SAKATA LA BARABARA ZA MWENDO KASI ni Kuwavuraga Wananchi.Ujenzi huchukua miaka,Inakuaje ikikamilika HAKUNA MABASI ?
Hoja za KUPITISHA MALORI au KULIPIWA zinatoka wapi ? @ACTwazalendo Inaitaka Serikali kuja na majibu ya Kwanini Mbagala mpaka ss hakuna Huduma ya DART ?
MWANAMKE 🙏🏽 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🫡🫡.
Uhandisi ni UDADISI,UBUNIFU na UTATUZI WA MATATIZO,Kwenye hayo MWENYEWE NI MWANAMKE.
@ACTwazalendo -IDARA YA MIUNDOMBINU, Inajivunia WANAWAKE WOTE ndani ya Chama Chetu.
“YOU MAKE US PROUD”
“HAPPY WOMEN’S DAY”💃🏻💐🌺
KUCHELEWA UJENZI WA SGR PORT LINK ni KUJISAHAU ama UZEMBE?Mabehewa 260+ ya mizigo yamefika zaidi ya mwezi sasa.Chakushangaza Ujenzi w Port Link HAUJAKAMILIKA.@ACTwazalendo Inaitaka Serikali kuhimiza ujenzi huo ili Kupunzia Mzigo Barabara zetu.Tumelipa gharama kubwa sana kwny SGR.
BARABARA KUBONYEA NI CHANZO KIKUBWA CHA AJALI NCHINI.
Sababu zake ni pamoja na KUPITISHA MAGARI YENYE UZITO MKUBWA kuliko uwezo wa barabara.@ACTwazalendo Inaitaka Serikali kuongeza usimamizi kwenye MIZANI.Pia kuboresha mazingira ya Reli ili mizigo yenye uzito zaid itumie RELI.
WIMBI LA WAKANDARASI WA KIGENI.
@ACTwazalendo Inaitaka Serikali kuangalia zaidi Wakandarasi Wazawa kwenye Miradi.Sheria za manunuzi na kanuni Pingamizi za thamani za Miradi kwa wakandarasi WAZAWA Ziondolewe kabisa.WATANZANIA WAKIPEWA NAFASI WANAWEZA FANYA YAFANYWAYO NA WAGENI.
@ACTwazalendo INGEKUA MADARAKANI.
Hivi VIKASHATA VYA KUKARABATI BARABARA vingekua vinakatwa na kukujazwa Muda mmoja badala kuachwa Masiku kadhaa na kuleta adha.
Pia matuta yote yangekua na alama maalum ( Reflective) Kuepuka AJALI ZITOKANAZO NA MATUTA.
@ACTBarazaKivuli
UJENZI MWENDO KASI G.MBOTO
@ACTwazalendo Tunaitaka Serikali kusimamia Wafanyakazi Kufanya kazi kwenye mavazi yote ya kulinda afya zao (FULL PPE).Pia layer za juu (leveling,Binder Surface & Seal) Ziwekwe Kwa Pamoja na Base course Kuepuka Upunjaji wa Lami na madhara mengine mengi.
BARABARA YA LAMI WAKATI HUU WA JOTO KALI, Lami hudhoofika na hivyo
@ACTwazalendo Inakukumbusha yafuatayo :
1.Barabara hukosa Mkamatano na kua laini hivyo muda wote endesha kwa tahadhari.
2.Mara zote hakiki upepo wa tairi zako uko vizuri.
3.Mara zote hakiki coolants kwenye chombo
Mabango haya ni kwa ajili ya WATANZANIA WOTE.Kuyaandika KINGEREZA ni kuwakosesha
WATANZANIA WENGI nafasi ya kujua kinachoendelea .Yaandikwe na kwa KISWAHILI na Yaongezwe taarifa kama GHARAMA,VIPIMO na MUDA wa kukamilishwa Mradi. “Transparency”
@ACTwazalendo@ACTBarazaKivuli
TAHADHARI :
UWANJA MPYA DODOMA UNAOJENGWA KWA BIL 328.6 Tshs.
Kujengwa kwa mfumo wa “design and build contract” Kichaka cha ubadhilifu na kupoteza control ya mradi.Huzaa “Potential comflict of interest”.Mkandarasi analipwa na ana design mwenyewe on process!
@ACTBarazaKivuli
KULIPIA BARABARA YA MWENDOKASI .
Pamoja na yaliyoainishwa na @ACTwazalendo juzi,
@ACTBarazaKivuli tunawaongezea kua Haitowezekana kudhibiti msongamano kwenye hiyo lane. Hivyo ni KUUA zana ya mwendokasi.
“BRT is an operation on exclusive right-of-way, with no access for others ”
@ACTwazalendo Tumesema sana swala la KUCHELEWA KWA SGR,DART MBAGALA na leo Huu wa DART G.MBOTO.
Na Kuhusu DART,@ACTBarazaKivuli Tuliwasihi kuhusu Mkandarasi huyu wa Gongolamboto.
Mpaka sasa ucheleweshaji ni zaidi ya siku 200.
WAJIBIKENI KUNUSURU HASARA KWA TAIFA.
ACT Wazalendo tunapinga vikali kauli iliyotolewa jana Februari 14, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Ndg. Abdallah Ulega, akipendekeza kuwekwa utaratibu wa kulipia matumizi ya barabara ya mwendokasi kwa wale wanaotaka kuepuka foleni. Kauli hii haipaswi kupuuzwa ni ushahidi mwingine wa jinsi serikali inavyokosa huruma kwa wananchi wake na kukosa uwajibikaji kwa maslahi ya wananchi.
Mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam ulijengwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania na hivyo ni haki ya kila mwananchi kuutumia bila vikwazo vya gharama. Kuweka ada kwa huduma ambayo ilikusudiwa kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri wa umma ni kinyume na malengo. Huu ni ubaguzi wa wazi ambapo sasa wananchi maskini watalazimika kubaki kwenye foleni kwa sababu hawawezi kumudu gharama mpya.
Aidha, mfano uliotolewa na Waziri Ulega kuhusu Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni kama jambo la mafaniko ni dhihaka kwa wananchi. Inashangaza, licha ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu ada kubwa za daraja hilo na serikali kutoonesha nia ya kushughulikia changamoto hiyo. Sasa Waziri anapendekeza mfumo huo wa uonevu uendelezwe kwenye barabara za mwendokasi. Huu ni uthibitisho kwamba serikali ya CCM haina ajenda ya maendeleo yanayowalenga wananchi bali inaendeleza siasa za kutengeneza vikwazo vya kiuchumi kwa wananchi.
ACT Wazalendo tunasisitiza kwamba:
i. Barabara ya mwendokasi ni mali ya umma na haitakiwi kuwa biashara ya kuwanufaisha wachache.
ii. Waziri Ulega angejikita kuchukua hatua madhubuti za kutatua changamoto za uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi ili kuleta ufanisi na kumaliza tatizo la msongamano, uhaba wa magari na uchakavu.
iii. Serikali ina wajibu wa kuhakikisha huduma za usafiri wa umma zinabaki kuwa nafuu na kupatikana kwa wananchi wote bila ubaguzi wa kiuchumi.
iv. Kama serikali inaona kuna haja ya kuwa na barabara ya haraka ya kulipia (Express toll road) ijenge au iruhusu sekta binafsi ijenge kwa ajili hiyo badala ya kutumia miradi iliyojengwa kwa fedha za umma au mikopo itakayolipwa na fedha za umma ili kuwanufaisha watu wachache tu (vibopa).
Tunaitaka serikali kuacha mara moja mawazo haya dhalimu na badala yake kuelekeza juhudi katika kuboresha miundombinu kwa ajili ya wote.
Aidha, tunatoa wito kwa Serikali kutafakari ujenzi wa barabara za mzunguko (ring roads) kuzunguka Mji wa Dar es Salaam ili kuyaondoa Malori kutumia barabara za katikati ya mji yanapobeba mizigo kutoka bandari ya Dar e s Salaam.
Imetolewa na;
Eng. Mohammed Mtambo
Waziri Kivuli wa Miundombinu
@ACTwazalendo .
Februari 15, 2025.
"Kauli ya kutaka kulipia barabara ya mabasi ya mwendokasi Dar es salaam inapaswa kupingwa mara moja. Barabara ya mwendokasi ni mali ya umma na haitakiwi kuwa biashara ya kuwanufaisha wachache.
Waziri Kivuli wa Miundombinu
@MtamboMJ_1#TaifaLaWote#MaslahiYaWote@ACTwazalendo
"Kauli ya kutaka kulipia barabara ya mabasi ya mwendokasi Dar es salaam inapaswa kupingwa mara moja. Barabara ya mwendokasi ni mali ya umma na haitakiwi kuwa biashara ya kuwanufaisha wachache.
Waziri Kivuli wa Miundombinu
@MtamboMJ_1#TaifaLaWote#MaslahiYaWote@ACTwazalendo