.
Tumeshuhudia kwa macho yetu thamani ya umoja, na tumehisi kwa mioyo yetu uzito wa upendo na mshikamano wenu.
Leo nimekutana #Mashujaa waliobeba mwanga na matumaini ya hatima ya mji wetu.
Mashujaa wetu walikua mstari wa mbele kuhakikisha kila mwana @KigomaUjijiMC anasimama na kusema kupitia kura yake.
Mmehimiza kwa nguvu na ujasiri, Kupiga kura sababu kura zao ni sauti ya mabadiliko.
VIDEO:
Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa na mgombea Udiwani wa chama hicho kata ya Gungu Hussein Baswariyyu, mara baada kumaliza kufanya mkutano na kuomba kura kwa wakazi wa kata hiyo, Oktoba 24, 2025.
Mgombea Ubunge @KigomaUjijiMC@zittokabwe anayo ramani ya kuufufua mji wa kihistoria wa Ujiji kupitia “Ujiji City.” Hatua hii inalenga kuurejesha Ujiji katika hadhi yake ya zamani kama kitovu cha biashara na maendeleo katika Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania.
#ChaguaMwami2025.