Mkutano wa CPHIA ni jukwaa linalowakutanisha viongozi wa serikali, watunga sera, wanasayansi na wataalamu wa afya kujadili vipaumbele vya afya ya umma barani Afrika. Rais Dkt. Samia atazindua mpango wa afya ya mama na watoto wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Addis Ababa. #AUMaternalHealthChampionSamia Suluhu Hassan
SALAMU MOJA TU YA MKONO YENYE TABASAMU INAWEZA BADILI HADITHI.
Pale Boman'gombe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, allinua mkono kuwasalimu wananchi huku akitabasamu. Nyuma kabisa ya umati, msichana mdogo aliyebebwa mabegani ili aweze kumwona Rais naye akatabasamu na kumpungia mkono.
Jioni ile, aliporudi nyumbani, alimsimulia mama yake kwa shauku kubwa, "Mama, unafikiri aliniona?" aliuliza. โNafikiri alikuona," mama yake akajibu . "Na wewe si ulimwona?"
Binti huyo alitungua daftari lake la shule chini ya swali "Unataka kuwa nani utakapokuwa mkubwa?" alifuta jibu lake la awali na kuandฤฑka jingine.
"Nataka kuwa kiongozi. Nataka kuwa Rais kama Mama Samia." akaendelea kuandฤฑka, "Nitakapokuwa Rais, nami nitatazama hadi nyuma kabisa ya umati, kama Mama Samia, ili nami nibadili ndoto ya mtoto mwingine."
Alifunga daftari lake huku akitabasamu.
Siku hiyo, ndoto mpya ilizaliwa moyoni mwake.
Yote yanawezekana. Tuendelee kuamini na kuzifuata ndoto zetu.
The Diplomat ๐น๐ฟ