Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amesema,Manispaa hiyo imeendelea kufanya vizuri kwenye usimamizi na matumizi mazuri ya fedha za umma na kupelekea kupata hati safi (Unqualified Opinion) kwa mara ya 18 mfululizo kuanzia 2006/2007 mpaka 2023/2024
NASAHA ZA VIONGOZI WAKATI WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI JUNI 20,2025
"Tunarudi kwenye maeneo yetu, msije mkaharibu taswira yenu, hatutaki vurugu wala purukushani, tukafanye michakato ya Uchaguzi kwa amani, tukabishane kwa hoja ili tuweze kurudi kwenye uongozi," Mhe. Salumu Naida
NASAHA ZA VIONGOZI WAKATI WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI JUNI 20,2025
"Tunarudi mtaani,ninaomba tukacheze siasa safi,twendeni tukamsemee Mhe. Rais,twendeni tukaseme kazi zilizofanyika,tulipewa miaka mitano kama haukufanya kitu chochote usitukane watu,usimtafute mchawi" Meya Ndile
NASAHA ZA VIONGOZI WAKATI WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI JUNI 20,2025
"Niwatakie Kila lenye kheri kwenye kinyang'anyiro, nendeni mkafanye kampeni kistaarabu, zinazojali utu, tusitengeneze kampeni zitakazomuachia mtu kidonda,kuna maisha baada ya Uchaguzi" RC Mtwara
#19/03/2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. @SuluhuSamia anatimiza Miaka 4 ya Nguvu Madarakani.
Kwa Upande wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani tunajivunia na tunamshukuru Rais kwa mafanikio lukuki ikiwemo Ujenzi wa Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya, Ununuzi
wa vifaa tiba, Ujenzi wa shule mpya Msingi na Sekondari sambamba na ongezeko la madarasa katika shule mbalimbali.
Mengine ni pamoja na Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi, Matundu ya vyoo, ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, ujenzi wa Nyumba ya Watumishi na mengine mengi.
Hakika imekua
"Tupo kwenye kipindi Cha msinu wa masika, mvua zimeanza kunyesha na baadhi ya barabara zimeanza kuharibika, Niwaombe TARURA na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani mufanye ukaguzi barabara zote ili kubaini sehemu korofi na kuzifanyia marekebisho"Mhe. Shadida Ndile
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Abdallah Mwaipaya amewataka Madiwani kutumia siku tatu zilizobaki za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuhamasisha wananchi katika Kata zao kwenda kujiandikisha katika Daftari hilo ili wapate fursa ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu
Katika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Leo Januari 27,2025 , Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL.Patrick Sawala akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Abdalah Mwaipaya wamekata keki kusherehekea siku hiyo