Ndani ya masaa 48 tumefikia 10% ya 340M.
Hiki chama ni dude kubwa sana. Licha ya makelele yote wananchi wameamua kufanikisha hili na hakuna wa kuturudisha nyuma.
Hakikisha unarepost ujumbe huu unafikia maelfu ya Watanzania watimize haki yao ya kikatiba kuchangia MABDILIKO YA KWELI KWENYE TAIFA LETU.
#FreeTunduLissu
#KatibaMpya
REPOST 500
@sukununu01@joeselasini Hakuna Kupisha, Siku Rais akipisha uchunguzi wa Serikali yake kuwa na report chafu za matumizi ya Kodi za wananchi ndio Siku Heche atapisha uchunguzi.
"Wafuasi wangu kwenye social media, X (twitter), Instagram, Facebook, Tiktok, mamilioni ya Watanzania na marafiki zangu wengine wote naomba tushiriki katika hili jambo kubwa na jema kabisa la #Tonetone, tutengeneze mvua itakayotuwezesha kukomboa nchi yetu." Mhe. Lissu, Mwenyekiti Chadema Taifa.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Tanzania na Uongozi wake hasa Katambi na Mwigulu wanachekesha sana
1. Zuia mikutano tunawajadili hapa hapa kila mtu Ana mtandao,
2. TCRA zima JamiiForums na Twitter- Tutatumia VPN
3. Zuai Ruzuku ya CHADEMA- Tuna tone tone
4. Ficha Habari sisi tutaziibua
5. Msigwa atoe Ufafanuzi, atapigwa snapa hadi ajifafanue
6. Zuia Maandamano kwa wananchi! Tutaandamana raia na JWTZ
Nilipofika hapa nakumbuka hata IRAQ inatudai 🙌🏼🙌🏼🙌🏼
‼️🚨TUNDU LISSU UPDATE‼️
The Chairman of CHADEMA, Tundu Lissu, is expected to cross-examine the Commissioner General of Prisons and the Warden of Ukonga Prison in Constitutional case No. 7300 of 2026 before the High Court of Tanzania, in Dodoma. The case was opened by lawyers Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu, and Paul Kisabo against the Attorney General, the Commissioner General of Prisons, and the Warden of Ukonga Prison, requesting the court to decide on the violation of constitutional principles in the prison.
Among the main issues complained about are leaders and members of CHADEMA being prevented from seeing Lissu, as well as the eavesdropping of prison guards —listening to confidential conversations between Lissu and his lawyers when they are conducting legal consultations—a violation of the right to privacy.
🔥LISSU HAPOI‼️
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, anatarajiwa kuwahoji kwa maswali ya dodoso (cross-examination) Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga katika Shauri la Kikatiba Namba 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.
Mnyukano huo wa kisheria utaanza kesho Julai 1 hadi Julai 3, 2026. Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya mtandao (online) mbele ya jopo la majaji watatu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha, na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.
Shauri hilo lilifunguliwa na mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu, na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza, na Mkuu wa Gereza la Ukonga, wakiiomba mahakama kuamua kuhusu ukiukwaji wa misingi ya kikatiba gerezani.
Miongoni mwa mambo makuu yanayolalamikiwa ni pamoja na viongozi na wanachama kuzuiwa kumuona Lissu, pamoja na vitendo vya askari magereza vya kusikiliza mazungumzo ya siri kati ya mwanasiasa huyo na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria—jambo linalokiuka haki ya faragha.
Katika shauri hili, Tundu Lissu ametajwa kama mmoja wa wajibu maombi (Respondents), huku Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kikishiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya mahakama kukubali maombi yao.
#FreeTunduLissu
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Ujumbe Kutoka Kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania 🇹🇿 Bara John Heche.
✍️👇
🗣️”Watanzania msiogope, Nchi hii ni ya kwetu sote... Tunaipenda na wote tunatamani kuishi maisha yenye staha na heshima.
Kwa mda mrefu kikundi cha watu wachache wanatumia rasimali na utajiri wa Nchi yetu kwa manufaa yao wenyewe na familia zao.
Vijana wengi hawana ajira wakemata tamaa, hawana matumaini tena na familia nyingi zinateseka na kuishi maisha duni sana. Nyumba wanazokaa watu wetu, hali ya maji, umeme na miundombinu ni duni sana. Elimu za watoto wetu na hata hospitali zetu bado ni za chini mno.
Manyanyaso, mateso, utekaji, wizi, hujuma na kukosekana kwa haki, vimegeuzwa kuwa mambo ya kawaida kwenye Nchi hii.
Tunataka yote haya yafike mwisho, hili ni Taifa teule la Mungu, lazima liongozwe kwa heshima na nidhamu sio uhuni na vitisho.
Wakati ni sasa, msiogope ushindi uko karibu.”
#MeaMswahiliUPDATES
Siku nzima ya leo magari mawili ya polisi na polisi wakiwa wameziba nyuso zao na silaha kubwa kubwa, wamenifuatilia tangu nikiwa Urambo kwa kupokezana mpaka nafika Kigoma.. njiani nimesimama mara mbili kuwauliza shida yao ni nini kwangu hawakuwa na majibu ya maana.
Nimefika hapa Kigoma kila ninakopita na hapa Hotelin kwangu wamejaa maafisa wakiwa na nguo za Kiraia..
Mimi ni Mwanasiasa wa upinzani ninaetimiza wajibu wangu wa kikatiba… Chama chetu ni chama cha siasa ambacho kimesajiliwa na chenye haki zote katika Nchi hii.
Nimepokea taarifa nyingi kwa watu wema wakitaka niwe makini, wengine wanasema mimi na familia yangu tumetolewa maelekezo mabaya.
Nitatimiza wajibu wangu bila uoga wala hofu, hakuna mtu anaweza kuniondoa kwenye haki na wajibu wa kutetea Nchi yangu na watu wetu.
Ninawashauri watawala dhalimu kuacha kucheza na utulivu huu uliopo . Hofu haijawahi kuzaa amani, hofu huzaa hofu zaidi.
Hakuna siku nitakimbia Nchi yangu.
@Baradhuli2 People Power mnachanganyikiwa. Yaani Makamu amesema sasaivi tunaomba Lissu mikitano ikiisha Tunasimama na Maandamano Msiseme hatujawaambia. Mtangaze hali zenu za Hatari hadi mkome. Hatari number moja ni CCM NA VIONGOZI WAKE.
Hapa ni MPANDA KATAVI.
Mkoa ambao miaka miwili nyuma WALINIOKOA na kutoka kwenye Mbuga yenye wanyama wakali (MBUGA YA KATAVI).
Walinilinda siku zote 2 nilizokuwa nimelazwa kwenye hospitali yao (WanaCHADEMA).
Leo wamepokea Makamu mwenyekiti HECHE ambae amebeba injiri ya kuhubiri HAKI za ndugu zetu wanaotekwa na waliouliwa kikatili MO29.
CHADEMA ndio chama pekee nchini kinacholia na watanzania wanaolia, KATAVI mpanda ni watu ambao wameumizwa sana na hawa wakoloni weusi-leo ilikuwa zamu yao kupokea IBADA YA HAKI.
Hii nyomi inaongea namna ambavyo watanzania wamechoka na wanataka MABADILIKO.
Hongera mpanda kwa IBADA NJEMA YA HAKI LEO.
REPOST 200
#FreeTunduLissu
#katibaMpyaFreeTunduLissu
No force can stop an idea whose time haa come!
This is Mbeya - the stronghold of CHADEMA with a very rich and fertile land in #Tanzania
In October 2025, during #TanzaniaMassacre thousands were killed wantonly by police and security forces even street children and Mbeya still bears the scars! Yesterday thousands filled fearlessly the CHADEMA rally led by @HecheJohn to demand justice, #FreeTunduLissu and constitutional reforms!
Muda wa mabadiliko ulishawadia CCM na Samia wakagoma kwa risasi na mauaji halaiki kutoka na kukubali matokeo halisi ila hawawezi kushindana na mabadiliko! CCM - Mliwaua sana wana Mbeya ila oneni walivyo majasiri na bila woga wamesimama kuhesabiwa! Mtawatisha nini mamilioni waliowakataeni hata baada ya kuwaulia ndugu zao!?
Mjiandae kuondoka hakuna kingine!
Chadema hamtaweza kukiua kwa sasa kwa sababu Chadema ni yetu sote hadi tutakapopata mabadiliko - tusio wanachama na walio wanachama!
Mjipange kuondoka kutuua hamtaweza kutumaliza
#TutaelewanaTu
@godbless_lema Mh. Mkutano wa Mwisho kama Mh. MWENYEKITI WETU HAJATOKA, tunaomba hakuna kupoa, Tukeshe kila siku hadi atoke. Hakuna namana Ingine. Hii Mahakama haina haki tena. Uongozi wenu imara katika kumtoa LIssu unahitajika na unasubiriwa kwa nguvu. Msikate tamaa.
Licha Ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Tunduma Kuhamisha eneo la mkutano wetu ambapo awali lilipangwa kufanyika Tunduma mjini, na kulipeleka umbali wa takribani kilomita 15 kutoka mjini.
Lakini umbali haujatosha kuwazuia Wananchi wa Tunduma kuja kwenye Mkutano wetu, wamefurika kwa wingi tena bila kusombwa kwenye mafuso wala kupewa posho.
Chadema inapendwa sana, huwezi kuzuia Mahaba ya Wananchi kwa CHAMA CHAO.