Si vibaya kuwa rafiki, ila chunga sana kinywa chako
Shetani huwa hayupo mbali, ( Shetani ni Roho na Mungu ni Roho maana ake wote hawaonekani katika kimwili hivyo hukaa ndani ya miyoyo)
Shetani hukaa ndani ya mtu, kuna siri zako ukianza kushare kwa rafiki ndio mwanzo wa kifeli
@Mr_Simon256
Si vibaya kuwa rafiki, ila chunga sana kinywa chako
Shetani huwa hayupo mbali, ( Shetani ni Roho na Mungu ni Roho maana ake wote hawaonekani katika kimwili hivyo hukaa ndani ya miyoyo)
Shetani hukaa ndani ya mtu, kuna siri zako ukianza kushare kwa rafiki ndio mwanzo wa kifeli
@Mr_Simon256
Ukiona kila mara unarudia yale yale ya zamani ( makosa yako) emu kalisha mwili wako chini, tafuta sehem tulivu kisha jitafakari unachangamoto gani kichwani 🧠
Kama Kijana Bado unapambana na unatamani kuajiriwa Serikalini, Mashirika makubwa jamani angalia sana unacho Post mtandaoni, Sasa hivi Social Media ni CV yako ya Pili, Shauri zako 🚶♀️
Kuna vitu ukipoteza unaweza kuvinunua tena.
Pesa unaweza kutafuta nyingine.
Simu unaweza kununua nyingine.
Gari unaweza kununua tena.
Lakini miaka ya ujana haiwezi kurudi.
Ndiyo maana usitumie miaka yako yote ukisema:
“Bado nina muda.”
Ndiyo, una muda.
Lakini muda huo ndio mtaji wako.
Tumia sehemu yake kujenga maisha ambayo utayashukuru baadaye.
Usifurahie ujana mpaka usahau future yako.
Na usiogope future mpaka usifurahie ujana wako.
Jenga balance.
Enjoy life, lakini pia jenga maisha.
Mshahara ni kama kidonge ambacho mtu hupewa ili kupunguza maumivu,
Mshahara pekee inakusaidia kusahau ndoto zako
" Mtu alietajirika au kuwa na mafanikio kupitia mshahara huyo ni mwizi"
● ili uwe na mafanikio ni lazima uwe na chanzo kingine cha mapato
Mshahara ni kama kidonge ambacho mtu hupewa ili kupunguza maumivu,
Mshahara pekee inakusaidia kusahau ndoto zako
" Mtu alietajirika au kuwa na mafanikio kupitia mshahara huyo ni mwizi"
● ili uwe na mafanikio ni lazima uwe na chanzo kingine cha mapato
------> ooh, kumbe kila mtu ana mawazo mazuri ya aina tofauti za biashara ambazo akifanya anaweza kuingiza kiasi fulani cha pesa
-------> ila sasa tatizo ni kwamba kuweka hayo mawazo katika vitendo ndo changamoto ilipo
BRENDA RUPIA MSICHANA WA ACCOUNTING HADI KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO WA CHADEMA
Brenda Jonas Rupia ni mwanasiasa wa Tanzania na kiongozi wa CHADEMA ambaye amejijenga kupitia shughuli za uongozi wa chama, hususan ndani ya Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) kabla ya kufikia nafasi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA
Septemba 2026, alipokuwa akitoa ushahidi Mahakama Kuu kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyeketi wa CHADEMA Mhe. Tundu Lissu, Brenda alieleza kuwa alikuwa na umri wa miaka 34 na kwamba angefikisha miaka 35 tarehe 10 ya mwezi huo hivyo amezaliwa September 1991
Brenda alisoma Bachelor of Science in Accounting yaani Shahada ya Sayansi ya Uhasibu, University of Gloucestershire nchini Uingereza
Katika ushahidi wake mahakamani, alisema alianza masomo hayo mwaka 2009 na kuyamaliza mwaka 2013. Pia alisema hiyo ndiyo taaluma yake ya kitaaluma aliyokuwa nayo
Baada ya kumaliza chuo mwaka 2013, Brenda alianza kufanya kazi katika taaluma yake ya uhasibu
Alieleza kuwa aliwahi kufanya kazi kama Accountant kwenye kampuni ya TAZ’S CARS, kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya magari. Alifanya kazi hiyo kwa takribani mwaka mmoja yaaani kuanzia mwaka 2013 hadi 2014
Baadae aliacha kazi hiyo, akaanza kujishughulisha na biashara binafsi ambapo alianza biashara Kariakoo, Dar es Salaam akianza na biashara ya bidhaa za urembo, hususan human hair na baadaye akaingia pia kwenye biashara ya electronics
Kwa hiyo, kabla ya siasa kuwa sehemu kubwa ya maisha yake ya umma, Brenda alikuwa na msingi wa taaluma ya uhasibu pamoja na uzoefu wa ujasiriamali
Brenda alianza kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CHADEMA kuanzia takribani mwaka 2015
Miongoni mwa nafasi alizowahi kushika ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Mwananyamala ndani ya Jimbo la Kinondoni. Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Jimbo la Kinondoni
Baadaye alipanda zaidi kwenye uongozi wa BAWACHA na mwaka 2024 akawa Katibu wa BAWACHA Mkoa wa kichama Kinondoni. BAWACHA ni Baraza la Wanawake la CHADEMA
Hatua kubwa katika safari yake ya kisiasa ilikuja tarehe 12 Machi 2025, alipoteuliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA
Nafasi hiyo ilimfanya awe mmoja wa viongozi wanaowakilisha chama kwenye eneo la mawasiliano, kutoa taarifa za chama na kueleza misimamo ya CHADEMA kwa umma
Kwenye nafasi yake ya mawasiliano, Brenda amekuwa akionekana katika shughuli mbalimbali za chama na amekuwa akitumia majukwaa ya mawasiliano ya kisasa, ikiwemo X na Instagram, kusambaza taarifa na ujumbe wa kisiasa wa CHADEMA
Mwaka 2026 aliongeza kujulikana kwake kitaifa baada ya kuitwa kuwa shahidi wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Tundu Lissu. Katika ushahidi wake, alieleza historia yake ya elimu, kazi na nafasi mbalimbali alizowahi kushika ndani ya CHADEMA