G-55, Mandela, na Safari ya Kujisafisha Chadema: Tunakoelekea Ndiyo Tunakostahili Kuwa
Kitendo cha kundi la G-55 kujiondoa ndani ya CHADEMA kimeniamsha fikra juu ya jambo la msingi sana kuhusu uhai wa vyama vya siasa—kuwa si kila msongamano ni mshikamano, na si kila idadi ni nguvu halisi.
Nilijikuta nikikumbuka mwaka ambao CHADEMA, chini ya Katibu Mkuu wa wakati huo, Dkt. Wilbrod Slaa, ilifanya mikutano kadhaa ya ndani. Wakati huo huo, Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Wilaya ya Ubungo lilikuwa na kongamano maalum katika Ukumbi wa Landmark Hotel. Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Miongoni mwa wazungumzaji wakuu alikuwa Mwanasheria wa chama—Tundu Antipas Lissu.
Katika hotuba yake, Lissu alitumia mfano wa kihistoria kutoka Afrika Kusini, akimnukuu Nelson Mandela na harakati za ANC dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid). Mandela, kwa mujibu wa Lissu, alikuwa mkali sana katika kuhakikisha kuwa mapandikizi yote ndani ya ANC—Waafrika waliokuwa wakifanya kazi kwa maslahi ya serikali ya Makaburu—yanang’olewa bila huruma. Hili liliwezesha harakati za ukombozi kuwa safi, imara na za kweli.
Lissu alisisitiza kuwa CHADEMA pia ilikuwa inapitia kipindi kama hicho: mapambano dhidi ya mfumo dhalimu hayangefanikiwa ikiwa chama kingeendelea kubeba mizigo ya watu walioko ndani lakini roho zao ziko nje. Kwa wakati huo, aliyekuwa kinara wa tuhuma hizo alikuwa Zitto Kabwe.
Leo hii, tukirejea msimamo wa #NoReformNoElection (NRNE)—ambao ndiyo dira ya sasa ya chama—ni dhahiri kuwa Tundu Lissu, akiwa Mwenyekiti, ameendeleza kwa ujasiri falsafa ile ile: CHADEMA lazima kijisafishe. Lakini tofauti na kutumia nguvu au vurugu, chama kinajenga mazingira ya ndani ambayo yanawalazimisha wenyewe kujiondoa. Wamejitoa kwa hiari, lakini si kwa bahati mbaya—ni kwa sababu ya moto wa misimamo ya kweli.
Katika mazingira ya sasa ya kisiasa nchini Tanzania, CHADEMA ndicho chama pekee chenye upinzani halisi dhidi ya CCM na dola, na kinachobeba matumaini ya mamilioni ya Watanzania. Kwa hali hiyo, ilitarajiwa kuwa moja ya mikakati ya kimya ya dola ni kuvuruga chama hicho kutoka ndani kwa kupandikiza watu wa kuharibu dira na mshikamano wake.
Kwa mantiki hiyo, programu ya NRNE imekuwa kama nyoka anayejivua gamba—kujisafisha kwa njia ya asili. Kujiondoa kwa G-55 si pigo; ni neema. Ni hatua ya kuongeza usafi wa chama. Ni hatua ya kujenga msingi imara wa chama cha watu, si cha nyadhifa.
CHADEMA haipaswi kuwa chama cha wenye kiu ya ubunge, udiwani au uwakilishi. Inapaswa kuwa chama cha watu wanaoamini katika mabadiliko ya mfumo, hata kama wao hawatanufaika binafsi. Chama hiki kinahitaji watu walio tayari kupigania maslahi ya umma hata kama haitaleta faida kwao binafsi.
Kwa hiyo, kujiondoa kwa G-55 ni baraka kwa CHADEMA—ni nafasi ya kuimarika, kupendwa zaidi na kuvutia maelfu ya Watanzania walio nje ambao wanatafuta nyumba ya kisiasa ya kweli, siyo ya mahesabu binafsi. Ni nafasi ya chama kuwa chama cha watu wa aina ya Lissu—wanaoishi mbele ya muda.
CHADEMA inaendelea kuwa mwanga wa matumaini, na kuondoka kwa wale waliokuwa kivuli tu kumeifanya iangaze zaidi.
Anderson Ndambo
Mtetezi wa Haki za binadamu na Mchambuzi huru.
@EliabuDanford SIO KWELI:
Mwili ndio nafsi. 1Pet3:20 inasema ktk gharika ya noah walipona nafsi nane.
Pia kuna maandiko mengi yanayoita mwili kuwa nafsi.
Hata Ezekiel 18:4 inaonyesha nafsi inakufa.
Roho ni uhai tulio nao. Ni kama umeme ndani ya Tv ikiwa hautakuwepo itazima.
Swali la mwisho kwa leo:
Kesi ya MHAINI wanashindwa kuiendesha kwa UWAZI hapo Kisutu (open court) kwa KUOGOPA wananchi, je UCHAGUZI wa 🇹🇿 nzima mtaweza?
HILI NI SHAMBULIO DHIDI YA UTAWALA WA SHERIA.
Nimeshtushwa Mno na Shambulio la kikatili linalokosa misingi ya Utu na lisiloweza kuelezeka mbele ya Jamii yeyote uenye watu Timamu
Ni msingi wa Kisheria na Kikatiba kwamba
1. Mahakama ni chombo huru kinachopaswa kufanya kazi bila mashinikizo, vitisho au uingiliaji wowote kutoka kwa vyombo vingine vya dola. Polisi kuzuia wananchi kuhudhuria kesi ni sawa na kudhibiti mazingira ya kimahakama kinyume na katiba.
Na wajibu huu unatakiwa kulindwa na Mahakama yenyewe kupiti Hakimi anayeendesha kesi husika.Lazima Haki ionekane ikitendeka
2. Wananchi wana haki ya kikatiba ,Kisheria na kidemokrasia ya kushuhudia mwenendo wa mashauri mahakamani, ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji.
Kuzuia haki hii bila kuwepo kwa msingi wa kisheria wala kikanuni na kutafuta njia mbadala zinazo zuia haki ya wananchi kushujudia na Kuona Haki Ikitendeka ni kuzuia ushiriki wa umma katika mchakato wa haki.
3.Wananchi wakikusanyika kwa amani kwenda kushuhudia kesi, basi kuwakamata au kuwaumiza na muwatupa porini ni ukiukaji wa haki yao ya kikatiba ya kukusanyika na kujieleza.
TLS tumekuwa tukisisitiza na kukemea ukiukaji huu wa sheria na matumizi mabaya ya kisheria.
Tuneielekeza Kamati ya TLS kukaa na kuona namna bora ya kushughukikia jambo hili kwa uzito na njia zinazostahiki.
Tunatoa pole kwa wahanga wote wa vitendo hivi vya kikatili vilivyotendwa dhidi yao na pia tuna washauru
1.Kwenda Polisi Mara moja wapatiwe PF 3 ni haki yao.
2.Wale wanaokataliwa wawekeke kumbu kumbu kumbu ya barua au ushahidi husika ikiwemo picha na Madhila waliyo pata.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivi na kuonekana kuanza kuota mizizi na kuzoeleka TLS itaona namna bora ya kushirikiana na wahanga katika kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa taasisi na kila muhusika kwa jina lake kuona namna kamilifu ya kushughulikia jambo hili baada ya kupata Taarifa kamili kutoka kwa Kamati husika.
BAK Mwabukusi
President - TLS.