Ninayajua maumivu ya kushindwa kulipa ada maana nishawahi yapitia na ikanibidi nikae mwaka mmoja nyumbani huku wenzangu wakiendelea na masomo๐
Ni jambo linaloumiza sana lakini watanzania ni watu wema sana mimi nilipokosa ada mitandao ilitumika kupaza sauti nikachangiwa ada na kuendelea na masomo na watu ambao wengi hatujawahi hata kukutana nao.
Hivyo basi kwa unyenyekevu mkubwa sana naomba tumsaidie huyu mdogo wetu kupata ada ili aweze kufanya mitihani yake.
Nawaombeni ndugu zangu tufanye kwa moyo wa upendo kabisa na Mwenyezi Mungu atatubariki sana๐
Natanguliza shukrani๐