Kweli ya mwisho na muhimu ni kwamba ndani yako una nguvu kubwa, nguvu inayoendesha ulimwengu, nguvu ya asili ipo ndani yako, ukiweza kuifikia na kuitumia utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8:18
Jenga utambulisho wako ili usije ukapotelea kwenye mifuko ya wengine.
Kua na tabia ambazo zinakutambulisha na kukutofautisha na wengine.
Kuwa na kanuni zinazokuongoza na uzifuate.
Usipelekeshwe na mkumbo
Bidii yako na maarifa yako vitakukutanisha na bahati yako.
Uvivu utakupishanisha na bahati yako.
Hii ni kusema kuwa mtu anajitengenezea bahati yake mwenyewe.