Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa itakayoanza tarehe 3 hadi 5 Juni, 2026 kwa mualiko wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Mheshimiwa Vladimir Putin
WILAYA YA HANANG-MANYARA
Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi ameanza ziara mkoa wa Manyara kwa kutembelea Mabalozi na kufanya vikao vya shina,Kukagua miradi ya Maendeleo na Kufanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Hanang mkoani humo.@kenanikihongosi@ccmtanzania #Kazinaututunasongambele
#Ziara inaendelea Kesho Babati Mjini.
JK AKUTANA NA BI. CATHERINE P. CONRAD MINJA, NI MSICHANA ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA MAFANIKIO KATIKA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI (MOI) MIAKA 18 ILIYOPITA
Asubuhi ya Ijumaa, Novemba 14, 2008 Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, alisimama kwa muda kando ya kitanda cha binti mdogo Catherine P. Conrdad Minja mwenye umri wa miaka minne katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI), akimsabahi na kumtakia nafuu ya haraka baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo, akiwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika Taasisi hiyo.
Jioni ya Ijumaa Mei 29, 2026 - yaani leo - Rais huyo mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mara nyingine na Catherine P. Conrad Minja ambaye Julai 19 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 22 , ikiwa ni miaka 18 toka walipoonana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo.
Catherine hivi sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akisomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Kairuki jijini Dar es salaam, alifika ofisini kwa Rais Mstaafu kumsabahi na kumshukuru kwa juhudi zake za kuanzisha na kusimamia taasisi za magonjwa ya moyo.
Dkt. Kikwete amempongeza Catherine kwa kuchagua masomo ya udaktari kama alivyomuahidi miaka 18 iliyopita, na amefurahi kumuona mmoja wa wagonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji Taasisi ya MOI ambayo ni moja ya taasisi za rufaa zinazoongoza Afrika Mashariki katika kushughulikia kesi ngumu za magonjwa na majeraha ya mifupa, misuli, viungo, ubongo na mfumo wa fahamu.
Catherine amemwambia Rais Mstaafu kwamba angependa kuwa Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo huko mbeleni, ili asaidie watu wenye shida hiyo iwe kama shukrani zake kwa Mungu kwa kuwezesha apone na kuendelea kuishi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea Taarifa ya Sensa ya Wanyamapori iliyofanyika nchi nzima mwaka 2024 – 2025 iliyowasilishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, tarehe 29 Mei, 2026 Ikulu Dar es Salaam.
WAZIRI MKUU AKUTANA NA PROF. JANABI BRAZZAVILLE
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika (WHO AFRO), Profesa Mohamed Janabi ambapo walijadili masuala mbalimbali ya maendeleo, hususan ushirikiano katika sekta ya afya barani Afrika.
Pia, Dkt. Mwigulu alikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Mbundi pamoja na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Afrika (FP-ICGLR), Balozi Dkt. Deo Mwapinga.
Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unaoendelea jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo leo Jumatano Mei 27, 2026.
Standard Chartered Tanzania yaandaa Kikao cha Ushauri na Ulezi Shule ya Sekondari ya Pugu Boys.
Standard Chartered Tanzania, kupitia programu yake ya Kujitolea kwa Wafanyakazi (Employee Volunteering – EV), iliandaa kikao cha ulezi na ushauri katika Shule ya Sekondari ya Pugu Boys tarehe 23 Mei 2026, kikihusisha zaidi ya wanafunzi 150 katika uzoefu wa kujifunza wa mwingiliano na wenye manufaa makubwa.
Kikao hicho kilijumuisha mada mbalimbali muhimu zikiwemo elimu ya fedha, nidhamu, maendeleo ya tabia, mwongozo wa taaluma, pamoja na namna ya kukabiliana na ushawishi hasi. Lengo la mpango huu lilikuwa kuwapatia wanafunzi stadi muhimu za maisha, kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na kujenga msingi imara kwa mustakabali wao.
Katika kikao hicho, wafanyakazi wa Standard Chartered Tanzania walishiriki maarifa ya vitendo pamoja na uzoefu wao binafsi ili kuwahamasisha wanafunzi kuchukua jukumu la maendeleo yao binafsi, ustawi wa kifedha, na matarajio yao ya taaluma. Ushiriki huu ni sehemu ya juhudi pana za Benki katika kusaidia maendeleo ya vijana na uwezeshaji wa jamii.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Bw. Herman Kasekende, Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Banking & Coverage, alisisitiza umuhimu wa ulezi na kuwa mfano bora kwa vijana:
“Mtoto wa kiume ni muhimu sana kwangu, na kuwalea kupitia ushauri ni jambo ambalo nina shauku kubwa nalo. Kila mmoja wetu ana jukumu muhimu katika kuunda kizazi kijacho cha wanaume — watu ambao watatoa mchango chanya kwa jamii.
Natumaini mtapata mafunzo yenye thamani kutoka katika mjadala wa leo — iwe ni kuelewa jinsi ya kusimamia fedha zenu (si mapema sana kuanza), kukuza ujuzi sahihi wa kufanikiwa katika taaluma zenu, au kuweka kipaumbele katika afya yenu ya akili na mwili, pamoja na mafunzo mengine ya maisha.”
Kikao hicho cha ulezi na ushauri ni sehemu ya programu endelevu za Kujitolea kwa Wafanyakazi za Standard Chartered Tanzania, ambapo wafanyakazi hutenga muda wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii zenye athari chanya kama vile upandaji miti, usafi wa fukwe, mwongozo wa taaluma, na programu za elimu ya fedha.
Kupitia mipango hii, Benki inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuendeleza biashara na ustawi kwa kuwekeza katika jamii na kuwawezesha vijana wa kizazi kijacho.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza kuwakamata raia wanne wa Kichina kwa tuhuma za ujambazi na utekaji kwa wafanyabiashara wa Kichina nchini. @PolisiTanzania
*DKT. MWIGULU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA CONGO BRAZAVILLE*
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo (Jumatatu, Mei 25, 2026) kwenda Brazzaville, Jamhuri ya Kongo kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Mkutano huo utafanyika Mei 26 – 27, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kintele jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.
Mkutano huu ni jukwaa muhimu la majadiliano ya kimkakati kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya dunia, yakihusisha nchi wanachama, taasisi za kikanda na kimataifa ambalo linahusisha kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali za fedha ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika na kuimarisha uwezo wa bara kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kifedha duniani.
Mkutano huo utawakutanisha wajumbe wapatao 3000 ikiwemo Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika, Watunga Sera, wafanyabiashara, Taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo, Wajasiriamali pamoja na Wawekezaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Kigali, Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) tarehe 19 Mei, 2026.
Mkutano huo wa Kimataifa unawakutanisha pia wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya kimataifa, ambapo utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Mkutano huo pia unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela katika makazi yake Kilimani Jijini Dodoma leo tarehe 13 Mei 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam wakati akitokea nchini Uganda ambapo alihudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Jijini Kampala, tarehe 12 Mei, 2026.
Ruth Zaipuna Kuipeleka NMB Jukwaa la Kimataifa Cambridge.
Katika hatua muhimu kwa sekta ya benki nchini na uongozi wa taasisi za kibiashara barani Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ruth Zaipuna, anatarajiwa kuzungumza katika Cambridge Africa Business Conference 2026, utakaofanyika Mei 30, 2026 katika Chou cha Biashara cha Cambridge Judge chini ya Chuo Kikuu cha Cambridge Uingereza.
Katika jukwaa hilo, Zaipuna anatarajiwa kutoa hotuba kuu kuhusu safari ya mageuzi ya NMB na mchango wake katika uchumi wa Tanzania, akieleza namna benki hiyo ilivyokua kutoka katika mizizi ya huduma ndogo za fedha hadi kuwa moja ya taasisi zinazoongoza katika sekta ya fedha nchini.
Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Kujenga Mustakabali wa Afrika: Mitaji, Ubunifu na Ukuaji wa Kiwango cha Bara,” unalenga kujadili nafasi ya Afrika katika kuchochea ukuaji kupitia mitaji, ubunifu na uwezo wa taasisi za Afrika kufanya kazi kwa kiwango cha bara, hususan katika mazingira ya AfCFTA.
Akizungumzia mwaliko huo, Zaipuna alisema ni heshima kwa NMB na Tanzania, akibainisha kuwa safari ya benki hiyo inaonesha kuwa taasisi zinazoongozwa na Waafrika zinaweza kujenga ubora wa kiwango cha dunia huku zikibaki karibu na mahitaji ya wananchi, biashara na vipaumbele vya taifa.
*Mwisho*
RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUELEKEA UGANDA KUHUDHURIA SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS MUSEVENI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Uganda kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni tarehe 12 Mei, 2026.
STANDARD CHARTERED YAANDAA TUKIO MAALUM LA KUTAZAMA MECHI KWA KLABU YA MASHABIKI WA LFC NA WATEJA WAKE.
Standard Chartered Tanzania iliandaa tukio maalum la kutazama mubashara mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ya Ligi Kuu England kati ya Liverpool FC na Chelsea FC siku ya Jumamosi, tarehe 9 Mei 2026.
Tukio hilo lililofanyika Bravo Coco jijini Dar es Salaam, liliwakutanisha wanachama wa Klabu ya Mashabiki wa Liverpool FC nchini pamoja na baadhi ya wateja wa Standard Chartered kwa alasiri ya kipekee iliyojawa na burudani ya soka, urafiki na mshikamano wa kijamii.
Tukio hili lilikuwa sehemu ya dhamira endelevu ya Benki ya kuimarisha mahusiano na wateja wake pamoja na kusherehekea ushirikiano wake wa kimataifa na Liverpool FC kwa njia yenye maana kwa jamii ya hapa nchini.
Eneo la tukio lilipambwa kwa mandhari ya kuvutia yaliyochochewa na uwanja wa Anfield, yakiambatana na mapambo maalum, maswali ya maarifa kuhusu klabu, pamoja na zawadi zenye nembo — yote yakilenga kuboresha uzoefu wa watazamaji na kuenzi mapenzi ya mashabiki wa Liverpool nchini Tanzania.
“Soka lina namna ya kipekee ya kuwaunganisha watu, na tunafurahia kuunda nyakati zinazotuunganisha na wateja pamoja na jamii zetu nje ya shughuli za kibenki. Tunathamini fursa zinazotuwezesha kuhusiana zaidi ya huduma za benki, kuimarisha mahusiano na kuunda kumbukumbu nzuri na jamii tunazozihudumia,” alisema George Binde, Afisa Mkuu wa Fedha wa Standard Chartered Bank Tanzania.
Standard Chartered inaendelea kutumia ushirikiano wake wa kimataifa katika michezo kujenga mahusiano ya kudumu na kutoa thamani ya kipekee kwa wateja na jamii katika masoko yake mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuph Makamba katika makazi yake Tegeta Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Mei 2026.
Benki ya Exim Tanzania Yapanua Huduma zake kwa Kufungua Tawi Jipya Geita
Benki ya Exim Tanzania imezindua rasmi tawi lake jipya mkoani Geita, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wateja wa eneo hilo, hususani wanaofanya shughuli ndani ya mnyororo wa thamani wa sekta ya madini pamoja na wakulima, wafanyabiashara wadogo na wa kati.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde pamoja na viongozi wa Serikali, wadau wa sekta ya madini,wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde alisema:
“Sekta ya madini inaendelea kuwa nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Uwepo wa taasisi za kifedha kama Benki ya Exim hapa Geita utaongeza upatikanaji wa mitaji na kuwawezesha wachimbaji pamoja na wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi,” alisema.
“Hatua hii inaendana vizuri na jitihada za Serikali kuhakikisha manufaa ya sekta ya madini yanawanufaisha Watanzania wengi zaidi,” aliongeza.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Jaffari Matundu alisema tawi hilo jipya linaakisi dhamira ya kimkakati ya benki hiyo ya kusogeza huduma za kifedha karibu na maeneo yenye ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi.
“Geita ni kitovu muhimu cha shughuli za kiuchumi kinachoendeshwa na sekta ya madini pamoja na biashara zinazoiunga mkono. Kupitia tawi hili, tunalenga kutoa huduma za kifedha zilizo salama, rahisi kufikiwa na zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu, kuanzia wachimbaji wadogo hadi wafanyabiashara wakubwa,” alisema.
Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa suluhisho za kifedha zinazochochea ukuaji wa biashara na kuongeza ushirikishwaji wa kifedha nchini.
“Wajibu wetu unaenda zaidi ya huduma za benki. Tupo kama mshirika wa muda mrefu katika ukuaji wa biashara na maendeleo ya jamii,” aliongeza.
Kama sehemu ya dhamira yake ya kuisaidia jamii kupitia programu ya Exim Cares, benki hiyo pia ilitoa msaada kwa Hospitali ya Manispaa ya Geita kufuatia changamoto zilizobainika katika utoaji wa huduma za afya ya uzazi, watoto wachanga pamoja na huduma za dharura katika eneo hilo.
Msaada huo unatarajiwa kuimarisha uwezo wa hospitali kutoa huduma kwa wakati, kuboresha mwitikio wa huduma za dharura kwa wagonjwa mahututi, na kuchangia matokeo bora ya afya kwa kina mama, watoto wachanga na jamii ya Geita kwa ujumla.
Akizungumzia msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki kwa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Andrew Lyimo alisema:
“Tunaamini ukuaji wa kifedha lazima uende sambamba na ustawi wa jamii. Mchango huu ni sehemu ya jitihada zetu pana za kuunga mkono huduma muhimu za kijamii na kuboresha maisha ya wananchi.”
Tawi la Geita ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Exim wa kupanua uwepo wake katika maeneo muhimu ya kiuchumi nchini Tanzania. Katika safari hii ya ukuaji, benki hiyo imeendelea kuongeza mtandao wake katika maeneo yenye fursa kubwa za biashara, ikiwemo maeneo ya utalii na ukarimu kama Paje Zanzibar, huku ikiendelea kuhakikisha biashara na jamii zinapata huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji yao pamoja na huduma za kisasa za kibenki.
Ikiendelea kuimarisha dhamira yake ya kusaidia ukuaji wa biashara, Benki ya Exim imeendelea kuanzisha suluhisho mbalimbali zinazojibu mahitaji yanayobadilika ya watu binafsi na biashara katika sekta tofauti. Kutokana na ongezeko la mahitaji ya huduma za mikopo ya magari na uendeshaji bora wa biashara, hivi karibuni benki hiyo iliingia katika ushirikiano wa kimkakati na Toyota Tanzania Limited unaolenga kurahisisha umiliki wa magari kwa watu binafsi na biashara.
Benki hiyo pia imeendelea kuimarisha huduma zake za ufadhili wa mnyororo wa ugavi(supply chain) ili kusaidia biashara katika sekta mbalimbali kupata mtaji wa uendeshaji na kuongeza ufanisi wa shughuli zao. @Exim_BankTZ
Blue Ticks, Red Flags & a Cold Gin: Somo Kutoka Gordon’s & Tonic.
Dating siku hizi? Hapana… hiyo ni full-time job ambayo haina contract.Unapambana na kazi mchana, usiku unapambana na feelings.
Mtu anakutumia “good morning babe” leo, kesho anakuacha kwenye blue ticks kama umetuma application ya kazi. No response. No update. Hakuna hata “seen with respect.”
Unajiuliza: shida iko wapi? Kadri unavyofikiria, ndivyo unachoka zaidi.Ukweli ni huu—mahusiano mazuri si rahisi. Na consistency? Hiyo ni luxury.
Watu wanabadilika. Mood zinabadilika. Kitu pekee kinachobaki consistent ni confusion… na machozi ya kiwango cha juu kidogo.
Halafu kuna vitu vingine vidogo vinavyokuja kuku-save. Kama baridi ya jioni baada ya siku ndefu.
Kama funda la kwanza la kinywaji kilichotengenezwa vizuri kwa ustadi. Gordon’s Premix Cocktail waliinielewa kidogo hapo.
Unajua ile feeling ya kufungua kitu, na unajua kabisa kitakuwa sawa?Hakuna masuala ya kukisia. Hakuna “leo itakuwaje?”
Gordon’s Premix ni perfectly mixed. Tamu. And always consistent.
Tofauti na baadhi ya watu—hii haina mixed signals. Baada ya siku ya emails zisizoisha na chats zisizojibiwa, unahitaji kitu ambacho hakikuchoshi kufikiria.
Hakuna “tonic imeisha.” Hakuna “subiri kidogo.” Hakuna drama.Unachofungua, ndicho unachokipata.
Na labda hapo ndipo somo lilipo. Especially ikiwa baridi na mvua hizi zinazoendelea.
Consistency sio kelele. Sio promises nyingi.
Ni ile hali ya kujua—hata bila kuuliza—kila kitu kiko sawa.
Watu watafanya ugumu uwe mgumu zaidi.
Lakini angalau, si kila kitu maishani kinahitaji effort hiyo.
Vingine… vinafanya tu kazi.
Kama ile cocktail in a bottle, Gordon’s Premix.
@Gordon's_ea
#PerfectPair #YouMeAndGordonsTonic