Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo naRais wa Jamhuri ya Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa tarehe 09 Juni, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mlezi wa Mtandao wa Wanawake Viongozi Afrika (AWLN) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Liberia Mhe. Ellen Johnson Sirleaf mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 20 Aprili, 2026.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwingi wa rehema kwa kunijalia kuifikia siku nyingine ya kumbukizi ya kuzaliwa na umri wa miaka 66. Kwa moyo wa dhati, nimepokea na ninawashukuru nyote kwa salamu zenu za upendo.
Nimesherehekea siku hii kwa kupanda miti. Wito wangu kwenu, tujenge na tuendeleze utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira ili nayo yaendelee kututunza sisi na vizazi vijavyo.
Muungano wa Tanzania...
Ni mkataba wa kisiasa uliofanyika tarehe 26 Aprili 1964 kati ya Tanganyika na Zanzibar, uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo, bado ni kiini cha nguvu ya pamoja katika uchumi, usalama na utambulisho wetu kama taifa. 🇹🇿
#miminamuungano#tanzania