"Nafurahi kucheza na Chama na Aziz Ki ni Wachezaji wakubwa, kila Mchezaji anatamani kucheza timu kama Yanga ili ushinde makombe na ilikuwa ni ndoto yangu kucheza timu kubwa sasa nipo hapa kufanya kazi na nilishapitia kipindi kigumu sana na sasa na-Enjoy" Amesema Prince Dube!
Muigizaji mkongwe Bambo amesema hakumzungumia Diamond sababu ya kiki ila alimzungumzia sababu alitaka kutoa kitu Kilchopo rohoni mwake. Aidha Bambo amesema yeye anaishi bila kutegemea kiki yeye anaishi maisha yake toka miaka hiyo mpaka leo hii.
Klabu ya Simba ipo kwenye mpango wa kumtambulisha kiungo wa zamani wa klabu ya Mbuni, Mwadui na Azam Fc, Awesu Ally Awesu akitokea klabu ya KMC. Awesu amekuwa na kiwango bora sana ndani ya kikosi cha KMC kwa msimu uliopita na anaweza kutangazwa na Simba muda wowote kuanzia sasa.
Mke wa Sadio Mané, Aisha Tamba, mwenye umri wa miaka 19, amehitimu masomo ya sekondari miezi minne baada ya kufunga ndoa katika sherehe ya kifahari nchini Senegal.
Aisha aligonga vichwa vya habari baada ya kuolewa na nyota huyo wa Al Nassr mwenye umri wa miaka 32, Januari 2024.
Mwanadada Rose Ndauka amesema ana nyumba mbili moja iko Mwanza na nyingine iko Dar na hizo nyumba amejenga kwa pesa ya uigizaji, Licha ya hayo Rose amesema japo amejenga hizo nyumba lakini bado hakuna nyumba hata moja ya ndoto zake.
Billnass amesema kuwa yeye bado mpangaji bado hajaanza kujenga kwani ndoto zake sio kumiliki mjengo kwasasa, Kuna muda ana anajishangaa maana anamiliki gari ambayo anaweza kununua nyumba, Aidha Billnass amesema yeye ni msanii lazima amiliki gari kali.
Harmonize amesema hakutengeneza Album ya Rais Samia Hassan Suluhu kwa ajili ya mauzo makubwa kwenye platform mbalimbali, Harmonize anasema alitengeneza Album hii kwa ajili ya Watanzania kuelewa na kujua miladi mbali mbali ambayo Mama Samia anafanya kwenye Taifa letu.
Mwamamuziki Harmonize amefunguka kuwa million moja ikimpata mtu mwenye akili Ya utafutaji ni mtaji tosha wakubadili maisha, Pia Harmonize amesema muda ambao anajitafuta alikuwa anaishi kwenye chumba cha 15k na alikuwa na biashara ya mtaji wa laki moja na nusu.
Mwanadada Irene Uwoya amewajibu wale wanaosema kuwa hawezi kuwa mchungaji sababu ana tattoo, Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Uwoya amesema "Mnaotaka nifute tatoo Mungu haangalii tatoo anaangalia matendo"
Uongozi wa Simba umeanza mazungumzo na Sporting Lagos FC ili kupata saini ya winga fundi wa kikosi hicho, Jonathan Alukwu ikiwa itashindwa kumpata Elie Mpanzu kutoka AS Vita, Alukwu mwenye miaka 21, anacheza FC Heart-land inaelezwa Simba wanajaribu kumshawishi ili ajiunge nao.
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji Mwanadada Wema Sepetu amesema kwasasa watu wasimchukulie poa kwani hataki tena kualikana kwenye mambo vya vibao kata, Pia Wema amesema mtoto yayote akitaka kuonana nae au kikao basi sehemu kama Ngorongoro hivi nasio kwenye mabar.
Inaelezwa kuwa Golikipa namba moja ya klabu ya Simba Aishi Manura aliomba kuondoka klabuni hapo na ili ajiunge na Azam Fc, Lakini Taarifa zinasema kuwa Raisi wa heshima Mo Dewji alikataa ombi hilo na kumtaka kipa huyo kubaki klabuni hapo.
“Sasa hivi pia dunia imebadilika tupo katika dunia ya umoja na usawa ingawa siamini kwenye hilo, mimi siamini kama mwanamke na mwanaume wanaweza kuwa sawa naamini mwanamke anaweza kuwa mkubwa zaidi ya mwanaume au mwanaume anaweza kuwa mkubwa zaidi ya mwanamke” Elizabeth Michael
Mwanadada Monalisa amesema ningumu Tanzania kuwa bilionea au kuwa msanii mkubwa na dunia kumjua
“Kwa mfano mimi nina takribani miaka 26 kwenye tasnia lakini wenda ningekuwa mbele ningekuwa bilionea sana ila hapa ndiyo kama hivi nilivyo sio rahisi kuwa msanii bongo” Monalisa
Msanii Duma amefunguka kuwa ni fahari kwake kukutana na mwanamke bikra kwenye kizazi hiki hata Alipoamua kuandika hivyo mitandaoni ilikuwa ni moja ya njia Ya kuonesha watu yuko proud kukutana na mwanamke bikra, Duma pia amesema mwanamke huyo bikra ndio mwanamke wake wamaisha.
“Sijawahi kuandikiwa na msanii wa kizazi kipya ila tukikutana kwenye session huwa napokea mawazo, Nimekua nikisikia lawama za watu kuwaandikia watu nyimbo ila hawapokei credit yoyote. Binafsi sioni kama ni shida kumpa mtu credit kama amekuandikia wimbo” ~ Joh Makini
“Nimeona wachezaji ambao klabu imewatangaza. Binafsi inanipa moyo kuuona msimu ujao itakuwa zamu yetu kunyakua mataji ambayo tuliyakosa msimu uliopita. Ukiachana na umri wao kiufundi ni wachezaji wazuri, ndio maana Simba ikawapa nafasi ya kuja kutumika ndani ya kikosi,” Ngoma.
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga raia wa Zambia Kennedy Musonda anaelekea kujiunga na klabu ya Tp Mazembe ya Congo DR. Hii Swap deal baina ya Jean Baleke kutua Young Africans na Kennedy Musonda kutua Tp Mazembe mazungumzo yamekamilika tayari