#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 25, 2026
Last time tuliishia part 458 so leo tunaendelea na -;
Part 459
Imepigwa high court
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Mwenyekiti Lissu nae pia ameingia.
Mawakili wa Serikali wamechelewa sana kuingia Mahakamani na wameingia wakati mmoja na Majaji.
Mwenyekiti Lissu yupo anapanga vitu vyake pale juu na Majaji nao wanajiandaa na kuangalia nini Mwenyekiti Lissu anafanya ili tuendelee.
Jaji Ndunguru; Karani
Anasimama Karani anasoma Shauri namba….. Jamhuri vs Tundu Lissu.
Nassoro Katuga anasimama na kutambulisha wenzake Mrema, Ignas, Thawabu, Cathbert na Winniwa.
Na mshitakiwa yupo anajiwasilisha mwenyewe.
Mshitakiwa anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.
Nb. Hawa Mawakili wa serikali sijui kwanini wanasema anajiwasilisha mwenyewe. Ni Kujiwakilisha sio kujiwasilisha.
Mhe. Lissu anasema kutokana na mazingira ninayolazimika kujitetea niko Gerezani kwa mwaka mzima na najitetea mwenyewe na nimepiga kelele kuwa napoteza muda mrefu na nalazimika kuandaa final submission nikiwa mwenyewe.
Hii kazi nilitakiwa kuifanya kwa mwezi mmoja lakini mnanipa siku 5 haiwezekani.
Sasa leo siendi hoja ya sita, narudi nyuma kidogo kuongezea vitu muhimu sina namna.
Watu wanacheka.😂😂😂
Sasa naomba nirudi kwenye hoja ya maneno.
Hivi kwanini Mahakama ya Rufani katika Khatibu Gandi katika ukurasa wa 55 na 67 maneno matupu hayatengenezi hatia ya uhaini.
Mere words do not constitute treason under sect. 39(2)(d) of the Penal Code.
Mahakama ilisema hivyo kwasababu ilikuwa inafahamu historia ya Uhaini hapa Nchini.
Ilifahamu historia ya Sheria yetu kuhusu Uhaini, sitatumia masaa matatu kwenye hili.
Penal Code yetu ilitungwa Mwaka 1930 na Sheria yetu ilitungwa moja kwa moja kutoka Uingereza walikuwa wanatutawala hawa.
Mwaka mmoja kabla 1929 Bunge la Uingereza lilipendekeza sheria za jinai kwa ajili ya Tanganyika, Kenya, Uganda na Nyasa Land modern day Malawi.
Walipendekeza sheria kuu za jinai kwa nchi hizo zote kwahiyo 1930 ndio Penal Code ikatungwa.
Kutokana na draft na recommendation kutoka Westminster ya Bunge la Wingereza.
Sheria ya uhaini vifungu vinavyohusiana na Uhaini vilichukuliwa kutoka sheria ya makosa ya Uhaini ya Wingereza ya Mwaka 1848.
The Treason Fellony Act iliitwa hivyo hiyo sheria ya Uingereza na kwenye clause ya manifestation inasema manifest such intention by writing or printing or by open advicing speaking or by any overt act or deed.
Kwahiyo Sheria ya Uingereza ya 1848 ilikuwa imeweka uhaini wa kuzungumza au kutoa maneno.
Hicho kifungu kilichokuwa kinaruhusu maneno kuwa ni kosa la Uhaini kiliwekewa ukomo wa maisha. Ile Sheria kifungu cha 4 ilisema hicho kifungu kitatumika kwa miaka miwili tu.
Baada ya mwaka 1850 kiliacha kutumika. Maneno kutumika kama sababu ya kumtia mtu hatiani kiliacha kutumika huo mwaka wa 1850.
1891 that provision amended by repealing the word by advicing speaking. Yaliondolewa kwenye kifungu. The repealing Act was the statute law revision Act of 1891 the WestMinister Parliament.
From that time to this day English Law on treason is couched in exact the same term as it is provided under Sect. 39(2) of the Penal Code.
Our Penal Code enacted in 1930 upon direction of British governement. The direction was to apply the law of treason as the way as it existed.
Kwa vile English Law ilishafuta Uhaini wa Maneno ndio maana Sheria yetu ya Uhaini haijawahi kuwa na Uhaini wa Maneno.
Ndio maana Marehemu Jaji Mkuu Francis Nyalali alisema maneno matupu hayatengenezi tendo la Uhaini kwenye Khatibu Gandi. CJ alikuwa anajua na alifahamu hii Sheria ilitoka wapi na ikoje.
Kama ambavyo Sheria hii ilipendekezwa na Waingereza katika nchi nne nilizotaja. Nchi moja iliweka Uhaini wa Maneno. So The Ugandan Penal Code imejntroduce neno Utterances yaani matamashi kwenye Uhaini.
Part 460 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 458
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Sasa nimetumia the oxford advanced disctionary na Blacks Law dictionary kwasababu maneno hayo hayajawa defined kwenye sheria yetu. Na Bahati mbaya sijapata case law.
Mawakili wanaonisaidia kufanya research wanafanya kazi kubwa sana na Mungu awabariki lakini hawajapata definition ya overt act and deed kutoka kwenye case laws.
Hili ni eneo ambalo mnapaswa kutoa mwongozo for the future. Sasa niendelee Wahehsimiwa Majaji Information inasema hivi na hili ni tatizo la pili la Information.
The accused person manifested his intention by his deed of uttering by saying the following words
Sasa waliyoileta hiyo uttering hawajui wameleta kitu gani. Uttering kisheria ni nini?
Wametengeneza kitu ambacho kina destroy complitely their case.
Sheria Penal Code inasema nini maana ya Uttering ni neno la kisheria.
Maana ya kisheria imasema hivi Sect. 5 inasema hivi anasoma.
Haya ni matendo yanayohusiana na forgering, counterfeit na mambo yanayohusiana na hayo.
Kifungu cha 342 kinasema uttering false documents, kifungu cha 360 uttering counterfeit coin anasoma vifungu kadhaa vya Penal Code na kusema uttering pekee iliyopo kwenye Sheria ya Penal Code.
Ndio maana uttering nilimuuliza shahidi wa Jamhuri hilo neno uttering limetafsiriwa wapi? Hilo neno Utter lipo kwenye kifungu cha 53(b) cha Sheria ya Huduma ya Habari
Hati ya Mashitaka namna ilivyolitumia neno Uttering kwahiyo shitaka kwa vile lipo kwneye kanuni ya Adhabu basi Sheria inayotumika ni Kanuni ya Adhabu wala sio sheria ya Huduma ya Habari.
Kwenye Penal Code uttering ni mambo ya forgery na habari za coin huko. Shitaka hili ni bovu wameleta maneno ambayo hayapo kwenye sheria waliyotumia kunishitaki.
It is Complitely defective kwanza maneno sio matendo. Words can not be deed and the use of the word uttering destroys the legal validity of the infornation.
Authorities are now settled, the law are now settled on what should happen information introduce something which is alien to the law it invalidate such information. It makes the information incurably defective.
Time is long past for that hawawezi kuomba kurekebisha kitu kwa sasa. Authority ninayowapa ni Court of appeal of Tanzania in case of Osward Abubakar Mangula versus R CA 153 1993 CAT at Mbeya at page 5 to 6 Judge Samatta as he then was.
Kesi nyingine maarufu kwenye Law Reports Musa Mwaikunda vs R 2009 TLR 387
Na kesi nyingine ni Hassan Jumanne Msingwa sio Msigwa vs Republic CA 290/2014 CAT at Tabora. 1st December/2015. Justice Massati.
Kwahiyo by introducing uttering in to information the prosecution render the Information Incurable Defective.
The answer ti 5th issue must be negative that is to say a deed is not the same as the spoken words and the uttering pleaded in the infornation does not constitute an overt act as per section 39(2)(d) of the Penal Code.
Hati ya mashitaka haitibiki ni mbovu sana, wameingiza maneno ambayo sio maneno ya Kisheria, maneno ya mtaani yanaingizwa kwenye nyaraka za kisheria.
For purpose of treason uttering words does not constitute offence of treason.
Sasa niende kwenye issue no. 6
Jaji Ndunguru: Nafikiri uanze kesho hiyo hoja ili twende vizuri.
Mhe. Lissu: Ni sawa kabisa.
Jaji Ndunguru mashitaka mnasemaje?
Katuga: Tuanze kesho tu ni sawa, naunga mkono.
Jaji Ndunguru anacheka kidogo.😂
Basi tukutane kesho saa tatu asubuhi kwa ajili ya kujibu hilo swali la sita.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 457
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
An Act, attempt or omission punishable by law, hayo ndo makosa.
Kama hakijawekewa adhabu na hakijatamkwa sio makosa.
Hayo maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini sio makosa ya kihaini kwa mujibu wa kifungu cha 39 chote na vilevile sio makosa kwa mujibu wa makosa yaliyoorosheshwa kwenye sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Udiwani.
Sio makosa ya Jinai kokote kwahiyo ukiyasema yanakuwaje makosa ya kuchochea mtu kufanya jambo halali? Kosa lilitakiwa jambo lisiwe halali na liwe kinyume na sheria ndio lingekuwepo kosa hapo.
Waheshimiwa Majaji nataka nifunge kwenye hilo suala kwamba Je maneno yanayolalamikiwa ni makosa kwa mujibu wa Sheria?
Na jibu ndio hilo nililolionyesha na sio makosa ya Uhaini wala jinai nyingine.
Jibu la issue no. 4 ni Negative. Maneno niliyosema sio makosa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na sio pia ni Uhaini.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niende kwenye issue no. 5 inahusu uchapishaji yaani PUBLICATION.
No issue ya tano ni Deed yaani kitendo.
Inasema JE KUTAMKA YALE MANENO NI KITENDO KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Whether the alleged words constitute a deed?. Suala hili kwa lugha rahisi upande wa mashitaka wanasema kusema ni matendo.
Issue ni je maneno ni matendo?
Kwanza Waheshimiwa Majaji naomba nifafanue hii confusion imetokea wapi?
Hii ni confusion ya kutengenezwa makusudi na upande wa mashitaka. It is a delinerately confusion created ili kuhalalisha hoja fulani. Iko hivi kifungu cha 39(2)(d) kinasema any person who forms an intention to instigate any lerson or grouo of person to intimidate the executive and manifest such intention by any overt act or deed or by publishing by printing or writing shall be liable of conviction
Masharti ya kifungu lazima uthibitishe kwa kuchapisha maandiko au maandishi au kwa kitendo cha wazi. Khatibu Gandi ilisema mananeo matupu sio Uhaini.
Sasa ili wanitengenezee kosa wakasema maneno ni matendo kumkwepa Khatibu Gandi. Wamedraft mashitaka kwa kusema the accused manifested his intention by his deed of uttery. Kwahiyo namna ya kuhalalisha maneno haya ni kosa wakaona waseme maneno ni matendo. Wanataka kuepuka masharti ya sheria.
Ili kuendana na kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code.
Pia wametengeneza tofauti kwenye maneno ambayo haipo kwamba overt act na deed vinatofautiana. Utofauti wake ni nini?
Hoja yangu ya kwanza ni kwamba acts and deed in their plain meaning means the same thing.
Kwa maana ya kawaida kiswahili chake ni kimoja kwamba ni MATENDO.
Kwenye kingereza in their plain english meaning oxford advanced learner disctionary an act means a particular thing that somebody does.
Hiyo dictionary inasema it is synonimous as an action. Kwa Kiswahili ni kitendo.
What is a deed in the same Dictionary a deed is a thing that somebody does. It is synonimous with an act.
Therefore a deed is essentially the same as an act. Kifungu cha 39(2)(d) kinaposema kitendo kitathibitishwa with an overt act or deed maana inasema inahitaji kitendo na sio kitu kingine.
Hayo maneno mawili kuthibitisha kwamba yanasema ni kitu kimoja twende kwenye Blacks Law Dictionary hiyo ni famous Kamusi ya Kisheria.
Blacks Law Dictiomary 7th Edition what does it say about an action is something done or perfomed. It also a deed.
It is a process of doing or perfoming. Haya ni matendo. Kwahiyo Wahehsimiwa Majaji an act is the same thing as a deed. Something that is done. It can not be something that is said
Maneno hayawezi kuwa ni Matendo. Kwahiyo hii charge inayonikabili inaposema nilithibitisha nia yangu ya uhaini kwa matendo yangu ya maneno haiwezekani. Words can not be deed. Na kwavile haiwezekani hii hati ya mashitaka ni Defective. Ni mbovu kwasababu imetaja kitu ambacho hakipo kwenye sheria.
The charge is defective on this particular point.
Part 458 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 456
Mahakama imerejea.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao wanaongozwa na Jaji Ndunguru.
Anasimama Katuga anasema corum iko kama asubuhi isipokuwa Ajuaye Zengeli, anasema wako tayari kwa ajili ya kuendeshea.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshitakiwa vipi?
Mhe. Lissu anamjibu niko tayari.
Mh. Lissu anasimama na kusema Wahehsimiwa Majaji tulipobreak nilipendekeza niingie kwenye hoja ya Sheria ya Uchaguzi na kama ambavyo nimeelezea kosa la Uhaini kama lilivyofafanuliwa kwenye Katiba.
Kosa nililoshitakiwa nalo halihusiani kabisa na kilichosemwa kwenye kanuni ya adhabu na ndio sheria pekee kwahiyo kama haya matendo niliyoshitakiwa nayo hayafit katika sehemu yoyote katika mojawapo ya matendo 10 ambayo kifungu cha 39 kimeyataja kwamba ukiyafanya haya unakuwa umefanya kosa la Uhaini.
Maana yake ni kwamba mimi sijafanya kosa lolote la Uhaini.
Sasa Wahehsimiwa Majaji kama sijafanya kosa lolote la Uhaini je nimefanya kosa lingine lolote kwa mujibu wa sheria za Tanzania? Ndicho ninachotaka kujadili kwa sasa.
Maneno ninayoshitakiwa nayo ni kuvuruga Uchaguzi na sheria No. 1 ya 2024 ndio Sheria inayosimamia uchaguzi kwenye nchi hii. Hiyo sheria ilitungwa kwa ajili ya Uchaguzi wa 2025 na sheria hiyo ilitungwa kusimamia uchaguzi ambao kwa mujibu wa DW 5 umekuwa ni uchaguzi ambao watu wengi wamekufa kuliko kipindi kingine chochote toka vita ya majimaji.
Sura ya 7 ya Sheria hiyo ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Inasema kwenye kichwa cha habari ni MAKOSA na ADHABU ZAKE.
Makosa yanayohusu Uchaguzi na adhabu zake. Waheshimiwa Majaji sheria hii katika Sura ya 7 imeorodhesha jumla ya Makosa 23 na adhabu zake.
Kuanzia kifungu cha 114 hadi 136 ni orodha ya makosa na adhabu zake. Makosa ambayo ukiyatenda unaweza kushitakiwa na kufungwa au ukapewa adhabu ya kijinai na kufungwa.
Maneno ambayo tunataka kujua ni makosa ni yale maneno tutazuia uchaguzi, tutavuruga uchaguzi na tutahamasisha uasi. Tumesema sio Uhaini hadi sasa kwa hoja tulizotoa. Sasa je ni kosa gani lingine?
Uzuri wa sheria hii umeandikwa Kiswahili kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kusoma. Kosa la 1 lipo kwenye kifungu cha 114 linaitwa kosa la uandikishaji wapiga kura,
2. Kutumia wadhifa kushawishi watu wasiwe wagombea kifungu cha 115.
3. Mwenendo usiofaa wa mtendaji wa uchaguzi.
4. Makosa yanayohusu daftari la Wapiga kura kifungu cha 119 hili nalo mimi sihusiki na hayo yote niliyotaja.
5. Mwenendo usiofaa wa maafisa uandikishaji.
6. Kifungu 121 makosa yanayohusu fomu za uchaguzi na karatasi za kura.
7. Kosa la mtu kutangaza amejitoa kwenye kinyang'anyiro.
8. Kifungu cha 123 vishawishi vya rushwa kwa ajili ya kujitoa hilo nalo sihusiki nalo.
9. Kifungu cha 124 margin inasema makosa mengineyo kutoa ushahidi wa uongo wakati wa tamko.
10. Utunzaji wa siri ni kosa pia. Kif. 125
11. Kifungu cha 126 hongo na takrima
12. Impersonation kujifanya mtu mwingine. Kuchukua kadi ya mpiga ya mwenzako.
13. Kupoteza sifa kwa kuhukumiwa kwa kosa la kitendo cha Rushwa.
14. Kosa la 14 liko kifungu cha 129 bad influence ushawishi mbaya.
15. Kosa la kif.130 hongo na rushwa kwa maafisa wa tume.
16. Hatia ya kujifanya mtu mwingine. Mimi ni Tundu Lissu wa miaka yote sijajifanya mtu mwingine.
17. Adhabu ya vitendo vya rushwa na vitendo haramu.
18. Kuingilia Mikutano halali ya hadhara ni kitendo haramu vilevile.
19. Makosa yanayohusu siku ya uchaguzi. Kuvaa nguo za chama siku ya uchaguzi. Hilo pia sijafanya.
20. Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wakati wa uchaguzi. Hilo nalo halinihusu katika kesi hii.
21. Kuchafua matangazo ya uchaguzi. Wagombea wameweka mapicha unararua.
Hayo ndio makosa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na ukiyafanya hayo yana adhabu zake zilizoelezwa kwenye sheria.
Hakuna kukinukisha hakuna kuzuia uchaguzi sio kosa kabisa. Na sio makosa kwasababu kifungu cha tano cha kanuni ya adhabu kimefafanua makosa ni vitu gani?
Part 457 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 455
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Waheshimiwa Majaji tuangalie sasa maneno yaliyoniweka gerezani mwaka na nusu inaelekea sasa.
Tuanze na neno tutavuruga uchaguzi, liko wapi kwenye hiyo list ya matendo 10 ya kihaini? Kuzuia uchaguzi, iko wapi?, kuhamasisha uasi kwa kingereza ni rebellion iko wapi kwenye Section 39??? Iko wapi Waheshimiwa majaji ili nilale usingizi mzuri leo kuwa nilisema maneno yanayokiuka sheria, ni wapi?? Haipo . Kukinukisha, iwe kukinukisha vibaya sana, kukinukisha sana sana ili angalua leo wanangu wherever they are walale kwa amani kuwa baba yao aliongea maneno ambayo yanakiuka sheria, yako wapi?? Hayapo waheshimiwa majaji.
Katiba imesema uhaini kama unavyofafanuliwa kwenye sheria, maneno yote yanayodaiwa niliyasema hayapo kwenye sheria, waheshimiwa majaji nimefungwa bure, nimeonewa, how can you say it otherwise? I am a father, nina ndugu wanakuja kila siku, nina wanachama hapa wanatoka everywhere in the country, a year and half, nalindwa na maaskari utafikiri ni muuaji wa aina gani? Why? Kwanini??
Waheshimiwa majaji kama hayapo kwenye kanuni ya adhabu, ugomvi ni uchaguzi, tunataka kuvuruga uchaguzi, tutazuia uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024
Jaji Ndunguru: Nadhani tubreak hapo , upande wa mashtaka mnasemaje?
Watu: hawapo😂😂😂
Job Mrema: hatuna pingamizi
Jaji Ndunguru: Unahisi kumaliza leo?
Mhe. Lissu: Hilo ni swali gumu Waheshimiwa majaji, huku anatoa tabasamu kama kawaida.
Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi saa nane na nusu
Imepigwa High Cooouuurrrttt
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 454
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mashahidi wote hao wamesema hayo maneno yanatengeneza kosa la uhaini. Mtayaona kwenye hizo kurasa. Without exception wametoa sababu zilezile. Sababu ya kwanini wamefanya hivyo ni Sababu za Mapolisi. Ni walewale hakuna jipya.
Kwa upande mwingine mashahidi wote wa utetezi wamesema maneno yale hayana shida yoyote. Na hayo yapo kwenye ukurasa wa 196 na 123 kwa DW1, 671 na 672, 679, 681, 698 to 700, 726 in the case of DW 2. L
Waheshimiwa Majaji DW 3 ipo 764 na anataja kurasa kadhaa hapo pia.
DW 4 upo kwenye ukurasa 810na DW5 930 anataja kurasa kadhaa zinazohusu mashahidi hao.
Wahehsimiwa majaji mashahidi wote wa utetezi without exception hayo maneno yanayodaiwa hayana kosa lolote kwenye sheria za Tanzania.
Waheshimiwa Majaji kwa vile kuna 2 sets of evidence which are diametrically oppose what is the position of the law.
Kujibu swali hili the statrting point on this question must nencesarily article 28(4) of the constitution.
Maneno ya Katiba ni muhimu sana inasema hivi, uhaini kama unavyofafanuliwa na Sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 28(4) ya Katiba)
Waheshimiwa majaji, Uhaini kwa nchi hii ni ule uliofafanuliwa na Sheria. Nje ya Sheria ni Maneno matupu. Kwa vile uhaini lazima uwe umefafanuliwa na Sheria, ni sheria ipi inafafanua uhaini? Ni kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu ndio kinafafanua uhaini.
Waheshimiwa majaji kifungu cha 39 ni muhimu sana kwenye kesi hii. Kama ninayotuhumiwa kuyafanya hayamo kwenye kifungu hiki hakuna uhaini hapa. Kifungu cha 39 kina vifungu vidogo vinne. Hivyo vifungu vidogo vinne vimetengeneza matendo 10 ambayo ukiyafanya yanatengeneza kosa la uhaini.
Kitendo cha kwanza cha kihaini kwenye kigungu cha 39 (1)(a) ni kumuua au kujaribu kumuua Rais. Kitendo cha pili cha kihaini ni kuendesha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano 39(1)(b).
Kifungu cha 39(2) kimetengeneza matendo manne. Hivyo kitendo cha tatu kinaitwa forming the intention to effect or forming the intention to instigate any person or group wasababishe kifo cha Rais au Rais atiwe kilema au ajeruhiwe au afungwe ni uhaini 39(2)(a)
Kitendo cha nne ni kutengeneza nia ya kuwezesha au ukatengeneza nia ya wengine wawezeshe Rais apinduliwe kwa njia zisizo halali kutoka kwenye nafasi yake kama rais na jina lake kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu ni kitendo cha uhaini 39(2)(b)
Kitendo cha tano ni kutengeneza nia ya kuwezesha au kuwawezesha kupinduliwa kwa Serikali ya JMT ni uhaini 39(2)(c). Kitendo cha sita ni hii niliyoshtakiwa nayo, ukitengeneza nia ya kuwezesha au kushawishi watu wawezeshe kutishiwa kwa Serikali, Bunge au Mahakama unakuwa umetenda kosa la uhaini 39(2)(d)
Kosa namba 7,8 na 9 yako kwenye kifungu cha 39(3). Kitendo cha 7 kipo 39(3)(a) ambacho kinasema ukijiunga au kushirikiana nao na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la uhaini. Kitendo cha 8 kinasema kuchochea mtu yeyote kuivamia Jamhuri ya Muungano kwa silaha au kama wale wakongo wanaitwa M23 ukiwaleta Tanzania ni uhaini.
Kitendo cha 9 cha kihaini kipo 39(3)(b) ukichukua silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kuibadilisha serikali ili ibadilishe mambo yake ni uhaini typically hapa ni Kama M23 au wale wa Somalia , 39(3)(c)
Kutendo cha 10 kipo kwenye 39(4) ni kusaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kwa kufanya kitendo chochote cha kumsaidia adui kama vile kuhatarisha maisha, ni kitendo cha uhaini, haya ndio makosa ya uhaini kwa Sheria za Tanzania. Nje ya haya ni maneno matupu, ni hisia, ni ignorance and such like.
Part 455 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 453
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Ushahidi wote huo wa mashahidi hao went largely uncontested by this army of this governement Lawyers. It remain intanct and therefore interm of the aforesaid authorities. Rumima, Nyerere failure to cross examined is deemed to be admission of the veracity of the defence testimony and story.
Hawakuhoji kwasababu walikubali story yetu.
Naomba nimalizie kwenye hoja hii kwa kusema yafuatayo.
Nimeshitakiwa kwa tuhuma ya kutengeneza nia ya kuchochea umma wakati sheria kifungu cha 39(2)d hakitambui umma. Kinatambua nia ya kuchochea mtu au kikundi.
Nimeshitakiwa kwa kutengeneza nia ya kuchochea umma ambao hautambuliki na sheria kuzuia uchaguzi wakati sheria haitambui nia ya kuzuia uchaguzi. Nia ya kuzuia uchaguzi haitambuliki na kifungu husika.
Nimeshitakiwa kwa kutengeneza nia ya kuchochea umma usiotambulika kuzuia uchaguzi usiotambulika kisheria ili kuitishia serikali ambayo sijaisema kokote kwenye maneno yangu na hawajaleta ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Nimeshitakiwa kwa sababu ya hisia na sheria hairuhusu mashitaka ya hisia.
Katika mazingira haya hili swala la tatu. Jibu lake sio lingine zaidi ya HAPANA.
The only logical and xorrect answer is and can only be NEGATIVE. That is to say the accused did not inform any intention to instigate any person or group of person to obstruct the 2025 general election for the purpose of intimidating the Executive of the URT.
on the basis of Grey Likungu Mataka to sustain a conviction on the charge of treason the prosecution must prove the intention to commit treasonous conduct.
The prosecution failed to prove the intention to commit treasonous act.
Nimemaliza swala la tatu. Naomba niende swala la nne sasa kwa ruhusa yenu.
Swala la nne linasema JE HAYO MANENO yaliyotamkwa na Mshitakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria?
Hayo maneno hayo yamekuwa maarufu sana, yanatengeneza kosa linalotambulika na sheria za nchi hii. Yanaonesha kosa? Do they constitute any offence known to Tanzania laws?
Nitajibu swali hilo kama ifuatavyo.
Swala hili lilijitokeza kutokana na tuhuma zilizoletwa upande wa Mashitaka kwamba the accused uttered words amounted to criminal offence which determination ilisababisha mkuu wa upelelezi kanda ya Dar es salaam kufanya upelelezi.
Haya ni maneno yao Jamhuri sio yangu.
Maneno yenyewe yakoje yanasema nini?
Kwenye mkutano wa Tarehe 03/04/2025 mtuhumiwa alidhihirisha nia yake kwa kusema maneno yafuatayo "wanasema kitu kimoja sahihi msimamo huu unaashiria uasi tutazuia uchaguzi na hiyo ndio namna .. huu uchaguzi tutauvuruga vibaya sana..."
Haya ndio maneno yanayisemwa yanadhihirisha nia ya uhaini. Na ndio criminal offence.
Wahehsimiwa Majaji kitu cha kwanza kabisa. Kuhusiana na maneno haya. Ni kwamba hakuna mahali kokote ambapo upande wa mashitaka umeyafafanua hayo maneno.
Hawajasema kuvuruga uchaguzi maana yake ni nini na kwanini ni kosa?
Kuhamasisha uasi ni nini na kwanini ni kosa?
Hawajasema kuzuia uchaguzi ni nini na kwanini ni kosa?
Hawajasema kukinukisha ni nini na kwanini ni kosa?
Sio wajibu wangu mimi mshitakiwa kuyatolea maneno hayo ufafanuzi na kuonesha kuwa sio makosa. Sio wajibu wangu kisheria.
Ni wajibu wa upande wa mashitaka kufafanua hayo maneno yana maana gani na kusema kwanini ni makosa. Ni wajibu wao kueleza kwanini wanadhani ni kosa.
It is a question of burden of proof na lazima tuambiane ni nani ana wajibu wa kuthibitisha. That burden it never shift from the prosecution.
Kwasababu hawajafafanua wameleta hisia zao juu ya hayo maneno. Waheshimiwa Majaji ushahidi wa upande wa mshitaka juu ya haya maneno uko ukurasa 146 in the case of PW 1. Ukurasa 183 na 184 in the case of PW 2, na ukurasa wa 444 hadi 446 in the case of PW 16.
Part 454 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 452
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Msimamo huu utaukuta kwenye maamuzi ya Mahakama hii kwenye kesi ya Justin Rutahirwa vs Bulchad Kalumna. Consolidated Criminal Appeal No... 2020 Justice Kilekamajenga alisema
Hisia hata kama ni nzito kiasi gani haziwezi zikawa msingi wa kutia mtu hatiani. Na hasahasa kwenye kesi nzito kama ya Murder.
Sasa hii ya kwangu sio kesi ya Murder.
Hii ni kesi ya Uhaini na Waheshimiwa Majaji UHAINI ni kosa pekee lililotajwa kwenye Katiba ya nchi. Ibara ya 28(4) inasema UHAINI KAMA UNAVYOFAFANULIWA NA SHERIA UTAKUWA NI KOSA LA JUU KABISA DHIDI YA JAMHURI YA MUUNGANO.
Ndio kosa kubwa kuliko yote kwneye nchi hii na adhabu yake ni kifo. Walionishitaki wanataka mnihukumu kifo kwasababu ya hisia zao. Kwasababu wanahisi nilikuwa nalenga kuitishia Serikali.
Waheshimiwa Majaji Mahakama hii kwa misingi hii ya kisheria haiwezi kuwakubalia. Na nawaomba Majaji msiitikie wito wao, wito wao ni wito wa hisia msiwakubalie mwaliko wanaoutaka. Kunitia hatiani kwasababu tu wanahisi nililenga kuitishia serikali.
Ushahidi wa Utetezi unasemaje juu ya hii hoja? Ushahidi wangu ulikuwa simple, straight foward and consistent kwenye hii hoja.
DW 1 589 na 590 nilizungumzia nia ya kuitisha huo mkutano kwamba told the court the meeting was inteded of bring together all prospective candidate of the party from across the country ams it was called with the intention of exolaining the party no reforms no election resolution made by the party conglese.
Ndio ilikuwa nia yetu na ndio ilikuwa nia yangu. Tuliitisha watia nia kuwaeleza msimamo wetu. That was the intention.
Specifically on those words nilisema yafuatayo ukurasa wa 596 wa records
In that discussion i did not refer to the governement and what intended to do to the governement. Nikaendelea kusema ghe allegation that our objective was to threten the govenrnrmt is therefore misplaced.
My purpose was to explain kwa watia nia kuhusu changamoto za masuala ya uchaguzi na ili waelewe msimamo wa Chama wa no reforms no Election.
There was no intention to threaten the governement because threatening the governement was never part of my agenda. I did not mobilize people to engage in violence or disorder. Nilisema tutapambana kutaka mageuzi hadi reforms zitakapopatikana.
I was extensively and vicious cross examined nilikaliwa kooni kwelikweli lakini naomba muangalie kwenye record kama huo ushahidi wangu juu ya nia yangu kwamba ulihojiwa hata mara moja.
Mimi nimeangalia hiyo rekodi yote sijaona these governement lawyers cross examined me juu ya nia yangu kwenye mkutano ule. Hakuna hata mara mija walipofanya hivyo. Waliniuliza maswali alfu lela ulela. That aspect complitely remain unchallenged Justice Rumima Katiti, Nyerere Nyague, Chora Samson Kiberit Mahakama ya Rufani all those cases from Court of Appeal have established a principle that failure to cross examine a witness on a material point is an admission of his version of the story.
Kutonihoji kuhusu nia yangu huwezi kusema hukubaliani na nia yangu ya kuitisha ule mkutano. Hiyo nia umeikubali kabisa.
Ushahidi wangu umeungwa mkono na DW 2 Kwenye ukurasa wa 161 wa rekodi. Na ukiangalia nae pia aliulizwa maswali mengi lakini hakubadili msimamo wake kabisa angalia ukurasa wa 691 he never waver the position. Alisema tuliazimia bagamoyo na tulihitaji kuuelezea kwa watia nia.
Msimamo huo huo uliungwa mkono na DW 3 ukurasa wa 732 na 779 na 791 na 795 of the record. Kwenye swala la nia nae hakushake kwenye suala la nia.
Msimamo wa Utetezi ulishikiliwa pia na DW 4 ukurasa 799 na 800 wa hizo rekodi za Mahakama.
Part 453 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
@HildaNewton21 maelezo ya Lissu yana jieleza yenyewe, hayahitaji hata ufafanuzi. walijua 39(2)(d) ita collapse, lakini clauses nyingine za 39 hazingefaa kabisa, so wakalazimisha hii ya 39(2)(d) hoping kwamba ISSUE YA KUCHAPISHA UCHOCHEZI NA KUUSAMBAZA MWENYEWE itakuwa NGUZO YA SHITAKA LAO, so
Mnajua kupika data kuhadaa dunia nyie; hakuna huduma yoyote ya afya, sembuse ya mama na mtoto?Never. Kama mnabisha ruhusuni foreign media ije kufanya investigative journalism ndani ya #Tanzania tuone kama mtadhubutu. Nyooo! Takataka nyie. Waongo. Wauwaji 🚮
Hii nchi hii yani mtu anabomolewa biashara yake anarecord video anamuomba raisi na serikali imusaidie hajui kama Hao ndio wameamua kufanya hivyo😅
Nchi inayo kuwa inaongoza kuagiza bidhaa nyingi kutoka nchi za nje bila ya kuwa na viwanda ni ngumu kutokuwa na machinga 👇👇
"VIWANDA VYOTE ALIVYOVIACHA MWAL. NYERERE VIKO WAPI?" -HECHE
Ni swali la Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanhuzi, Meatu, Mkoani Simiyu, ambapo ametumia nafasi hiyo kuibua KILIO cha upatikanaji wa ajira na, kile anachodai kwamba serikali chini ya CCM ndio iliyoua Viwanda ambavyo kwa miaka mingi vilikuwa mkomhozi wa Soko la ajira kila kona Nchini.
Hii mifumo yetu ya kiutawala ni yakuiboma yote, unajiuliza JD za RC,DC ni zipi hasa ? Ni either Vyeo hivi vifutwe au watu wavipate kwa ku-apply. Huyo anayewatea (Raisi) mwenyewe ana KIBURI kimejaa DEBE, hao wateule wake watawezaje kuwa wenye STAHA ?
Nimeguswa sana na maneno ya mwenyekiti Lissu leo wakati anaendelea kutoa hoja zake za majumuisho ya mwisho.Too emotional aiseee 😢 😭 😢
"Wamenishitaki kwa uongo,ninalala gerezani kwenye kachumba ka futi sita wakati nina nyumba yangu nzuri tu"Tundu Lissu