Tambua unapoelekezwa Njia na Kichaa pia unaweza fika sehemu husika kwa ufasaha kabisa ila kumbuka lazima utapitia njia yenye Jalala.
UKISHINDWA SEMA TUKUSAIDIE
MAISHA:
MPENDE mtu unaempenda sana lakini acha NAFASI, Na pia MCHUKIE mtu unaemchukia sana ila acha NAFASI
Haijawahi kufanikiwa JAMII yeyote ile Ndani yake hakuna MPUUZI maana Mpuuzi yule Yule ana NAFASI yake wakati fulani kwa JAMBO muhimu kwa UPUUZI wake ule
PAKA HALI KASHATA
FURSA:
FURSA ukishaisikia kwa WATU wengine kama MJADALA hiyo sio Fursa tena
Usiwe MTU wa kukimbizana na kila FURSA unayoambiwa, Wakati mwingine usipokuwa MAKINI wewe ndio wanaokutafuta uwe Fursa yenyewe.
FURSA ni UTEKELEZAJI sio MBOMBELA
NUKUU YA IJUMAA:
Tunasema Uongo kwa sababu hatuna Ujasiri wa Kusema Ukweli, Ukweli hautupi Uhuru, unatupa Upweke
Ukisema ukweli utapata uhuru wa nafsi, Ukisema uongo utapata uhuru wa umma, Heri Uhuru wa Nafsi kuliko wa Umma
SGR UNAKAA MBELE ILA UNAVUTWA NYUMA NA UNAFURAHIA
MANENO wawili ambayo yanamtambulisha mtu mwenye upungufu wa HEKIMA ni haya Mjinga na Mpumbavu.
SISI Tumeshapita katika Ujinga sasa Tunaishi NYAKATI ambazo mwenye uelewa wa jambo analazimika kukaa KIMYA ili asimuudhi MPUMBAVU.
AMBULANCE IPO MAKABURINI.
SIKU TULIVU:
Unapokuwa katika UHITAJI usipende kuchagua mtoa HUDUMA angalia huduma UNAYO PATA.
Wakati Mwingine KICHAA pia anaweza kukuonyesha NJIA ya kufika unapotaka ila UJIANDAE tu kwa kupitia njia lilipo JALALA usijali harufu zingatia LOCATION.
EPUKA NENO "NIJAZIE" NDOTONI
MABORESHO yaliyofanywa na TFF ktk Ligi Kuu Msimu 2026/2027 chini TPLB hasa FVS na MPANGILIO wa Ratiba ni MAENDELEO Endelevu Chanja ila ANGALIZO Kuna TIMU Zisipobadilika kuacha MAZOEA ili kuendana na kukubaliana na hivi vitu Zitapata TABU sana Msimu huu.
MAJI YAMELOWA CHEPECHEPE
KUKOSEA ndiyo mwanzo mzuri wa kujifunza, Unakuwa na FURSA ya Kujifunza kipi kinafanya KAZI na kipi hakifanyi, KUOGOPA Kukosea ndio Mzizi wa kukosa KUJIAMINI.
USIOGOPE Kukosea Maishani, sababu MAISHA hayaji na Maelekezo.
LUKU IMEKATA ILA TAA INAWAKA
Ni WEWE Mwenyewe Ndio Mwenye UAMUZI wa Jinsi ya Watu utakavyotaka WAKUONE, Unavyojiandaa wakati Unaangalia KIOO chako na Unavyojiona ndio WATU Watakavyokuona ULIVYO
UKIANGALIA kwa Kioo chako Ukaona PANYA sawa, Ukaona SIMBA sawa UHALISIA wako unao Wewe na ndio JAMII itavyokuona.
TAFAKURI:
Katika SANAA Ukiona Mchoraji
Amechora PICHA ya Ng'ombe kwenye
Ubao Mzuri halafu baadae akaandika
Maneno pale chini "Huyu ni Ng'ombe"
Ujue kuna TATIZO Ndani yake na Hajiamini kwa KITU anachofanya.
MOTO UMEUNGUA!!
"Mwanamke na Ajifunze katika Utulivu na Utiifu kabisa, Mimi simruhusu Mwanamke Kufundisha wala kuwa na Mamlaka juu ya Mwanamume, lazima Anyamaze” -
1 Timotheo 2:11-12
SIKU NJEMA NYOTE
MAJIBU mengi ya MATATIZO yetu huwa yamo ndani yetu, Tunachokosa huwa ni MASWALI Sahihi katika WAKATI Muafaka ndani ya SEHEMU husika na Au UJASIRI wa Kujiuliza hayo Maswali Sahihi, MAISHA ni kama TAULO Unajifuta Ukitoka KUOGA ila bado linachafuka.
NJOO TUKUPOPOE ONDOKA TUKUSEME
JALALA ni sehemu kwa JAMII inapokea kile ambacho hakihitajiki ili kukihifadhi, Na Umuhimu wake bado linawekwa mbali, maneno ya kejeli 'LICHAFU', linanuka wakati JAMII ndio iliyosababisha hayo, FARAJA moja wapo ni kuona Kuna Jamii (VICHAA) wanalitegemea ktk MAISHA yao kwa chakula.
TRANSFORMATION:
Ili Kuwa vile Unavyotaka ni Lazima Ukubali Kupitia MAUMIVU ya Kubadilika vile Ulivyo sasa.
NGAMIA Kashanyanyuka Anaangalia Jua Linapotokea ili ajue KIBLA ni Wapi.
Ukitaka WATU Waijue THAMANI Yako Kuwa SULUHISHO ya Matatizo Yako Mwenyewe.
Mwenyezi Mungu Ametupa MASIKIO Mawili na Pia ULIMI Mmoja Hivyo Tunatakiwa Kusikiliza Zaidi Kuliko Kuongea.
CHAKULA KIMEPITA NJIA YA HEWA
NUKUU:
Sio kila UKWELI Mchungu ni TIBA, UKWELI mwingine huwasilisha UJUMBE wa chuki ambao MTU amebeba dhidi yako.
"Usidharau Ulichokula Njaa huwa ina tabia ya Kujirudia".
IJUMAA MUBARAK.
Mjasiriamali anauza Nazi Kila Mnunuzi Anaenunua Anachagua Nazi kwa Kugongagonga kupata Nzuri mpaka Zinauzwa Zote
Hivi Zile Nazi Zisizofaa Zilizokuwa Zinaachwa na Wanunuzi ziko wapi au Nazo Zilikuwa Nzuri kwa Wanaofuata ndio maana Zikaisha zote?
NJOO TUKUPOPOE ONDOKA TUKUSEME
Ili kuwa vile Unavyotaka ni Lazima Ukubaki Kupitia Maumivu ya Kubadilisha vile Ulivyo Sasa.
Mbuzi akiwa Katikati ya Simba Asijisahau kuwa Bado Yupo Kwenye Orodha ya Kuliwa.
ELEWA ILI UWAELEWE NDIO MUELEWANE
LEO KITAANI KWETU:
Kwenye MAISHA jambo muhimu sana unalopaswa kuwa nalo ni UVUMILIVU.
Asiyejua MATUMIZI sahihi ya AKILI yake Daima hukitumia KICHWA chake kama KIUNGO cha kubebea MIZIGO isiyomuhusu.
RAHA YA DERA LIGUSE MAUNGONI