BAADA ya kucheza na Mbeya City kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Tanzania akiwa na Azam FC; Kocha Florent Ibenge amefunguka kuwa ameshaona Ligi ya Bongo ni moja ya Ligi ngumu zaidi barani Afrika.
"Si rahisi. Michezo si rahisi, nadhani michuano hii (NBCPL) ni moja ya michuano migumu zaidi barani Afrika. Kwahio tunapaswa kuchukua alama kwa kila mchezo." Alisema Ibenge.
Akiongeza kuwa changamoto alizoziona zinamfanya atafute mbinu zaidi za kuliboresha kundi lake kwani hajaridhika na kiwango cha wachezaji.
Wachezaji nyota Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameonekana wakivaa beji maalum ya "Legacy" kwenye jezi zao wakati wa Kombe la Dunia 2026.
Beji hiyo imeanzishwa kwa mara ya kwanza na FIFA kutambua wachezaji waliocheza Kombe la Dunia mara tano au zaidi.
Mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala, amerejea rasmi kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kumaliza majukumu yake ya kimataifa.
Mukwala alikuwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda (Cranes) kwenye michuano ya AFCON.
Nyota wa Simba SC, Jonathan Sowah na Jean Ahoua, tayari wapo Zanzibar mapema na wameungana na wenzao kambini, wakianza maandalizi ya mechi zijazo za Kombe la Mapinduzi.
FT: YANGA SC 1️⃣➖️0️⃣ TRA United
⚽️ Ecua Celestin (29")
••
MAPINDUZI CUP 🏆
Baada ya ushindi Yanga itakutana na Singida Black Stars hatua ya nusu fainali Kombe la Mapinduzi.
KUTOKANA na mabadiliko ya ratiba ya ndege, Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, sasa inatarajiwa kuwasili Alhamisi ya wiki hii saa nne asubuhi, badala ya Jumatano saa mbili usiku kama ilivyotangazwa awali.
Kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Said Naushad ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Mbeya City.
Naushad anaungana na wachezaji Hijja Shamte na Chibad ambao wote walikuwepo Kagera.
Kiungo Ahmed Pipino anatajwa kujiunga na Klabu ya Singida Black Stars akitokea KMC FC.
Kila kitu kimekamilika; hivyo baada ya Lanso, sasa ni Pipino wote wakitokea Kino Boys.
(Ripoti: Felix)
Meneja Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema Camara anaendelea vizuri na matibabu ya jeraha la goti na kuna uwezekano mkubwa wa kurejea uwanjani mwishoni mwa mwezi huu Januari 2026.
Kwa upande wa Yakoub Suleiman, Ally amesema klabu inasubiri ripoti ya madaktari wa Taifa Stars
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumatano kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JKIA) majira ya saa mbili usiku.
Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuwa gumu kwani nyota huyo pia yupo kwenye rada za CAPS United ya Zimbabwe, ambao wanadaiwa kufikia hatua nzuri na za mwisho katika mchakato wa usajili.
(Ripoti: Felix)
INARIPOTIWA kuwa Klabu ya Singida Black Stars imefanya mazungumzo ya awali na mchezaji wa Silver Strikers, Uchizi Vunga, kuangalia uwezekano wa kupata huduma yake katika kikosi hicho.
Meneja Othmen Najjar akiwa Kocha amewahi:
🏆 Kubeba mataji 2 ya CAF Champions League
🏆 Kutwaa mataji 5 ya Ligi Kuu ya Tunisia
🏆 Kushinda mara 2 Kombe la FA la Tunisia
🏆 Kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Algeria mara 1
🏆 Kutwaa Kombe la FA la Algeria mara 1
Tunisia 🇹🇳 wamemtimua Kocha Mkuu wao Sami Trabelsi baada ya kufungwa na Mali 🇲🇱 kwenye hatua ya 16 Bora AFCON 2025.
Mechi hiyo Diarra alisimama kidete golini kuhakikisha adhabu za mikwaju ya penalti walizopewa hazitikisi nyavu zao.
BAADA ya Singida Black Stars kumbadilishia majukumua Miguel Gamondi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu; unaambiwa muda wowote kuanzia sasa mrithi wa Miguel Gamondi, David Ouma atatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.
ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Club Africain, Othmen Najjar ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Singida Black Stars atakayesaidiana kwa karibu na Kocha Mkuu David Ouma.
Othmen aliaga siku za hivi karibuni klabuni kuwa anaenda kuanza ukurasa mpya wa maisha yake.