Askofu Mkuu, Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwaichi amesema kwa yanayoendelea nchini kwasasa hatupaswi kujiita Kisiwa cha Amani
“Tupende kushughulikia mambo yetu kwa msingi wa ukweli zaidi, msingi wa haki, msingi wa amani na msingi unaompendeza Mungu. Kusudi tuweze kweli kudai kwamba sisi ni kisiwa cha amani, katika yale yanayoendelea zama hizi katika nchi yetu, nashauri tusithubutu kujiita kuwa ni kisiwa cha amani. Tusithubutu kujitanabaisha kama kisiwa cha amani”____ amesema Askofu Yuda Thadeus✍️
#KitengeUpdates
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti Viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya Taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.
Akiongea kwenye mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi, Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, amesema amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutumia nguvu bali kwa maridhiano na haki.
“Katika hali ya kawaida, nani anaharibu amani? anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi kwani mfumo wa sasa hauwezi kutupatia Viongozi wa haki na kweli”
“Kama amani inapatikana kweli kwa kurudi mezani, wote waliokamatwa kwa kudai haki wakiwemo Viongozi wa siasa waachiwe haraka bila masharti, na wengine wasikamatwe wala kusumbuliwa, pia mihimili isiingiliwe bali itende kazi zake kwa haki”
#MillardAyoUPDATES