leo ukipata bahati zungumza na mungu kwa niaba ya wengine,ziweke mbali dhiki za tumbo lako,mueleze awaponye njaa ya upendo na tumain,nenda kawaombee wale walioenda hospital,na hawajarud tena na uhai wao nyumban,leo usiende na majuto ya kutofanikiwa malengo yako,ila waombe wengine
Ukikosea omba msamaha,kama neno lako linaweza kurudisha amani,zungumza.
Ikiwa unahisi mambo hayapo sawa, kaa upande wa kujenga.
Maisha ni zaidi ya, AMUA UNACHOTAKA, NAISHI MAISHA YANGU.
Umri wako ni mdogo sana kuamini,kila unayempoteza unaweza kupata mbadala wake.
~Nielewe
Binaadamu anakupa thamani pale anapokuhitaji tu.
Hata sahani yenye Chakula kizuri huwa inakuwa chafu baada ya Chakula kumalizika.,
Na hao ndio Binaadam ishi nao kwa Tahadhari.
Nielewe
Nimepitia maumivu wengine wakihisi nipo sawa, nilicheka katikati ya upweke mkubwa
Hamna alioyeona usiku mrefu niliouishi nyakati ambazo wao wamelala
Wala ni kwa kiasi gani niliyakumbatia matatizo yangu, huku nikiteketea sirini
Nyuma ya Tabasamu langu, Kuna hadithi msiyoielewa.
Mama zetu walianza kutubeba tumboni, Kisha mgongoni..
Na sasa kokote waendapo wametubeba mioyoni mwao..
Tunapambana ili siku moja tuwaondolee simanzi kwenye Dunia yenye mengi..
Mungu tusaidie��
~Nielewe
Tumechoka ndio, lakini ndoto zetu tumuachie nani?
Tunalala hoi tunamka hoi hadi wachawi wanaweza kutupeleka shamba na bado tukategea kulima.
Tunawaza mengi huku tukijipa imani, labda kesho haitokuja na adhabu nyingi kama leo🙏😔
~Nielewe
Niliwahi kuwekwa kwenye box la kuonewa huruma hadi nikaogopa.
Kijani haikuwa onyo,kumbe kuna nyakati ndio nyekundu tuliyoipuuza.
Kauli ya usijali, ilikuwa na tafsiri ya utaumia lakini kidogokidogo.
Visasi ingekuwa rahisi,kila Moyo uliojeruhiwa ungekuwa na kaburi lake
~Nielewe
Nafsi bora maishani ni zile ambazo baada ya ku survive kwenye moto, hurudi na maji kuokoa wengine..
Baada ya kufika safari yako, hutengeneza njia na wengine wapite..
Mafanikio ni kuyashinda majaribu yako, na kuwapa wengine sababu ya kushinda changamoto zao.
~Nielewe
Zipo nyakati hata yule usiyemjua, naye anahitaji msaada wako uliyojificha kwenye huruma uliyonayo.
Tumaini la mwisho la wengine hakikisha linaishia pia kwenye moyo wako.
Tuwape wengine tabasamu, Mungu anaona, atatupa la kwetu.
~Nielewe
Vita yetu ni kuhusu mabadiliko ya sisi wa jana,dhidi ya sisi wa leo tunaojitafuta.
Ukituona hatutaki utani,ni kwasababu vichekesho havileti ugali mezani.
Tukikwambia muogope Mungu,tunamaanisha usidhulumu jasho la unaemuweza
Tumwambie Mungu ahsante,sisi ni zaidi ya wale wa jana
Hakuna cha kuogopa zaidi duniani, Kama kufanikiwa katika vingi visivyo na maana.
Kwa maana dunia haitakutambua kama mjinga, pindi utakapofeli mtihani wa uchizi.
~Nielewe
Chini pagumu na panaumiza sana.
Mwanaume hata kama hana chochote, bado jamii inamtaka atoe.
Mwanaume akiomba msaada ameiweka chini heshima na utu wake..
Kama una nafasi msaidie, goti la mwanaume halina thamani.
~Nielewe
Kama mtu anaweza kukupenda kupita kiasi.
Basi amini anaweza vilevile kukuchukia kupindukia.
Kwasababu..
Kioo kizuri chenye taswira inayong'aa kinaweza kubadirika na kuwa silaha nzito pale kinapovunjika.
~Nielewe