Hello Weekend Hustler 🫵
Want a chance to win 5️⃣0️⃣0️⃣ USDT with our Weekend Quiz?
All you gotta do is ...
1. Follow @OKX
2. RT + comment your answer below
Have a go!👇
Habari familia ya BitcoinSafariTz,
Kwa sasa tumesitisha huduma zetu hadi wiki ijayo ili kutoa heshima na maombi kwa ndugu zetu waliopoteza maisha wakipigania uhuru, amani na demokrasia nchini mwetu. Mungu awalaze mahali pema na awape faraja familia zao.
Trading is like going to school. You spend years studying before you get the high-paying job.
The problem is that most traders want the paycheck before doing the learning...
That’s why they drop out early and lose.
Learn first. Earn later. That’s how you succeed in trading.
Bitcoin Halving ni nini?
Bitcoin halving ni tukio linalotokea kila baada ya takriban miaka minne, ambapo zawadi (reward) ya Bitcoin wanayopata wachimbaji (miners) inapungua kwa nusu (50%). Hii ni sehemu ya mfumo wa Bitcoin uliowekwa na muundaji wake, Satoshi Nakamoto, ili kudhibiti usambazaji wa Bitcoin na kulinda thamani yake dhidi ya mfumuko wa bei.
Inavyofanya Kazi:
Wakati wachimbaji wanathibitisha muamala (transaction) kwenye mtandao wa Bitcoin, wanazawadiwa Bitcoin mpya. Mwanzoni walikuwa wakipata 50 BTC kwa kila block, lakini halving za awali zimesababisha kupungua kwa kiwango hiki:
- 2009: 50 BTC
- 2012: 25 BTC (halving ya kwanza)
- 2016: 12.5 BTC
- 2020: 6.25 BTC
- 2024: 3.125 BTC
Halving inayofuata inatarajiwa kufanyika 2028.
Faida za Bitcoin Halving:
1. Kudhibiti mfumuko wa bei (inflation): Kwa kupunguza kiasi cha Bitcoin mpya zinazotengenezwa, halving huzuia mfumuko wa bei kama ilivyo kwenye sarafu za kawaida zinazochapishwa kiholela.
2. Kuongeza thamani: Mara nyingi, halving huambatana na ongezeko la bei ya Bitcoin kwa sababu usambazaji unapungua lakini mahitaji yanaongezeka.
3. Kuchochea matumizi ya teknolojia ya Bitcoin: Halving huleta hamasa kwa jamii kujifunza na kuwekeza zaidi kwenye Bitcoin.
Mfano Hai:
Fikiria dhahabu. Kadri inavyokuwa ngumu kuipata, ndivyo thamani yake inavyopanda. Vivyo hivyo, Bitcoin inazidi kuwa adimu (scarce) kila halving. Mwaka 2020 kabla ya halving, BTC ilikuwa karibu 8,000. Baada ya halving, ilifikia zaidi ya 60,000 mwaka uliofuata.
Bitcoin halving ni sehemu muhimu ya mfumo wa Bitcoin wa kuhakikisha kuwa BTC inabaki kuwa sarafu ya kidigitali yenye thamani na isiyodhibitiwa na mtu au taasisi. Ni tukio muhimu kwa wawekezaji, wachimbaji, na watumiaji wa Bitcoin kote duniani.
Cheza na Crypto kwa Akili
1.Usitumie leverage, Fanya biashara kwa pesa zako halisi. Leverage inaweza kukuua kimya kimya. Ukikosea kidogo tu, unachoma.
2 Usingie kwa FOMO Usinunue coin kwa sababu tu watu wanasema “inapanda sasa hivi.” Tulia, fanya utafiti wako mwenyewe.
3 Shikilia coin 3-5 kuu tu Usiwena coin nyingi sana. Bora coin chache unazozielewa vizuri kuliko nyingi usizojua zinafanya nini.
4 Hifadhi crypto zako mwenyewe Usiziache kwenye exchange. Tumia wallet yenye private keys zako. “Not your keys, not your coins.”
5 Degen bag isiwe zaidi ya 10% Kama unapenda kucheza na miradi ya hatari, weka pesa kidogo tu. Ukiipoteza, usiumie.
6 HODL muda mrefu Faida halisi inakuja kwa subira. Crypto nzuri haipandi mara moja, inajijenga taratibu.
7 Zoom out Acha kuangalia chart kila dakika. Angalia picha kubwa ya miezi na miaka, ndipo utaona mwendo halisi.
8 Tegemea kushuka mara kwa mara Kushuka 30–35% ni kawaida kabisa. Usipanic, hayo ni mapumziko ya soko.
9 BTFD 😎 Kama una imani na mradi, nunua zaidi wakati bei ziko chini. Hapo ndipo watu wenye akili huongeza holdings.
DFTU – Don’t Forget To Understand
Kabla ya kufanya chochote, elewa unachofanya. Crypto siyo mbio, ni safari, subira na nidhamu.
To survive a full Bitcoin cycle…you need the brain of a philosopher,
the patience of a monk,
and the pain tolerance of a psychopath.
Only a few truly make it through.🔥🙌