Lakini tunapokuwa tunaongelea tabia na life style za Gen Z huwa tunasahau
kuwa tabia na lifestlye ni mazao ya malezi na mazingira waliyolelewa na kukulia!!
Swali ni nani kawalea?
Nani kawakuza!?
Jibu ni sisi!!
Sisi ndio baba/mama/kaka na dada zao tuliowalea na kuwakuza hawa!!
Kwahiyo tabia na kila kitu wanachokiishi hawa madogolasi ni sisi ndio tumewapandikiza waishi hivyo!!
Kama pongezi tupewe sisi
Kama lawama tupewe sisi!
"Jeshi la Polisi wapuuze taarifa za uongo za ndani ya Jeshi la Polisi lenyewe zinazodaiwa kuwa za kiintelejensia, kwamba watu wa Chadema wanapanga kufanya vurugu kwa wanachokiita kumuokoa @TunduALissu kutoka kwenye mikono ya magereza na Polisi, uongo mtupu." Mhe. @jjmnyika
My Bro , Husein Mwinyi.
Ninakuandikia kwa masikitiko makubwa kufuatia kauli zinazoendelea kutolewa na baadhi ya viongozi kutoka Zanzibar ambazo, kwa mtazamo wangu, zinaonesha ubaguzi wa wazi dhidi ya Watanganyika. Kwa muda mrefu nimekuwa na imani kwamba fikra za namna hiyo haziwezi kupata nafasi katika uongozi wako. Ikiwa nimekosea katika tathmini hiyo, basi nitakuwa nimekosea kwa kiasi kikubwa sana.
Kauli hizi si hatari kwa mshikamano wa Muungano pekee, bali pia ni mbegu ya mgawanyiko wa kijamii na kisiasa ambayo inaweza kuzaa matokeo mabaya kwa Taifa letu. Kinachonisikitisha zaidi ni ukimya wako. Katika mazingira ya sasa, ukimya huo unaweza kutafsiriwa kama ridhaa au baraka kutoka mamlaka za juu, jambo ambalo linaweza kueleza kwa nini kauli hizi zinaendelea kutolewa kwa mfululizo, zikiwa na simulizi moja na bila hofu yoyote.
Kwa kweli, naogopa hata kuingia katika mjadala wa nafasi na fursa ambazo Wazanzibari wamewahi kushika au wanazoendelea kushika katika Muungano huu. Kufanya hivyo kungekuwa ni kuushusha mjadala kwenye kiwango ambacho siamini kinafaa kwa Taifa letu. Historia inaonesha wazi kuwa Wazanzibari wamepewa na wameendelea kupata nafasi kubwa za uongozi katika Jamhuri ya Muungano, ikiwemo nafasi ya Rais wa Tanzania. Hivyo, hoja za kuwatenga au kuwadharau Watanganyika hazina msingi wa haki wala busara.
Ninaamini kwamba maneno yana nguvu. Yanajenga, lakini pia yanaweza kubomoa. Kauli za ubaguzi zikipewa nafasi ya kukua bila kukemewa, zitajenga chuki, zitaongeza mgawanyiko, na hatimaye kila upande utajikuta umepoteza. Taifa lolote linaloruhusu ukweli kunyimwa nafasi huku upendeleo na ubaguzi vikipewa sauti, hujenga mazingira ya migogoro ambayo baadaye huwa vigumu kuyarekebisha.
Sioni mustakabali mwema ikiwa mwenendo huu utaendelea. Wakati wa kukemea na kusimama upande wa haki ni sasa. Kesho inaweza kuwa imechelewa.
Polepole alikuwa mbele ya nyakati, alitoa onyo sababu alijua mpango waliokuwa wanakwenda tekeleza october 29 dhidi ya Watanzania
Alimuonya sana Samia kuachana na huo mpango, mpaka wakati anaongea haya tayari kulikuwa na tetesi ya silaha kuingizwa nchini
Samia akashupaza shingo na kupiga risasi waangamanaji, kwenye uapisho ndani ya kambi ya jeshi Kikwete alionekana ana shangilia akiwa na Samia
Kwa maana nyingi wote wawili wamekuwa kwenye hii mipango kwa muda mrefu wakapewa maonyo wakapuuza na kuendelea
Tukakomboe nchi 7/7
"Nitoe wito kwa Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kama watendaji na viongozi wanaosimamia muhimili wa mahakama katika majukumu, siyo tu ya usimamizi wa haki na majukumu ya kiutawala kuweza kuingilia kati jambo hili, ili mahakama kwa ujumla wake isipate aibu ya kuonyesha kwamba imeshiriki njama za kudhibiti watu kuwepo kwenye mahakama ya umma ambayo ni mahakama ya wazi." Mhe. @jjmnyika
🚨🇧🇷 Breaking: Carlo Ancelotti call Éderson to replace Wesley at the World Cup for Brazil!
Atalanta’s midfielder joins immediately and then he will sign as Manchester United new player in July. #MUFC
Hii serikali haijifunzi wala haijali yale yaliyotokea!!
Jana wasafi, waziri anahojiwa anaulizwa sababu za utekaji anatumia dakika 10 kuongelea sababu tofauti tofauti halafu the main one anai-skip!
Anakumbushwa na Ade kuhusu sababu za kisiasa, anasema kauli chonganishi za kisiasa zinaweza kuwa sababu!!
So adhabu ya mtu anayetoa kauli chonganishi za kisiasa ni kutekwa na kuuliwa, hakuna adhabu nyingine!
Imagine na huyo ndio waziri wa Home Affairs!!
Majibu kama haya ya kujifanya hujui tatizo! Ndio hujaza vijana hasira na chuki na kuamua kuingia barabarani then baadae mnasema wameshawishiwa na watu wa nje