Msijifundishe lugha ya Mushrikiyn – bila ya kuwa kuna umuhimu ndani yake – wala Msiingie makanisani wakati wa sherehe zao kwa sababu Hasira za Allaah huteremka juu yao.” [Al-Bayhaqiy].
Amesema aliy ibn Abii twaalib Radhwiyallahu anhu :
Hawatoacha watu kitu katika dini yao kwa kutaka kutengeneza dunia yao ila Allah atafungua juu yao lenye madhara juu yao,na lenye shari juu yao kutokana nalo.
الزُّهد والرَّقائق لابن المبارك - (1646)
عن معاذ قال: أوصان�� رسول الله ﷺ فقال:
Kutoka kwa muadh Amesema :aliniusia Rasulullah swalallahu alayhi wasalam akasema :
(لا تشركْ باللهِ شيئًا، وإِن قُطِّعْتَ، وحُرِّقْتَ).
Usimshirikishe Allah na chochote, hata kama utakatwa au utaunguzwa.
📚 رواه أحمد في مسنده.
Amesema ibn mas'uud Radhwiyallahu anhu:
" كان الرجل منا إذا تعلم عشر آيات لم يجاوزهن حتى يعرف معانيهن، والعمل بهن "
Alikua mtu miongoni mwetu atakapojifunza Aya kumi haongezi mpaka afahamu maana yake na azifanyie kazi.
[ رواه ��بن جرير في تفسيره (81) ]