Twende mbele turudi nyumba, wahadhiri wa Tanzania nanyi huwa mna kiherehere sana cha kuilambalamba dola miguu.
Kile kiherehere cha kuitukuza dola kwenye kila sentensi, kualika dola kwenye kila tukio, kuituza dola na kuijaza sifa, kuitetea dola kwenye kila uchafu kama mlivyofanya kwenye ule utapeli wa bandari, na mengine mengi, matokeo yake ndio kama haya.
Kipindi cha utapeli wa chaguzi ndio mpo mstari wa mbele kabisa na majezi yenu ya kijani huku mkihadaa umma kwa chambuzi za kiwaki.
Kwa kiasi kikubwa sana mmekuwa mkitumika kuhalalisha ushenzi wa dola na kuizoesha kuwaona kama dekio lake.
Umma wa watanzania unanyanyaswa na kunyonywa kuliko kawaida, ninyi ndio kwanza mnafanya kazi ya kumtetea mnyonyaji.
Hiki kiherehere kinawanyima nguvu na uhalali wa kupambana na dola kwa sababu mnaonekana kama mbuzi wa Bwana Heri kwenye shamba la Bwana Heri.
Hitaji la intellectual freedom linapaswa kuonekana kuanzia kwenye matendo ya hao wanaolihitaji.
Kuna wakati ni muhimu kuweka maslahi binafsi pembeni na kutambua kuwa hakuna aliye salama mbele ya dola dhalimu.
Leo mwenzenu ametekwa na dola, badala ya kuchukua hatua kupigania uhuru wake, ninyi ndio kwanza mnasema “tunadhani huko mbele…..”
Mbele wapi? Nini kinachowazuia kuchukua hatua kama umoja wa wahadhiri? Ni ipi kazi ya union yenu?
Mnakumbuka lile shairi la Mchungaji Martin Niemoller? Linaenda kwa mtindo unaofanana na huu:
Kwanza waliwawinda CHADEMA,
Sikupiga kelele kwa sababu mimi sio CHADEMA.
Kisha wakawawinda wanaharakati,
Sikupiga kelele kwa sababu mimi sio mwanaharakati.
Kisha wakawawinda waandishi wa habari,
Sikupiga kelele kwa sababu mimi sio mwandishi wa habari.
Kisha wakawawinda viongozi wa dini,
Sikupiga kelele kwa sababu mimi sio kiongozi wa dini.
Sasa wananiwinda mimi,
Bahati mbaya hakuna yeyote aliyebaki kunipigia kelele.
Tujifunze!!
Kwako @nchimbie , kama haya unayoyasema ni sehemu ya project ya “kukinusuru chama” naomba nikwambie kwamba baada ya October 29 hakuna chochote kitakachoinusuru CCM na hasira za Watanzania.
Watanzania tunakuomba uangalie jinsi ya KUINUSURU TANZANIA, na sio kuinusuru CCM.
CCM imeshafika mwisho….. Na mioyoni mwetu Watanzania tumeshafunga ukurasa wa CCM.
WOW……….
I will reserve my comments for now maana naogopa kuamini mtu wa CCM 100%, nikikumbuka imani niliyoweka kwa Magufuli na kampeni niliyomfanyia alafu kilichokuja kutokea basi najikuta najiambia nijipe muda ila naroho yangu inataka mnoooo kumuamini Nchimbi maana alichosema ndicho nchi nzima tunalilia………
Ila let me say again, WOW!!!!!!!!!!!!!
Ni kosa la UHAINI Tundu Lissu kudai Katiba Mpya na utawala bora - bado yuko jela!
Maelfu wameuwawa, survivors tuna makovu ya kudumu, wote tukidai Katiba na utawala bora!
Leo Nchimbi anarudia madai hayohayo, eti tutapata Katiba 2028, mnamuona shujaa!
Hebu mjiheshimu bana!