Ubalozi unashukuru kwa taarifa ya ndugu @DuniaSlaveDunia kuhusu Watanzania waliokamatwa nchini Afrika Kusini na kupelekwa Lindela Repatriation Center, kwa kosa la kuishi bila Vibali nchini Afrika Kusini.
Aidha, katika utaratibu wa kawaida wa Ubalozi, tarehe 19 Mei, 2026 Ubalozi ulitembelea Kituo hicho ili kubaini iwapo wapo Watanzania wenzetu wanaoshikiliwa. Zoezi la Utambuzi lilibaini uwepo wa Watanzania 60 wanaoshikiliwa katika Kituo hicho kwa kuishi nchini Afrika Kusini bila ya Vibali. Ubalozi uliwapa Watanzania hao Hati za Dharura za Kusafiria (ETD).
Mwisho, Ubalozi unaarifu kuwa namba alizoweka ndugu @DuniaSlaveDunia kwenye taarifa yake ni za simu ya mezani isiyo ya Ubalozi. Ubalozi unapenda kuarifu kuwa, namba sahihi ya Ubalozi ni +27 12 342 4371. Barua Pepe ya Ubalozi ni [email protected] au [email protected].
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini