1Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa
Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Wagalatia 2:16
hali tukijua ya kuwa mwanadamu
hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria,bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo,wala si kwa matendo ya sheria;maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenymwili atakayehesabiwahaki.
Yakobo 1:2-3
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.