Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
Hili ndio kanisa la kusali na kutoa sadaka ya KUJIMALIZA.
Haya mahubiri huwezi kuyasikia akihubiri kibaka kama MWAMPOSA.
Leo nchi nzima tunasali kuwaombea wapendwa wetu #Mo29#TukutaneParokiani
Repost 200
Kwa yeyote amjuae huyu mama au ana mawasiliano yake au watu wa karibu wanaoweza kumpata naomba utusaidie. Mtoto wake aliuawa October 29, mama alihudhuria graduation ya mtoto na hiyo picha. Wapo wanaopendezwa kumjulia hali na kusaidia na kuwa wanae wapya. Tafadhali Retweet 🙏🏽
Mhe. Lissu: Hiyo PGO 236 inasema investigation statements sasa ni kweli kwa mujibu wa hiyo PGO mtu anayeandika maelezo ya shahidi anakuwa tofauti na huyo anayemuandikia?
ASP Geofrey Lutufye: unaweza jiandika mwenyewe.
Mhe. Lissu: PGO ya ngapi?
ASP Geofrey Lutufye : Sikumbuki
Mhe. Lissu: Ngoja nikupe PGO ujikumbushe.
ASP Geofrey Lutufye : Mi nimesema siwezi kukumbuka.
Mhe. Lissu: apatiwe PGO amepewa.
Mhe. Lissu: Sasa tuonyeshe PGO gani inasema unaweza jiandika mwenyewe.
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kukumbuka.
Mhe. Lissu: Hukumbuki au hujui.
ASP Geofrey Lutufye : Sijui.
Nimecheka sana 🤣🤣🤣🤣
Haya yote yanayoendelea KIPANYA alishasema "Media zote Tanzania ni TOILET PAPER".
Kesi ya Tundu Lissu Haifanyiki GIZANI watu wanafuatilia kwenye mitandao ya kijamiii kwa mamilioni wanaona kinachoendeles hata kama mmefunga isiruke live.
Jana Usiku Media ya ITV NA AZAM TV zote zilipewa SCRIPT moja ambayo ilikuwa na ujumbe mmoja kuelezea upande mmoja wa mashahidi wa Jamuhuru wakidai walihamasika kuvuruga uchaguzi baada ya kusmikia Tundu Lissu.
Hakuna hata media moja iliyojitahidi kuelezea yale maswali magumu ya Tundu Lissu kwa mashahidi wa kubumba ambao walishindwa kuyajibu ikiwemo yule Askari nyota mbili hajui hata PGO yake.
Haya yote MEDIA ZA BONGO zinafunika na kuripoti taaarifa ambazo zinalenga kuonyesha Lissu hana utetezi kabisa mahakamani kwenye kesi ya kubumba inayoendelea.
Huko ni kujitafutia AIBU TUU ZA KIPUMBAVU-yale yale ya kutaka kuzuia mliyofanya Gizani oktoba 29 dunia isione baadae kila kitu kipo duniani mmebaki mnalaumiana mnafanyaje.
Hii ni dunia ya tekinolojia hakuna UCHAFU UTAFANYIKA GIZANI DUNIA ISIJUE-KESI YA LISSU INAFUATILIWA KWA MAMILIONI MNAJICHOSHA KUONYESHA KWAMBA HATUJUI KINACHOENDELEA.
Na tuliamua kuandika yote yanayoendelea mahakamani tulijua tuu huu upumbavu huko mbele unakuja. Ona sasa mnaaibika, tunapowaambia mnadili na kizazi che akili kama MCHWA MUELEWE.
TUTAKUWEPO🫵😎
ukiona post hi Repost, ✌
Kila Mwananchi MTanzania mzalendo unakila sababu yaku Reposti 1000 ifike duniani hi post mwisho wa mateso sasa basi 🤲😭
DPP mfutie Tundulisu kesi ni uwonevu
Reposti 1000?
#MsiogopeTumeshinda