#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 493
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Naomba nimalizie hoja ya mwisho ambayo ilikuwa ni maelezo yaliyoko kwenye witness statement na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Tutawaalika D1 hadi D16, what exactly kilichofanyika ni kuonyesha ommissions kwa asilimia kubwa na hata kama kulikuwa na contradictions zilikuwa minor which do not go to tje root of the case, kwa mfano aliyekosea dini, hiyo ni contradiction inayoenda kwenye root of the case kuliko aliyesema anagari 2 then baadae akagundulika ana gari 5 yeye ndio aaminiwe?
Ushahidi wa hao mashahidi ulikuwa chini ya kiapo na wanapaswa kuaminika, maneno haya yapo kesi ya Abel Orua Matiku and others vs Republic criminal appeal no 441 of 2020.
Kwenye maelezo yote hakukuwa na inconsistency isipokuwa ommissions na ushahidi wao haujahama kutoka kwenye msingi uliopo kwenye vielelezo hivyo ina defeat kifungu cha 163 cha CPA kuhusu contradictions, na kama zipo ni very minor, ni submission yetu kwamba kwa ushahidi wetu wa mashahidi 17 tumethibitisha pasipokuacha shaka na mtakapokuwa mnachambua ushahidi mshtakiwa awe convicted as charged.
Waheshimiwa majaji naongea na wenzangu wanasema hawana cha kuongeza kwa kile ambacho nimefanya submission.
Waheshimiwa Majaji kwa kumaliza kusema hayao tunaomba sekunde 5 tuweze kuwashukuru maana shauri hili lilianza mwaka jana septemba hadi mwishoni septemba 2026 kwa kusikiliza mashahidi wetu 17 na watano waliotusaidia.
Tunawashukuru sana kwa jinsi Mahakama ilivyo to treat kama binadamu pale ambapo tulikosea. Tunamshukuru pia kaka yetu kwa umri na taaluma, mbali na maneno makali hayakuweza kujenga kitu kibaya isipokuwa tafsiri ya sheria na kwa upande wetu ilikuwa to discharge wajibu wetu katika kuthibitisha shtaka na kwa kifungu hiki ambacho kinakuwa tested kwa mara ha kwanza.
Ni hayo tu kwa upande wa Jamhuri.
Mara baada ya Wakili Katuga kusema kuwa amemamaliza kuwasilisha submission kwa upande wa Jamhuri.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa una rejoinder yoyote?
Mhe. Lissu anamjibu huku anacheka, Waheshimiwa Majaji, mimi nilimaliza jana sina lingine.
Majaji wanacheka. 😀😀😀
Jaji Ndunguru amemwambia kumchomekea akijua kabisa hawezi kuwa na la kusema kwasababu zamu yake ilishaisha.
Jaji Ndunguru anasema basi tunashukuru shitaka lilikuwa refu sana, tunawashukuru pia hata Wananchi pamoja na kwamba walikuwa wanatuchochea kufanya fujo kidogo lakini hatukuchocheka.
Kwa leo tunaishia hapa.
Ngoja tupate muda ili tuweze kufanya kitu kwa ajili ya hukumu. Tutafakari neno kwa neno.
Tarehe 06/11/2026 tutatoa hukumu.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 492
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Katuga anasema kuna hoja ilitolewa kuwa mashahidi wa jamhuri sio competent and lack credibility kwasababu they were acting under their superior Ramadhan Kingai na IGP Wambura kuwa waliwahi kushiriki kumshtaki mshtakiwa mara kwa mara.
Tunaalika Mahakama kuangalia ni sheria gani inasema hawa sio competent? Ni submission yetu kuwa hakuna sheria ya namna hiyo. Ni maneo ya Popart Emmanuel vs Republic criminal appeal no 200 of 2010 at page 5 as a regard to the reliance of witness from one office we know no law which states that they are not competent, police officers are competent to testfy, what is important is what they are saying is true. Mahakama ilisema walikuwa competent to testfy.
Kesi inayotafsiri kuwa kila shahidi ni competent ni DDP vs Sharif Mohamed and 6 Others criminal appeal no 74 of 2016 CAT walisema kila mtu ni competent to testfy mwenye knowledge na matter at issue at the trial.
Kulikuwa na hoja kuwa hawawezi kutestify sababu walijiandika maelezo yao wao wenyewe, utetezi huu haukuwa supported na kifungu chochote cha sheria rather rejea ya kifungu cha 11 cha CPA kinachosema Polisi anaweza kumuandika mtu yoyote maelezo.
Kifungu hiki hakijaweka utaratibu wa je huyo polisi anayefanya investigation anaandikwa maelezo na nani? Kwakuwa hakuna kifungu mahususi kilicho restrict police anayepeleleza kuandika maelezo yake na declaration kuahidi kuandika maelezo kwa usahihi, kwahiyo hakuna kosa linalopelekea shahidi huyo kutokuwa competent.
Waheshimiwa majaji hoja nyingine ilikuwa kwamba hao mashahidi ambao ni polisi officers na wale mashahidi ambao walichocheka wale wenye majina ya P ni mashahidi ambao wana interest to save.
Tukianza na washtakiwa ambao walikuja kutoa ushahidi kifungu cha 151 cha Sheria ya Ushahidi kinasema an accomplice shall be a competent witness, kama walichocheka na maneno ya mshtakiwa ni washtakiwa wenza.
Waheshimuwa majaji hoja kuwa mashahidi hawa wana interest to save wameiambia mahakama uongo, hoja ni kwamba waliona kideo au hawakukna,? Walichocheka au hawakuchocheka? Lalamiko kuwa wana interest to save yasichukuliwe kwa uzito, kesi ya Basil John Mlay vs Republic criminal appeal no 306 of 2018.
Part 493 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 491
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Jaji Ndunguru anamwambia Katuga, hebu rudia tena hapo.
Kutokuwepo kwa video haimaanishi kwamba mashahidi wa Jamhuri hawawezi kuthibitisha hoja ya kwamba walisikia maneno hayo ya uchochezi iliyoko kwenye YouTube channel ya Jambo.
Video ya Jambo matumizi yake ilikuwa just to back up ushahidi wa mashahidi waliosikia na sio kwamba kutokuwepo kwa video maana yake mashahidi hawa hawaaminiki. Kila shahidi anastahili kuaminiwa unless mahakama iwe na sababu za kutokumwamini shahidi huyo.
Maneno hayo yapo kwenye kesi ya Goodluck Kyanda versus Jamhuri (2006) TLR ikieleza haki ya mashahidi kuaminiwa. Kama ambavyo tumesema mashahidi waliona na wakachocheka na mshtakiwa anasema alitamka hayo maneno hivyo mtaona jinsi gani ushahidi wa defense una carry forward kesi ya Jamhuri.
Suala kwamba oral testmony inaweza kuthibitisha documentary evidence inaelezwa kwenye kesi ya Abbas Kondo Gede vs Republic criminal appeal no 472 of 2017 CAT ilisema therefore, oral evidence if worth of credit is sufficient without documentary evidence to prove a fact or title.
Thus where a fact may be proved by oral evidence it has not neccessary that documentary evidence must substitute oral evidence. Hivyo inaweza kuthibitishwa without even kutoa documentary evidenve ambayo ni video
Ni hitimisho kuwa manifestation imethibitishwa pasipokuacha shaka regardless ya kutokuwepo kwa hiyo video.
Tunajua kwamba ni jukumu letu kuthibitisha shtaka pasipokuacha shaka, ila tumewarejesha kwenye ushahidi wa Jamhuri, mahakama inapotoa uamuzi inalazimishwa to consider utetezi wa mshtakiwa, ni rai ya Jamhuri kuwa mahakama ni muhimu kuangalia theory ya defense na ni wazi kwamba ushahidi wa utetetzi umeshindwa kabisa kuonyesha doubt ushahidi wa Jamhuri.
Katika kujaribu kuweka matundu kwenye prosecution case, upande wa utetezi ulisema kulikuwa na mikanganyiko na mapungufu katika ushahidi. Waheshimiwa majaji mapungufu ambayo yalionyeshwa na upande wa utetezi ni minor na hayana madhara kwa maana hayaendi to the root of the case.
Minor contradictions ni vitu ambavyo haviepukiki wakati wa trial kwasababu kila shahidi anatoa ushahidi jinsi alivyoona, alivyosokia yaani zile sense za ushahidi.
Minor contradictions na discrepancies ni msimamo wa kisheria kwamba zinaithibitishia mahakama kuwa sio mashahidi waliokuwa coached before testfying rather wanatoa ushahidi kulingana na nature ya ushahidi wao.
Ni msimamao wa kisheria kwamba contradiction ambayo haiendi to the root of the matter ichukuliwe kawaida tu. Kuna neno la kilatini linasema De minimis non curat lex , meaning “The law does not concern itself with trifles.”
Waheshimiwa majaji haya maneno yanatoka kwenye kesi ya Mussa Mbelechamo vs Republic criminal appeal no 912 of 2023 katika ukurasa wa 8 wanasema minor contradictions do not affect conviction.
Ni submission yetu hizo minor contradictions does not affect the root of the case..
Part 492 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 490
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Waheshimiwa majaji kwanini mashahidi watatu kati ya 17 wa Jamhuri wameeleza maneno ya law and order? Kifungu cha 132 cha Cap 6 kinasema hakuna namba mahsusi ya mashahidi inayotumika kuthibitisha existence ya hoja fulani, hata mmoja anatosha, mbali na namba hii ya mashahidi wa jamhuri kuthibitisha na kufafanua kwanini maneno ya mshtakiwa ni uhaini inatosha kuthibitisha.
Naomba niende sasa hoja ya tatu kama nia ya mshtakiwa ilidhihirishwa. Tumeomba mahakama ku note kwamba hakuna dispute kuwa mshtakiwa alitamka hayo maneno, hoja mnayotakiwa kuitolea uamuzi kuwa aliisambaza? Ambapo kwenye Oxford Dictionary publication is to make something known to the public.
Ukiangalisha ushahidi, manifestation ilifanyika by deed of uttering and publishing alleged words (kwa kitendo
Chake cha kutoa na kusambaza, kutoa maneno hayo kwa umma).
Kuhusu kusambaza hapa kuna aina mbili ya publication ya haya maneno. Maneno haya kwanza yalisambazwa kwa mara ya kwanza tarehe 3/4/2025 kwa watu walioko kwenye mkutano, ikiwemo PW17 katika ukurasa wa 491 anasema alisikia mshtakiwa akisema tutazuia uchaguzi na tutakinukisha, kwahiyo tayari kwa shahidi huyu hiyo nia ilikuwa known, ilikuwa communicated kwa huyu shahidi lakini ni ushahidi pia kuwa DW2 anakiri kuyasikia hayo maneno na DW3, DW4
Publication ni to make it known kwahiyo haya maneno yalikuwa communicated kwa watu waliokuwepo kwenye mkutano. Maneno haya pia yalisambazwa kwa umma kwenye social media specifically YouTube.
PW17 alisema kwamba walikuwa wanafanya livebroadcasting ya mkutano huo, ushahidi ambao umeungwa mkono na upande wa utetezi na ililetwa hoja kuwa mshtakiwa sio yeye aliyealika mkutano wala kuwaalika waandishi wa habari.
Ukisoma ushahidi wa PW17 katika ukurasa wa 497 anasema, we livestreamed the video through you. Kuhusiana na ushahidi wa mshtakiwa kwamba sisi mimi niliyefanya mkutano, is immaterial, suala la mahakama kujiuliza ni kwamba mshtakiwa alisambaza au hakusambaza?
Aliandaliwa speech au hakuandaliwa? Majibu ya utetezi ni kuwa hakuandaliw speech, ni ushahdii wa mshtakiwa katika ukurasa wa 590 anasema we held the meeting which is the subject of this case na through huo mkutano ndio alisambaza hayo maneno. PW17 nae alisema kuna muda alisema waliambiwa waondoke kwaajili ya mambo yao mengine ya ndani
Mshtakiwa alisema pale ambapo tunataka kupublish matter zetu kwa umma tunaalika waandishi wa habari. Mkutano ulikuwa livestreamed, alitaka umma ujue, umma umejua anasema tena yeye hajasambaza. Waheshimiwa majaji tunatafsiri sheria kiupande upande, kwa ushahidi huu ni wazi mstakiwa alikusudia na amesambaza nia yake kwa umma , hivyo tunasema jamhuri imethibitishwa pasipo na shaka.
DW3 anasema mshtakiwa alitaka taarifa yake iufikie umma wa watanzania, mshtakiwa mwenyewe anasema kuwa ukiona waandishi wa habari ni kwamba wanataka taarifa yao iwafikie umma.
Utetezi wao ni best evidence kwasababu mshtakiwa alitaka taarifa yake iwafikie umma waweze kuchocheka, baada ya kuchocheka walikamatwa, wakatoa ushahidi mahakamani.
Waheshimiwa majaji mnaweza kuambiwa kwamba hao mashahidi wanaosema waliiona video, video iko wapi?
Video ni moja ya electronic evidence, ushahidi wa ki elektroniki ni document kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Ushahidi.
Ikiwa document inamaanisha ni moja ya admissible document, kuna oral testmony, kuna real evidence (ushahidi wa exhibits), hizi aina sa ushahdii kisheria hakuna kubwa zaidi ya mwenzie. Absence ya documentary evidence haimaanishi kwamba it can be proved by oral testmony.
Part 491 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 489
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Katuga anasema Treasonable intention ya mshtakiwa pia inathibitishwa kwa kauli aliyoitoa tarehe 03/04/2025 hapa pia upande wa Jamhuri unabebwa na upande wa defense, DW4 Brenda Rupia yeye anasema alikuwepo tarehe 03/04 na alimsikia mshtakiwa akisema kwani tukikinukisha watatuua?
Si watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini? Hivyo mshtakiwa alitamka akiamini kuwa atafunguliwa kesi ya uhaini. Ni kitu gani ambacho Waheshimiwa majaji mtakitafuta kuthibitisha nia ya uhaini??
Waheshimiwa Majaji kwenye shauri nililolitaja ushahidi wa mshtakiwa ni the best evidence dhidi yake alivolunteer kuyasema hayo.
Waheshimiwa majaji mahakama yenu sasa itajiuliza kweli zile kauli zilichochea umma? Upande wa mashtaka umeleta mashahidi waliochocheka na maneno ya mshtakiwa na wanatoka sehemu tofauti tofauti ya umma wa watanzania ambao ni named kama P. Mashahidi hao wote waliiambia mahakama ni kwa jinsi gani walichocheka na maneno ya mshtakiwa, wanachama, wafuasi, wengine wapenzi wa mwenyekiti ambaye hapa ni mshtakiwa.
Kwenye ukurasa wa 397 wa records unaonyesha kwamba alichocheka kwa kiwango ambacho kinamleta chuki na alipanga kumsapoti mwenye kwa kuungana kupinga kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kuwapiga na kuwarushia mawe.
Ushahidi wa mashahidi hawa unaungwa mkono na DW2,3,4 waliunga mkono kuwa mshtakiwa hakufafanua alipotamka maneno tutazuia uchaguzi, au tutahamasisha uasi, tutavuruga uchaguzi au kukinukisha.
Ushahidi wa utetezi ni kwamba watu waliosikia hotuba ya Mwenyekiti wana haki na kutafsiri kwa kadri wanavyoona inafaa.
Point hiyo tunasema hao watu wana haki ya kuamini na kufanyia kazi uchochezi uliofanywa na mshtakiwa tukikopa ushahidi kutoka kwa mshtakiwa mwenyewe akiiambia Mahakama kuwa yeye ni mtu wa kuheshimika na kuaminika na watu, huu ushahdii nao pia una carryforward kesi ya Jamhuri kwani anaaminika na kuheshimika.
Ni submission yetu kwamba kupitia haya maneno kwenye hati ya mashtaka na ushahidi wa Jamhuri ulioungwa mkono na upande wa utetezi ni wazi kwamba mshtakiwa aliform intention to isntigate the public to intimidate the public na kwamba maneno hayo yalilenga Serikali yenye wajibu wa kusimamia sheria na kuvuruga uchaguzi ni kuitisha mamlaka inayosimamia sheria ambayo ni serikali.
Maelezo kuwa maneno hayo yalitolewa kwa nia ya kuitishia serikali yaliungwa mkono na ushahidi wa PW16 kwenye ukurasa wa 445, kuwa kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi yalilenga kuvuruga amani ya nchi.
Maneno ya shahidi huyu yanaungwa mkono na ushahidi wa DW1, ukurasa wa 619 anasema serikali ina wajibu wa ku administer na kuenforce sheria zilizotungwa na Bunge na ukurasa wa 622 kuwa Police ndio wana maingain law and order na ukuraswa wa 813 DW4 Brenda alisema ni Police ndio wanawajibu wa maintain peace and security na DW5 alisema executive ndio ina wajibu wa to maintain peace and ordee.
Waheshimiwa ni rahisi sasa kuona kumbe kuchochea umma, kuvunja amani ni as good as good ni kumtisha yule mwenye majukumu hayo ambaye ni executive regardless kama ametishika au hajatishika, hivyo maneno hayakulenga Mahakama au Bunge.
Waheshimiwa Majaji Ibara ya 147(2) ya Katiba ya JMT inaelekeza kwamba serikali itakuza na kuimarisha majeshi ya aina mbalimbali kwaajili ya usalama na ulinzi wa watu wa Tanzania.
Ushahidi wa PW16 unaungwa mkono na kifungu cha 5(a)(b) cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Wasaidizi wake Cap 322 kwamba ni jukumu la serikali kulinda amani.
Hapa pia tunakopa ushahidi wa DW1 kwamba Polisi inafanya kazi chini ya Serikali na iia jukumu la to maintain law and order ukijumuisha na kesi ya Hamisi chuma supra hivyo unavyotishia jeshi la polisi unatishia walinzi wa amani ambao ushahidi huo umeungwa mkono na DW1-DW4.
Part 490 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 488
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Katuga anasema Mashahidi wote wa Jamhuri waliyosikia hayo maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, walisema waliyasikia kupitia YouTube ya Jambo Tv na PW17 mtumishi wa Jambo Tv aliyasikia na kuyarusha moja kwa moja.
Wakati wa maswali ya dodosa kuhusu kutamka maneno hayo, mshtakiwa hakudodosa ila tu alisema maneno hayo yanatengeneza kosa?
Hivyo ushahidi huo haukudodoswa na uliungwa mkono na mashahidi wote wa utetezi, mshtakiwa mwenyewe alisema ni kweli alitamka hayo maneno lakini anachokipinga yeye ni kuyasambaza kwa umma, DW2 alisema pia mshtakiwa alitamka hayo matamshi.
Kwahiyo kupitia ushahidi wa jamhuri ulioungwa mkono kuwa hakuna dispute mshtakiwa kutamka maneno haya tarehe 03/04/2025
Hivyo hayo maneno yaliyotokana na hotuba ndefu ya mshtakiwa ni maneno yenye sentensi timilifu na zenye kueleweka. Ushahidi uliotolewa na jamhuri umeelezea jinsi ulivyoyapokea na kuyaelewa hayo maneno na yalieleweka kwa mashahidi wa upande wa jamhuri, PW1 alieleza kuwa maneno hayo yalilenga kuitishia serikali.
Mbali na mashahidi kusema kuwa waliyaelewa na kuyatafsiri, bado ushahidi wao unaungwa mkono na ushahidi wa DW3 ambaye nae anaunga mkono kwamba maneno yalikuwa quoted kwenye hati ya mashtaka ni maneno yaliyotimilika na yenye kuleta maana, vilevile DW4
Waheshimiwa majaji sasa tuyatafsiri basi maneno yenyewe tuone kama yana maana au hayana maana, neno uasi limetafsiriwa kwenye kamusi kuu ya kiswahili kwa kumaanisha kwamba uasi ni kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu kwa lengo la kujaribu kubadili mfumo wa kisiasa wa nchi yao.
Tafsiri ya pili uasi ni kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka au kupinga sheria na taratibu zilizopo kama vile katika taasisi, shirika au chama (kisawe chake yaani synonymous yake ni uhalifu. Kwa mazingira ya kesi tafsiri ya kwanza ndio ina fiti.
Ni ushahidi wa DW3 katika ukurasa wa 819 slogan ya no reforms no election ililenga kuleta mabadiliko kwenye siasa za nchi. Kwenye ukurasa wa 829 DW3.
Tunajua sio jukumu la utetezi kuthibitisha kesi lakini ni msimamo wa kisheria kwamba ushahdii wa defense unaweza kuibeba mbele kesi ya Jamhuri.
Msimamo huu upo katika kesi ya Hamisi Chuma Hando Muhoja versus Republic criminal appeap no 36 of 2018 citing with approval case ya Haruna mtopeni vs R CAT ilisema accused person akitoa ushaidi unaoipeleka kesi ya jamhuri mbele mahakama itatumia ushahidi huo katika kuamua kuhusu hatia yake.
Nimeleta hii kesi japo ushahidi tunaoutumia ni wa Brenda Rupia shahidi wa defense tunaomba mahakama hii iutumie na tafsiri ya kwanza ya neno uasi. Tafsiri ya neno uasi lilikuwa ni kuhamasisha uvunjaji wa sheria ili kuleta mabadiliko.
Part 489 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 487
Tumerejea mchana huu baada ya mapumnziko.
Anasimama Katuga anasema quorum iko kama asubuhi na wako tayari kuendelea.
Anasema naomba kuendelea na kiini cha shitaka namba 2 baada ya kile cha kwanza kwamba mshitakiwa ana duty ya utii.
Upande wa Jamhuri unasema kwamba mshitakiwa kwa ushahidi uliotolewa imethibitika kwamba alitengeneza nia ya kuchochea umma kwa nia ya kuitisha serikali ili ifanye yale anayoyataka.
Na hiyo ni kutokana na sentensi au maneno yakiyotamkwa na mshitakiwa na upande wa mashitaka kuyanukuu kwenye hati ya mashitaka.
Maneno hayo utaona mshitakiwa akieleza umma kwamba kuhamasisha uasi ni namna ya kupata mabadiliko. Utaona anasema kukinukisha ni namna ya kupata mabadiliko.
Kwahiyo maneno yenyewe yaliyotumika kwenye mashitaka yakithibitishwa yametamkwa na mshitakiwa tafsiri yake vile yakivyokaa yalilenga ku compel kuitishia serikali iweze kufanya anayoyaamini mshitakiwa yanatakiwa kufanywa.
Waheshimiwa Majaji neno uchochezi au instigation kwenye hati ya mashitaka kabla ya kwenda kutengeneza nia ya ku instigate ni busara tunaona Jamhuri tupate tafsiri ya neno to instigate.
Katika Mahakama Supreme Court ya India katika kesi ya Mahendra KC vs State of Karnataka and another Criminal Appeal No. 1238/2021 walidefine to instigate
Is to provoke, insight, ....
Katuga kingereza chake kina matege sana haeleweki anatakamka nini? Mdomo mzito unaweza kudhan anaongea kisukuma.
Kwa tafsiri hiyo unaweza kuwa uchochezi maneno au conduct lakini uchochezi huo labda u suggest madhara au unajitosheleza na uchochezi huo uwe capable kuwekwa hadharani.
Sasa Mahakama tunaialika iyapime maneno yakiyopo kwenye hati ya mashitaka kwamba yalichochea umma kwa nia ya kuitisha Serikali.
Tunaomba Mahakama i note kitu muhimu kuhususiana na maneno haya. Maneno haya hayajakubalika katika kipindi cha PH lakini wakati wa usikilizwaji upande wa Jamhuri kupitia mashahidi wake 16 isipokuwa PW 3 walieleza kumsikia mshitakiwa akitamka maneno haya yaliyotamkwa kwenye hati ya mashitaka.
Part 488 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 486
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Kuna simu imeita kama dakika mbili hivi ya mzee sana, Jaji Ndunguru amesema atoke nje akazime simu yake, ni mzee sana, hata kuitoa simu ilipokuwa imekuwa shida sana
Ilikuwa break kidogo
Ushahidi huu unaonyesha maana ya Executive na linamfanya mshtakiwa aweze kuandaa ushahidi wake, kilichotishwa ni Jukumu la Serikali katika to maintaib peace, law and order. Mahakama ikijiuliza Executive iliyotumika kwenye hati ya mashtaka ni ile iliyopo kwenye sheria na ushahidi uliotolewa.
Important point to cosnider kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambayo inaweza kuwa sub element ya kifungu cha 39 ambayo hati ya mashtaka imetumika kumshtaki accused iliachana na neno deed ikatumia for the purpose of intimidating Executive, it is our submission kwamba neno lililotumika hapo linamaanisha whether the executive is intimidated or not is immaterial.
Hivi sasa ni saa saba tunaomba break ya one hour
Jaji Ndunguru mshtakiwa unasemaje?
Lissu: Ni sawa
Jaji Ndunguru: mnaintend kumaliza leo?
Katuga: sisi tunajikita kwenye hoja ili tumalize waheshimiwa majaji sisi hatutataja mambo ya pilau sisi hatutajikita huko
Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi saa nane na robo
Imepigwa High Coooouuuuurrrrrttt
Majaji wanatoka
Tukutane saa nane na robo.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 485
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Waheshimiwa Majaji baada ya kuthibitisha hoja ya kwanza mahakama inabaki na hoja mbili tu kama mshtakiwa aliform intention kwa nia ya kuitishia Serikali. Neno Serikali kwenye kifungu cha 39(2)(d) limetumika tu neno Executive, Judiciary na Legislature.
Kifungu chote cha 39 cha Kanuni ya Adhabu hakuna tafsiri mahsusi ya neno Executive wala judiciary, kwamba tukisema judiciary tunakuwa tumemtishia nani , wakati gani na alikuwa wapi wala Executive wala Legislature.
Sio kwa kifungu hicho tu ila sheria nzima ya Kanuni ya Adhabu haina tafsiri ya neno Serikali, the same na Judiciary rather judicial proceedings zimekuwa defined na Legislature haijawa defined.
Ni msimamo wa Sheria kwamba inapaswa kutafsiriwa kama ilivyo au kama inavyopaswa kusema na aina hii ya utafsiri wa sheria ni plain meaning, katika kesi ya Nasibu Abubakari Ras versus Republic Criminal Appeal No 146 of 2021,
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania at Mbeya ilirejea shauri la jinai la Jamhuri versus Mwesige Godfrey and Another (19/02/2015) ambapo mahakama hii ya rufaa ilirejea kesi ya US Supreme Court kwenye kesi ya Caminetti verus United States 242 U.S, 479 - 227 (1917) it is elementary that the meaning of statute must in the first instance be sought in the language in which the act is formed and if it is plain.., the sole function of the court is to enforce it according to its terms, kwamba sheria itafsiriwe kwa lugha yake ambayo iliitengeneza kama inaeleweka na ni jukumu ka mahakama kuweza kuitumia jinsi ilivyo (plain meaning rule), ilicitiwa kesi ya Connect Cutt Nat’l bank verus R No 112 held that courts must presume that legislature linasema kwenye sheria kile ambacho kipo na chenye maana ya sheria ambacho inasema.
Kwenye kifungu cha 39 imetaja Executive without mentioning nani kwenye executive. Kama tulivyoeleza awali kazi ya hati ya mashtaka ni kumpa taarifa mshtakiwa kuhusiana na mashtaka yanayomkabili.
Ni msimamo pia wa kesi mbalimbali Mahakama ya Rufaa ikisema kuwa mshtakiwa anaweza akawa further informed na aina ya mashtaka yake kulingana na ushahidi utakaotolewa na Jamhuri.
Chargesheet can be explained or cured by evidence, imesemwa kwenye kesi ya Damian Luhede verus Republic Criminal Appeal no 501 of 2007 (reported Tanzlii 1/3/2012) katika kesi hii walikuwa wanaona kama kuna element moja ya shtaka haikuwa explained kwenye charge lakini ilikuwa cured na ushahidi kwenye ukurasa wa 5.
Waheshimiwa majaji naomba kuwaalika kwenye ushahidi, hati ya mashtaka. Mahakama yenu itaangalia nature ya ushahidi na utetezi.
PW1 katika ushahidi wake aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa la uhaini kwamba mshtakiwa alitoa hayo maneno alilenga kuitishia serikali kwakuwa serikali ndio yenye jukumu la kulinda sheria na kwamba uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria hivyo kutishia kuzuia uchaguzi ni kuitishia Serikali.
Lakini pia PW16 katika ukurasa wa 445 ameiambia mahakama kwamba maneno tutavuruga uchaguzi, tutahamasisha uasi yalilenga kuitisha serikali ambayo ina jukumu la kulinda nchi na maneno hayo yalilenga kutishia amani na utulivu, maneno hayo hayakulenga tu kuvuruga amani na utulivu bali yalilenga kuzuia uchaguzi unaofanyika kwa mujibu wa Katiba na Sheria ambayo ni kazi ya Government to enforve hizo sheria.
PW16 aliendelea kusema kuwa njia za kuzuia uchaguzi zilizotumika ni kupiga watu mawe, kuwazuia wapiga kura na ushahidi huo unaungwa mkono na mshtakiwa mwenyewe DW1 katika ukurasa wa 619 alisema Executive is responsible for administering and enforcing laws enacted by the Parliament lakini katika ukurasa wa 622 mshtakiwa pia anasema jukumu la to maintain peace and order ni jukumu la Polisi na kuwa ina operate chini ya serikali
Part 486 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 484
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Katuga anasema Waheshimiwa Majaji baada ya kuangalia maana ya kuthibitisha beyond reasonable doubt. Twende sasa tukaangalie ni kitu gani ambacho upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha. Katika kuangalia hili ni kuangalia viini au elements za kosa la jinai baada ya kuvitohoa kutoka kwenye kifungu cha 39. Kwa unyenyekevu waheshimiwa majaji tunaiomba mahakama ijiulize maswali yafuatayo
1. Kwa mujibu wa mashtaka haya, mshtakiwa ana wajibu wowote wa utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
2. Kama mshtakiwa alitengeneza nia kuchochea umma kwania ya kuitishia serikali.
3. Kama mshtakiwa alidhihirisha nia yake hiyo kwa kitendo cha kutoa na kusambaza maneno.
Hivi ndio viini vikuu ambavyo tunaomba Mahakama ijiulize, iache masuala ya mwanasiasa kwasababu hana immunity, suala la mzalendo kwani wapi yeye ana immunity?
Viini hivi ukiviangalia haviendi mbali na viini vilivyojadiliwa katika Ukurasa wa 14 wa Hatibu Gandhi na wenzake , Mahakama ya Rufaa ilichambua viini vitatu ial kesi hii ilihusisha kifungu cha 39(2)(a) na kiini a) ni allegience to the United Republic b) kama accused waliform nia ya uhaini na c) kama walidhihirisha nia hiyo by overt act.
Waheshimiwa majaji viini hivyo vinafanana na tulivyovitaja isipokuwa tu kwenye Hatibu Gandhi Mahakama ilipojadili manifestation by overt act, kesi iliyopo mbele yenu tunaomba mtafsiri manifestation by deed
Kwenye hivi viini yafuatayo ni majumuisho yetu ya kwanini vimethibitishwa na upande wa Jamhuri. Tukianza na kiini cha kwanza kama mshtakiwa ana duty of allegience to the URT. Kiini hiki hakikupingwa wakati wa hoja za awali zilizofanywa mbele ya Mahakama hii tukufu, ilikuwa ni moja ya undisputed facts kwenye preliminary hearing iliyofanyika 22/09/2025 na kurekodiwa kwenye memorandum of undisputed facts kwenye ukurasa wa 133 ya proceedings.
Dhumuni la kufanya preliminary hearing kwa mujibu wa kifungu cha 198 cha CPA R:E 2025 zoezi hili is not for cosmetic use, ni zoezi ambalo nia yake ni kuspeed trial kwa kuchambua yale yote yasiyobishaniwa na jambo lolote linaloandikwa kwenye memorandum of agreed facts inamaanisha yale yaliyokubaliwa hayahitaji further proof unless Mahakama itaona kuna haja ya kufanya hivyo. Haya sio maneno ya Katuga ila yapo kwenye kifungu cha 198(4) kwamba undisputed facts hayahitaji formal proof.
Baada ya hoja ambazo zimekubaliwa, ni jukumu kwa upande wa jmahuri kuthibitisha kile inachokituhumu sio kila undisputed facts, kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Ushahidi wajibu wa kuthibitisha wa Jamhuri ni yale inayoyatuhumu sio yote yaliyokataliwa wakati wa preliminary hearing.
Waheshimiwa majaji tuhuma zipo kwenye hati ya mashtaka, summary of evidence hazitengenezi tuhuma ila zinasomwa kwania ya ku identify mambo yasiyobishaniwa, hata the way zinavyotengenezwa ni kumpa nafasi mshtakiwa nafasi ya kuzielewa na kuzijibu. Zile summary of evidence matumizi yake yanaishia hapo na kinacho prevail ni memorandum of agreed facts. Tunaleta haya kutanua uelewa, ikitokea mtu akasema kwamba kwenye PH alituhumiwa msikubaliane nae kwasababu summary of evidence sio tuhuma.
Part 485 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 483
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Kwahiyo Public inazungumzia watu kwa mujibu wa kifungu hicho kama mashitaka yanamuhusu a person you have to mention that person.
Waheshimiwa Majaji ili uzungumzie group la watu ni lazima utaje hilo group.
Instigation ililenga group of person ulipaswa ulitaja hilo group.
😂😂😂 msiojua sheria mnateseka hapa. Kuna uchambuzi napewa hapa unanifurahisha sana niwaletea.
Kwahiyo ni neno gani litaconclude kama aliyekuwa amechocheka ni mtu mtu mmoja au kikundi cha watu.
Jamhuri ilimtuhumu mshitakiwa kuchochea umma kutokana na aina ya maneno na ushahidi ulivyokuwa hakulenga mtu mmoja au kikundi cha watu.
Kwahiyo tunachoweza kusema ni kwamba tulipotumia Public maana yake ni group of persons. Kwahiyo maana ya Public ni group of persons pia.
Sasa turudi kwenye nia sasa ya kutenda kosa hilo.
Kwenye kusambaza kuna mambo mawili maandishi au michoro au by overt act or by deed
😂😂😂 yaani kiswahili cha printing cha KATUGA ni Michoro, analeta mambo kama yale ya machawa wa Mbowe walioenda Ubwabwani wakiulizwa No Reforms, No Election maana yake nini wanasema maana yake ni kupandisha joto, tusomesheni watoto jamani.
Sasa mashitaka yake ni ku atter na kupublish yaani kutamka kusambaza, sasa kwenye manifestation haya maneno overt act na deed yanaonesha wazi kuwa they are not similar.
Blacks Law Dictionary imesema deed is as something that is done or carried out.
Lakini the same dictionary imedefine overr act kwa is an outward, physical manifestation of the….. especially by the conspirator and an overt act can constitute an overt act of conspiracy
Kwahiyo haya maneno they are not similar.
Waheshimiwa Majaji kuonesha utofauti kwenye kesi ya Khatib Gandhi and others vs R TLR 196. No. 12 at page 67
Walijadili overt act by individual wakasema maneno ya individual hayatoshi kuwa ni uhaini kwahiyo hakukuwa na tendo la conspiracy pale.
Kwenye kesi hii kuonesha overt act is something not applicable, hii kesi mpya nchini kwetu, hapa ni manifestation ya deed tu.
Oxford dictionary imedefine manifest is to show something cleary especially attitude and feeling or quality.
Kwahiyo hiyo ndio maana ya manifest.
Hati yetu ya mashitaka ni very interesting. Manifestation tuliyosema ni kutoa na kusambaza maneno.
To utter means using or dealing with and attemting to use kwahiyo nimesema utter ni kitendo kinachopaswa kiambatane na kitu mbele.
Sasa Mahakama tukufu inaweza kujiuliza uttering words maana yake kwenye Penal Code kuna makosa ya kutumia uttering of maneno ya kuudhi.
Waheshimiwa Majaji kwa kuelezea kwa kirefu kidogo naomba nigusie kidogo kwenye adhabu.
Kifungu hiki cha 39(2)(d) Cha Penal Code kinasema atakuwa liable to conviction to death.
Kwamba shall be liable naomba hayo maneno yawe ni bold kwasababu mwanzo mwisho upande wa utetezi adhabu ya shauri hili ni kunyongwa tu.
Matumizi ya neno shall be liable ni msimamo wa sheria kwamba adhabu katika shitaka hili ni kuanzia 0 up to death penalty. The maximum penalty in death by hanging.
Mahakama yenu ina decretion yake ya kuamua aina ya adhabu.
Bahati John vs Jamhuri imesema the word shall be liable is not mandatory but it set the maximum penalty.
Kwahiyo Mahakama kwa utashi wake inaweza kutoa adhabu yoyote.
Pia sentence guideline ya 2023 inasema shall be liable maana yake mahakama itaangalia utashi wake kumpa adhabu mshitakiwa.
Sasa sisi ndio tuna jukumu la kuthibitisha mashitaka tuliyoleta lakini pia kupitia ushahidi wa utetezi wametusaidia sana kuthibitisha kesi yetu badala ya kuonesha matobo.
Ku prove beyond reasonable haina maana ku prove beyond shadow of doubt.
Part 484 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 482
Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission.
Katuga anasema Waheshimiwa Majaji intention to instigate person or group of person na mimi nikiangalia hati ya mashitaka ya Jamhuri imesema ali instigate umma kwa ujumla wake.
Nitaeleza hapa kwanini? Hati ya Mashitaka ilisema watu walichochewa ili wafanye nini? Aliuchochea umma wa Tanzania ili kuzuia General election ya 2025.
Hati yetu ya mashitaka iliachana na neno deed ikachukue neno for the purpose of intimidating the Executive na hapa ikaachana intimidating legislature or the Judiciary.
Kwahiyo ikabakiza intimidation ya Executive. Lakini tukiendelea kwenye hati yetu ya Mashitaka utaona kwamba ile njia aliyoitumia nia yake hati ya mashitaka iliachana by publishing any writing or printing by an overt act na imeachana na manifestation ya hiyo nia kwenye ku publish hiyo njia by overt act ikaacha.
Lakini ikachukuliwa manifestation by his deed kwa kitendo chake cha kutoa na kusambaza hayo maneno.
Sehemu zote nilizokuwa nasema hati ya mashitaka imeacha haya imechukua haya.
Mfano publication by writing or printing tumeacha na kuchukua nyingine mfano deed maana yake hayo maneno they are not similar unless ikitumika or basi sheria iwe imesema expressly kwamba maneno hayo yaongezwe. Neno lililotumika ni or sehemu zote.
Naomba nirudie hapo, anaaanza mwanzo.
NB. Kwa kifupi kumuelewa Katuga ni kazi sana.🤧
Kokote pale katika kutafsiri sheria linapotumika neno OR huwezi kuyakusanya kama kiroba ukaweka yote kwenye hati ya mashitaka ndio hati inakuwa defective.
Neno similar au maneno mengine yanayoonesha similarity yawe added ndio neno or lisitumike.
Haya maneno ambayo or imetumika kwenye hati ya mashitaka hayawezi kutumika kwa pamoja.
Neno or linapotumika sio utaratibu wetu bali Bunge lilitunga sheria kifungu cha 13 cha Sura ya Kwanza, Sheria ya TAFSIRI ZA SHERIA R.E 2023.
Kinasema hivi in relation to written Laws but Subject to subsection 4 when the word "or" used hautaweza kuyatumia kwa pamoja utakachagua moja.
Ili kuifanya hati ya mashitaka ieleweke tulichagua maneno ili hati ya Mashitaka ieleweke. Tulifanya hivyo tukiwa tunajua hati ya mashitaka ni muhimu sana ili kumtaarifu Mshitakiwa kuhusu mashitaka aliyokuwa nayo na aweze kujitetea.
Kifungu cha 39(2)(d) kimeanza na neno any person yanaonesha ni mtu yeyote mwenye utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hili neno Any Person halijamuondoa mtu yeyote labda awe na immunity.
Mtu mwingine anaweza kusema yeye ana cheo gani au mwanasiasa kwamba atakuwa excluded pale atakapoitisha Serikali.
Kifungu hiki hakijachambua huyo any person ametokea wapi?
Waheshimiwa Majaji niliomba kuwa nitasema pale kwenye kuhusu mtu yeyote au kikundi cha watu. Tumetumia neno Public, pale
kifungu kinapozungumzia watu watakaokuwa instigated yaani kushawishiwa. Sisi tumetumia neno umma badala ya mtu yeyote au kikundi cha watu.
Waheshimiwa Majaji tumetumia neno public kuleta clarity in term of the evidence intended in the evidence tuliotegemea kuutoa.
Kwamba Jamhuri ilipanga kuleta ushahidi gani hivyo hati ya mashitaka tunaiweka kama kifungu cha 135 cha CPA kuhusu namna Hati ya Mashitaka inavyotakiwa kuwa.
Waheshimiwa Majaji ......
Jaji Ndunguru: Sasa uongeze sauti hatukusikii kabisa.
Tulitumia neno PUBLIC ili kuifanya hati ya Mashitaka iweze kueleweka kwa mujibu wa kifungu cha 135.
Kama tulivyoeleza kuhusu kifungu cha 135 tuliweke kwa makusudi ili shitaka lieleweke.
Hiyo person or group of person they are coming from public, yasije onekana ni maneno ya Katuga. Ni kifungu cha 5 cha Penal Code ambacho kinasema maana ya Public kinasema hivi.
Part 483 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 29, 2026
Last time tuliishia part 480 so leo tunaendelea na -;
Part 481
Imepigwa high coooooourt
Majaji wameingia.
Mheshimiwa Lissu ameingia na kupokelewa na makofi mengi sana kawa kawaida yake.
Jaji anamuita karani.
Karani anasoma kesi namba Criminal session No. 19605/2025.
Anasimama Nassoro Katuga na kutambulisha kwa upande wa Mawakili wa Serikali na anasema wako tayari kwa upande wao kufanya mawasilisho ya mwisho.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa vipi?
Mhe. Tundu Lissu na yeye anasema yuko tayari.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
Jaji Upande wa Mashitaka tuendelee.
Anasimama Katuga anasema tunaomba kutoa ahadi kwamba kwa upande wa Jamhuri hatutakuwa na Majumuisho marefu kabisa, na tunaomba kuanza kama ifuatavyo:
Jaji wewe nani?
Nitakayeanza naitwa Katuga.
Katuga Mshitakiwa ameshitakiwa na uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(b) Cap. 16 R.E 2022.
Ambapo Kuhusiana na taarifa ya Mashitaka hii inaelezwa mnamo tar. 03/04/2025 ndani ya Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam alitengeneza nia ya kuchochea umma kuweza kuzuia Uchaguzi wa mwaka 2025 kwa nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alidhihirisha nia yake hiyo kwa kutoa na kusambaza maneno yafuatayo.
Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli kwasababu tunasema tutahamasisha uasi. Hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko kwahiyo tunakwenda kukinukisha sanasana huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwasababu tunaenda kukinukisha.
Haya maneno ndio upande wa Jamhuri tuliyaleta kwenu kuyaangalia kwamba maneno haya yalilenga kwa nia ya kuitisha Serikali ili ipate mabadiliko anayoyatafsiri ni mabadiliko.
Kifungu cha 39 tulichokitaja tulikifanyia research kuangalia kama Mahakama za Tanzania zimewahi kukitest. Majibu yetu yakawa ni kwamba kesi za Tanzania zilishitakiwa kwa kifungu cha 39(2)(a) na sio kifungu cha 39(2)(d).
Waheshimiwa Majaji naomba kama itawapendeza nimuongeze Job Mrema kwenye orodha ya Mawakili wa Serikali kwani alipata dharula.
Waheshimiwa Majaji kwakuwa tumejiridhisha kuwa haya ni mashitaka mapya kwenye Mahakama zetu basi tunaomba kutafsiri hati ya mashitaka yetu pamoja na Kifungu cha Sheria kwamba ni kitu gani upande wa Jamhuri wanapaswa kuthibitisha.
Waheshimiwa kwa kuanza kabisa naomba kuialika Mahakama hii kwenye kifungu husika cha 39(2)(d) cha Penal Code.
Waheshimiwa Majaji kifungu kinasema any person who being in the allegiance to the URT ..................
Kwamba mtu yeyote mwenye utii awe Tanzania au nje ya Tanzania atengeneze nia either kufanyika au kusababisha kufanyika au atengeneze nia ya kuchochea
Kwa mujibu wa kifungu cha 135 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Cap. 20 R.E 2023.
Waheshimiwa kwa mujibu wa kifungu hicho sheria inasema hati ya shitaka iwe na shitaka aliloshitakiwa na maelezo ya shitaka hilo.
Na kifungu cha 138(a)(iii) cha CPA kinasema technical terms hazitakiwi kutumika. Inatakiwa itumike ordinary language.
NB. Nimeweka vifungu vyote mnaweza kusoma hapo chini.
Tuendelee
Ukisoma kifungu cha 39 kinasema lazima mshitakiwa wa uhaini awe ni raia mwenye utii, sisi mshitakiwa wetu ni mtanzania.
Kwamba akiwa Tanzania au nje ya Tanzania. Sisi wa kwetu alikuwepo Tanzania.
Hati yetu ya mashitaka ikachukua forms an intention to instigate ikaachana na intention zingine, yenyewe ikabaki na nia ya kuchochea.
Ikaachana intetion to effect or cause to be effected kama inavyoonesha kwenye kifungu cha 39. Kwahiyo forms zingine za intention ikaachana nazo.
Part 482 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 480
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Mhe. Lissu anasema Kesi za uhaini sio kesi nyepesi ni kesi ngumu, kunaweza kuwa na presha kubwa na magumu lakini pamoja na ugumu wa kesi hii naona mmefanya kazi nzuri sana, mmetusikiliza, mmenipa nafasi ya kujitetea, hamkunikwaza, mmekuwa wavumilivu sana, mmefanya kazi kubwa, mmefanya kazi nzuri, nilitaka nisimalize bila kusema hayo pengine tusiweze kukutana maana hakuna anayejua kesho
Mawakili wa Serikali nao wamefanya kazi kubwa sana, they had a hopeless kesi, wamepambana, sio mbaya kuwaoa pongezi whichever way you will decide, nawatakieni kila la heri Waheshimiwa Majaji katika tafakari yenu.
Hayo ndio nilitaka yaingie kwenye record waheshimiwa Majaji, msispoyaingiza mtanikwaza,
Watu wamecheka sana😂😂😂😂😂😂
Jaji Ndunguru anasema kesi inaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. Naamini mawakili wa Serikali mtamaliza kesho
Katuga: Sisi tunafocus kwenye kesi naamini tutamaliza kesho sisi hayo maneno ya uzalendo hatuna
Jaji Ndunguru: Shauri litaendelea kesho saa tatu asubuhi kwa upande wa mashtaka kuwasilisha Mawasilisho yao ya mwisho.
Imepigwa High Cooooouuuurrrrtttt
Majaji wanatoka
Watu wamesimama wanapiga makofi mengi sana huku wakiiiimba Mwambaaaa!… Mwambaaaaa!…, Mwambaaaa!….
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 479
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Kesi ya Pili ni ya Mahakama Kuu: Saed Kubenea dhdi ya AG Misc Civil Cause No 28 of 2014 HC at DSM 7th October 2014. Mr. Justice Twaib ukurasa 17-21 Mahakama haiwezi ikaingilia migogoro ya kisiasa.
Ni kweli kwamba maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye kesi ya Mtikila na Kubenea yalihusu kesi za jinai yalihusu kesi za madai, swali langu ni je migogoro hiyo ya kisiasa ikigeuza kuwa ya kijinai, Mahakama itakubali kuingilia kisa tu imepakwa rangi za kijinai?
Mimi naiambia Mahakama isikubali kuingizwa kwenye migogoro ya kisiasa haitatoka salama, msimamo ule ule wa kwamba migogoro ya kisiasa isije Mahakamani iendelee na msimamo huo huo vinginevyo wale ambao wanahusika na kufungua kesi wataonea watu wengi sana kama ambavyo wamekuwa wakionea watu kutokana na ushahidi uliopo kwenye kesi hii.
Waheshimiwa Majaji hoja yangu ya mwisho inahusu aina ya mshtakiwa aliyepo mbele yenu.
Mshtakiwa ambaye kwa ushahidi wa DW2, amemuelezea mshtakiwa kwa maneno yako ukurasa wa 885, alisema amenifahamu kwa miaka 23.
DW3 ambaye amenifahamu kwa miaka 20 alisema kwenye ukurasa wa 760 wa record, the accused person is not capable of committing treason.
DW4 aliysema ananifaham kwa miaka 13, accused ni leader of democracy and human rights defender (ukurasa wa 811 wa record)
DW5 ambaye alisema amenifaham for more than 20 years “ a person of integrity and honest, a courageous leader who is not afraid to speak the truth (ukurasa 817 wa record) hayo maneno sio ya machawa wangu, hao ni Viongozi na mashahidi ambao nimefanya nao kazi, nimepambana nao pamoja kwenye mapambano ya nchi hii kwa miaka mingi.
Waheshimiwa Majaji kuthibitisha maneno yao angalia ushahidi kwenye record: Makamu Mwenyekiti IDU, Mshindi wa Tuzo mbalimbali, Mbunge wa Kuchaguliwa, Rais wa TLS, angelieni kwenye record then mjiulize kama kweli huyu mtu anaweza kutenda kosa la uhaini, pia mjiulize kwanini Jumuiya za Kimataifa zinanipigania, Mabalozi kila asubuhi wanakuja hapa, UN imesema niachiliwe, Je UN inaweza kuunga mkono uhaini?
Mawaziri wa Jumuiya ya madola wamesema niachiliwe ndani ya siku 30.
Hoja yangu ni kwamba ushahidi wa Jamhuri ni kinyume na picha ya huyu mtu anayedaiwa mhaini, I am a patriotic, am not a traitor.
Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo,
“I have fought against white domination and I have fought against blood domination, and My Lords, it is an ideal I am prepared to die for”
Nimepigania haki na Demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya Demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalizia kwa neno moja, Waheshimiwa Majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, Waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should nit hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope.
Kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini msiogope kuniachia huru, you have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn’t fit acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji.
Nimemaliza
Part 480 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 478
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Kwahiyo waheshimiwa Majaji, kesi imefunguliwa bila kufuata sheria because they were in a hurry to get Mwenyekiti for treason.
On this particular point, Mahakama hii iifutilie mbali hii kesi sababu imefunguliwa kinyume cha Sheria.
Hoja nyingine inayoonyesha mashaka na ya msingi kuhusiana na kesi hii inahusu matumizi ya criminal process kupambana na wapinzani wa kisiasa na Serikali, ushahidi wa hili mmeusikia nyie wenyewe kutoka kwa mashahidi watano wa utetezi.
Mfano mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe na wenzake 7 walilipishwa million 350, mashahidi wa utetezi kila mmoja wetu alielezea namna ambavyo tumetengenezewa kesi over years and years, kila shahidi amewaaambieni namna alivyokamatwa, alivyoshtakiwa.
Mimi Lissu niliwaeleza kesi yangu ya kwanza 2002 siku ya Christmas, Wanangu wameniambia Baba Christmas yetu ya kwanza ulikuwa gerezani, nimekuwa prosecuted na Kikwete, Magufuli na sasa Samia.
Ushahidi wa kwenye kesi hii unaonyesha jinsi ambavyo tumeteswa na makesi haya ya kisiasa.
Matumizi ya Criminal kesi dhidi ya Political opponents ni matumizi haramu ya sheria za kijinai, We are a multiparty state, hence we are allowed by the laws if this country to criticize the government in the harshest of terms, we are not obliged to love them, sheria haitukatazi kuwa wapinzani.
Ninaposema Sheria namaanisha Katiba na Penal Code Kifungu cha 55(2) na 63B kinaturuhusu kupinga mifumo yake, sera zake,
Jaji Ndunguru: Umebaki na saa moja
Mhe. Lissu: Nitamaliza
Mhe. Lissu anaendelea anasema hata sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS Act) hata kwenye yale ambayo imeyasema ni matishio kwa usalama wa taifa does not include under section 3: lawful advocacy, protest, dissent, tukifanya harakati za kuiondoa Serikali madarakani lawful maana Maandamano ni halali kwa nchi hii hilo sio tishio kwa usalama wa taifa kwasababu Katiba yetu inaruhusu mfumo wa Vyama vingi, Demokrasia ya vyama vingi.
Huu utamaduni wa DPP na Mapolisi kuendesha vita ya kisheria dhidi ya wapinzani wa CCM ni matumizi mabaya ya madaraka.
Na ofisi ya DPP Katiba hii inasema under 59B(4) DPP anatakiwa kuzingatia, nia ya kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya taratibu za utoaji haki, maslahi ya umma. Kuwafungulia wapinzani wa CCM kesi za jinai ni matumizi mabaya ya mamlaka na ni against maslahi ya umma, hii sio nchi ya CCM it used to be long time ago.
Waheshimiwa Majaji hizi kesi za kisiasa hizi Mahakama zetu zimesemaje?
Nianze na Freeman Mbowe na wenzake 7 (Sura- hii maana yake ambayo nimeshaitaja hapo nyuma).
Mmoja wa wakata rufaa ambaye ni John Heche alisema
“Kesho patachimbika, upumbavu unaofanyika kwenye nchi hii, wizi unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano lazima ukome”
Alikamatwa akashtakiwa na kufungwa na Hakimu mkazi kisutu na kulipa faini 350M, kwenye rufaa Jaji Mgeta alisema yafuatayo ukurasa wa 50 na 55,
“I see nothing in them ….this amounts to taking politics too far… a Democratic government must torelate criticism even in hashste terms…”.
Mimi nimeshtakiwa kwa kusema maneno ambayo ni malalamiko ya kiuchaguzi, this is taking Politics too far, wanataka kuigeuza nchi hii a Police State, Waheshimiwa Majaji waambieni this is taking Politics too far.
Lazima wawe na ngozi ngumu, wawe na uwezo wa kuvumilia mashambulizi ya kisiasa.
Waheshimiwa Majaji, Mahakama imetengeneza a Political doctrine kwamba Mahakama haitaingilia kati migogoro ya kisiasa.
The leading kesi ni AG Vs Rev. Mtikila Civil Appeal no 45 of 2009 full bench of CAT (ukurasa wa 37-41), benchi lote la Mahakama ya Rufani walisema migogoro ya kisiasa itatuliwe kisiasa iwe Bungeni au nje ya siasa.
Migogoro ya kisiasa mahali pake ni uwanja wa siasa.
Part 479 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 477
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
DW4 alisema Mkutano ulichukua masaa matatu hadi matatu na nusu na hotuba ya mshtakiwa ilichukua masaa mawili na nusu ukurasa wa 805.
DW5 amesema mkutano ulichukua masaa manne au zaidi na hotuba ilichukua zaidi ya masaa mawili ukurasa 883.
DW5 aliongeza mkorogo kwenye huo ushahidi kuwa aliona video hiyo hiyo Jambo TV yenye masaa mawili, video hiyo hiyo Chanzo TV yenye dakika 45 na video hiyo hiyo Mwanzo TV yenye dakika 60.
Waheshimiwa Majaji, nani alikuwa na wajibu wa kuthibitisha kuhusu video???
Jibu ni upande wa mashtaka na hawajathibitisha video yoyote.
Waheshimiwa Majaji, just to show how their case is hopeless, hicho kipande kilichopo kwenye hati ya mashtaka kina urefu kiasi gani?
PW3 alisema hayo maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, eti alisema haya maneno kwenye video ni dakika 8 na sekunde 37 ukurasa wa 233 wa record.
DW2 - DW 5 maneno hayo ni between 26 seconds to 2 minutes kwahiyo hayo maneno yanayolalamikiwa yanathibitishwaje katika confusion hii?
Hivyo upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitishwa chochote kuhusu video, maneno ambayo ukifumba macho ndio utakubaliana nao, nawaomba Waheshimiwa majaji msifumbe macho, msikubaliane nao walitakiwa kuthibitisha beyond reasonable doubt.
Video waliyotaka kuileta ilikataliwa Oktoba 23, 2025 lakini kati ya Oktoba last year na now Septemba Upande wa mashtaka haujawahi kuchukua hatua yoyote kwenda kurekebisha ili video iweze kuletwa na afisa anayekubalika kisheria, hawajafanya chochote leo ni miezi 11.
Mara nyingi Katuga ametuambia Mahakama sio ya mama yetu, na yeye sio ya mama yake kwahiyo msimkubalie.
Waheshimiwa majaji, hii kesi imefunguliwa kinyume cha Sheria.
Kifungu cha 4(3) of CPA, kifungu hiki kinasema kwamba pale ambapo jambo linalogombaniwa lina sura ya kimadai au kiutawala au kijinai lazima kwanza zile sura za kimadai au kiutawala zimalizwe kwanza ndo kesi ya jinai ifunguliwe.
🫡 Mhe. Lissu anatoa darasa ambalo nna uhakika hata Majaji kuna mengi wamejifunza kupitia hili darasa.
Haya tuendelee
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji kwenye kesi kama hii ni kipi ambacho kina sura ya kiutawala au kimadai?
Mmeambiwa Mshtakiwa ni Mwenyekiti wa Chadema, chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, masuala ya vyama vya siasa na matendo yao, makosa wakikosea yamekabidhiwa kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Kiongozi wa kisiasa akifanya jambo linalodhaniwa ni kosa lazima kwanza achukuliwe hatua na msajili wa vyama vya siasa, mamlaka yake yapo kwenye kifungu cha 7 cha Sheria hiyo.
Waheshimiwa Majaji ushahidi unasemaje? Mara tu Chadema na Mwenyekiti wake walipoanza kuhamasisha No Reforms, No election nchi nzima msajili wa vyama vya siasa aliiingilia kwa kutumia mamlaka yake niliyoyasema ukurasa wa 677 wa record, msajili aliingilia kati, ni ushahidi wa DW2 John John Mnyika.
Msajili alielezewa na akaelewa na akatoa taarifa kwa umma kuwa ameelewa hapo ilikuwa bado mimi sijakamatwa.
What happened after 3/4/2025? Ukurasa wa 681 DW2 anasema msajili aliandika barua kwa Lissu na niliipokea kwasababu Lissu alikuwa tayari amekamatwa na nilimjibu msajili kuwa Lissu tayari anashtakiwa kwa uhaini kuhusu hotuba yake ya 3/4/2025 kwahiyo ilikuwa inashughulikiwa na mamlaka nyingine.
Huu ushahidi wa DW2 haukuhojiwa hata kidogo na jeshi la mawakili wa Serikali meeaning in terms of justice Lumima Katiti case, huwezi ukashughulikia kijinai suala ambalo linaweza kushughulikiwa kimadai, kesi ya Robert Kadaso Mageni Vs Republic Criminal Appeal No 476 of 2026 CAT Songea 18/08/2023 Mr. Justice Ndika at page 2. Mahakama ya rufani ilisema Section 4(3) of the CPA, creates a binding requirement to exhausition of available civil and administrative remedies before criminal process can be invoked.
Part 478 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 476
Mahakama imerejea.
Majaji wameingia na Mhe. Lissu yupo.
Upande wa Jamhuri wanasema Quorum yao ipo vile vile kama ilivokuwa asubuhi.
Mhe. Lissu anaendelea kufanya final submission
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nilikuwa nazungunzia muktadha wa maneno yanayolalamikiwa na niliwaelekeza kwenye ushahidi wa DW4 na niliwatajia ukurasa wa 810-811 wanasema kitu kimoja hapa, huo ushahidi haukuhojiwa kabisa katika Cross-examination, maana yake ni kwamba hayo maneno yanayotoa muktadha kwenye huo ukurasa yamekubaliwa na upande wa mashtaka.
Once the context is understood, then haya maneno yanayolalamikiwa kuwa ni ya kihaini yanapoteza kabisa hiyo maana mbaya yaliyopewa na upande wa mashtaka.
Baada ya kutoa hiyo context kinachobaki ni kile ambacho DW2 alikisema, alisema kwenye ukurasa wa 679 kuwa the words complaigned of were political statements intended to mobilize the public to boycott the election, the objective is for the public to see the electrion deeply flawed and unacceptable disrupted and preventing it taking place because it would be an illegitimate election, na haya sio malengo ya kihaini kwa mujibu wa sheria za Tanzania
Waheshimiwa Majaji, tuhuma inasema mshtakiwa alichapisha hayo maneno kwenye Jambo TV, kila shahidi wa Jamhuri alizungumzia video.
Mashahidi wote wa utetezi vilevile wamezungumzia video.
Upande wa mashitaka kwenye preliminary hearing waliahidi kwamba wataleta video kuja kuthibitisha shtaka lao.
Kwenye list of documentary evidence ukurasa wa 135 upande wa mashtaka kwenye item 8 na 9 waliahidi kuwa wataleta video iliyopo kwenye flash na nyingi iko memory card, Waheshimiwa majaji hizo video ziko wapi? Hawajaleta video yoyote kati ya walizoahidi.
Waheshimiwa Majaji, He who alleges must prove, wameimba video, video lakini hawajaonyesha hata moja Mahakamani, watasema hivi lakini hawa watu wamekubali kuwa walisema hayo maneno, hata kama hatujaleta video hakuna ubishi kuwa maneno yalisemwa, hiyo hoja wakija nayo haina maana yoyote.
Kwasababu hakukuwa na makubaliano kwamba suala la video halina ubishi kwenye preliminary hearing hivyo kulikuwa na disagreement hivyo walipaswa kuleta video.
Sababu ya pili ni kwamba, pamoja na mshtakiwa na mashahidi wake kusema yale maneno yanayolalamikiwa aliyasema, ushahidi wetu ni kwamba hayo maneno hayana shida yoyote, hayathibitishi kosa lolote linalojulikana na Sheria za Tanzania. Ushahidi wa hayo maneno umekuwa contested throughout.
Sababu kubwa nyingine nawaalika msikubali kabisa Oral testimony isiyokuwa na video ni kwamba hakuna makubaliano miongoni mwa mashahidi juu ya hiyo video kama ninavyothibitisha hapa kwa mfano PW1 alisema hiyo video ina takribani urefu wa masaa 3 ukurasa wa 146 wa record.
PW2 anasema alianza kuangalia video kuanzaa saa 6:00 hadi saa nne asubuhi hivyo ni masaa 4 ukurasa 180, 184 na 206 wa records, PW3 anasema video ina urefu wa massa 3 na dakika 38 ukurasa wa 232 na shahidi huyohuyo anasema hiyo video ina masaa 3 na dakika 45 ukurasa wa 275.
PW16 anasema hiyo video ilikuwa ndefu na waliiangalia kwa takribani masaa mawili na dakika kadhaa ukurasa wa 443.
PW17 aliyerekodi na kuirusha na kuisambaza anasema video yake ina urefu wa takriban masaa matatu, maelezo hayo yapo ukurasa wa 491, 492.
Waheshimiwa majaji ni video ipi ya kwenda nayo? Hizi ni version 6 za upande wa mashtaka, sasa mtaenda na version ipi na hamjaona hata moja???
Kama hizo versions hazitoshi tuangalie za defense
DW1 yaani mimi Tundu Lissu, nilisema sijaona video ila nilizungumza kati ya masaa matatu hadi matano ukurasa 590 wa record.
DW2 alisema video ina urefu wa takribani masaa mawili au marefu kidogo ukurasa wa 663 wa record.
DW3 alisema video ina urefu wa lisaa na nusu hadi masaa mawili ukurasa 750.
Part 477 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 475
Mhe. Lissu anaendelea anasema Waheshimiwa Majaji, facts are very sturbon things (ukweli ni mbishi sana, ukweli huwa unakaa kufichwa and truth is concrete, ukweli ni mgumu kama jiwe.
Hicho ambacho kimefichwa kwenye hati ya mashtaka, yale ambayo hayapo kwasababu ya ellipses yameletwa kwenye ushahidi, huo ushahidi unaiwezesha mahakama kupata kile ambacho hati ya mashtaka ilitaka kukificha.
Ukweli wa kwanza ambao umeletwa na ushahidi ni kwamba hii kesi ni mgogoro wa kisiasa na wa kikatiba kuhusu chaguzi za Tanzania.
Mgogoro ambao umepiganiwa kwa miaka zaidi ya 30, ni mgogoro kuhusu chaguzi za nchi hii sasa umehamishiwa Mahakamani na kuvalishwa mavazi ya uhaini. Waheshimiwa majaji mmeletewa muamue ugonvi wa kisiasa kati ya Chadema na viongozi wake na CCM na Serikali yake.
Waheshimiwa majaji kwenye preliminary hearing iliyoko ukurasa wa 131-132 wa record upande wa mashtaka ulileta maelezo yanayoonyesha kwamba mgogoro huu ni wa uchaguzi, hata hati ya mashtaka yenyewe, hayo maneno yenyewe yanahusu uchaguzi, nia kwenye hati ya mashtaka ni kuchochea watu ili wazuie uchaguzi
Ukiacha hayo, maelezo yote ya maandishi, vielelezo vyote D1 hadi D16 vyote vinaonyesha ni mgogoro wa uchaguzi. Documentary records zote zinathibitisha kuwa huu ni mgogoro wa uchaguzi.
Ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa mashtaka na mashahidi 5 wa utetezi unaonyesha ni mgogoro wa kisiasa kuhusu uchaguzi.
Waheshimiwa Majaji huo muktadha ni muhimu sana kueelewa kuwa ni mgogoro wa kisiasa wa uchaguzi unaokuwa litigated in a criminal court.
Kwa miaka zaidi ya 30 from 1993 mtikila one mgogoro huu ulikuwa unapiganiwa katika mahakama za civil na majukwaa ya hadhara, vyombo vya habari na majukwaa ya sasa kama Bunge. Sasa Mawakili wa Serikali na Mapolisi wao wameuvalisha huu mgogoro mavazi ya kijinai.
Waheshimiwa majaji katika ushahidi wa pande zote mbili, ushahdii wa utetezi wa mashahidi wake wote ndio umetoa muktadha sahihi wa kesi hii.
Ushahidi wa utetezi umeonyesha huu mgogoro mrefu wa miaka mingi wa kikatiba na kisiasa kuhusu uchaguzi katika nchi yetu ambao umetufikisha hadi kwenye mgogoro wa uchaguzi wa mwaka jana.
Mashahidi wote wa upande wa utetezi wameelezea kwa kirefu hayo maneno yakiyopo kwenye hati ya mashtaka kama no reforms no election, ni kitu gani, imetokana na nini, wameelezea extensively.
Mashahidi wa upande wa utetezi in this particular case DW4 ameelezea mahakama kuwa hayo maneno wanasema “mshtakiwa aliposema wanasema kitu kimoja sahihi hapa” kwenye ukurasa wa 810-811 amesema Mwenyekiti alikuwa anawajibu G-55 waliokuwa wameandika mtandaoni, tumeipata hii kwa DW4 na hatukuipata kwa wale wenye wajibu wa kuthibitisha mashtaka yao
Waheshimiwa majaji upande wa mashtaka hawakusema chochote kuhusu juu ya maneno kama kukinukisha, maana tumeipata kutoka ushahidi wa utetezi.
Upande wa mashtaka kwa jinsi walivyoandika draft ya mashtaka na kunyofoa nyofoa hayo maneno walitaka kuonyesha kuna kosa kubwa sana lakini ushahidi wa utetezi umeonyesha hakuna kosa lolote lililofanyika, sio kukinukisha, sio kuvuruga uchaguzi, sio kuhamasisha uasi, hakuna kosa hilo
Ushahidi wa utetezi umetusaidia kuonyesha the missing context, upande wa mashtaka hawakutaka kutuonyesha hiyo context ila tumejua kwasababu ya utetezi.
Ukiangalia hayo maneno yanayolalamikiwa utafikiri kwamba huo mkutano wa 3/4/2025 ulikuwa na maneno hayo tu, kwamba mshtakiwa aliongea hayo maneno ya nusu dakika then washiriki wakaondoka.
Waheshimiwa majaji naomba mtafakari yafuatayo yaliyoko kwenye ushahidi. PW1
Jaji Ndunguru anasema kwanini tusibreak kwanza baadae ndio uje useme after break
Mhe. Lissu: Ni sawa waheshimiwa majaji, leo tutamaliza sitaki kesho kurudi hapa
Jaji Ndunguru: Ni wewe tu , kwa sauti ya upole huku akicheka
Watu kicheko sana.😂
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa tambua kuwa tukirudi tuna masaa mawili na nusu tu
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, I intend kumaliza leo
Jaji Ndunguru: Mahakama inahairishwa hadi saa nane na nusu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 474
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Kati ya hizi shahidi mbili za hawa wakwangu na za hawa wa Mapolisi au ziamini mashahidi wangu? Ushahidi wa watu waongo kama Mapolisi.
Rai yangu on the basis of Goodluck Kyando ushahidi na mashahidi wote wa Upande wa Mashitaka hawastahili kuaminiwa hata kidogo kwa sababu nilizozisema kwa kirefu sana kwasababu nzuri na za maana nilizoonesha kwenye ushahidi huu. Hawastahili kuaminiwa hata kidogo. Kati ya mashahidi wote 17 wa Jamhuri namuondoa shahidi PW 17 ambae ushahidi wake naona ni wa ukweli.
Ushahidi wa mashahidi wote wa Utetezi unastahili kuaminiwa na kukubaliwa kwasababu ambazo nimezizungumzia pia kwa kirefu.
Waheshimiwa Majaji kwa kusema hayo sina maana na naomba isichukuliwe kuwa ushahidi wote wa Utetezi haukuwa na mawaaaa. Sina maana hiyo. This is not to suggest that the defence evidence was in every sport sportless and free from blameshes.
Hakuna ushahidi ambao utatolewa kwenye Mahakama ambao hauna shida kwa asilimia 100 kupitia binadamu wa namna hii. Na ushahidi wa mashahidi wote wa upande wa utetezi ni ushahidi wa Binadamu.
Hata hivyo mashahidi wote wa utetezi tuliburuzwa sana kwenye cross Examination were able to show descrepancies. Lakini kitu muhimu ni ushahidi wao kwenye maswala muhimu yanayotengeneza hii kesi ushahidi wao ulikuwaje? On all fundamental issues ushahidi wao ulikuwaje?
Mambk ya Jezi ya Arsenal, Umelala Dubai hayo yote yalikuwa hayaibui wala kujibu jambo la msingi kwenye mambo ya msingi kuhusu kesi.
Nguza Vikings alias Babu Seya ilisemaje kuhusu contradictions or descrepancies za Upande wa Utetezi. Ilisema yafuatayo at page 25 a conviction in criminal cases is not based on contradiction of the defence evidence rather on the evidence adduced by the prosecution witnesses. Burden of proof lies on the prosecution side and not on the defence and the standard is beyond reasonable doubt. Discrepancies from the defence may assist the court to determine the prosecution has proved the case beyond reasonable doubt.
Nimemaliza kuzungumzia ushahidi na ushahidi niliouzungumzia unaonesha hakuna ushahidi wa kumtia mshitakiwa hatiani katika kesi hii. Badala yake kuna ushahidi wa kutosha wa kumuachia Mtuhumiwa.
Waheshimiwa Majaji naomba nizungumzie eneo lingine linaloleta mashaka makubwa kwenye kesi hii. Maeneo yanayocreate reasonable doubt.
Eneo lingine linaloleta mashaka makubwa na ya msingi ni jinsi ambavyo upande wa mashitaka umejaribu kuficha mambo muhimu kuhusu hiyo hotuba ya Tarehe 03/04/2025.
Kuna kila sababu ya kuonesha kesi imetengenezwa kwa kuficha na kuondoa maneno mengi ambayo yangekuwa ingeonesha hakukuwa na kesi yoyote. Umefanya kazi ya Cherry picking yaani maneno wasiyoyataka na kuyaondoa ili kuleta maana tofauti wasiyohitaji.
Naomba kwa ridhaa yenu niwarudishe kwenye hati ya mashitaka kwenye hayo maneno wanayoyalalamikia ukiyaangalia hayo maneno kwa makini una realize immediately kuna mambo mengi yameondolewa.
Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi.... anasoma hadi mwisho.
Hayo ndio maneno mtu asiyekuwa makini hataelewa
Kabla ya neno la kwanza kuna dot dot ziko tatu. Elpsis ziko hapo na maana yake kulikuwa na maneno kabla ya wanasema. Maneno ya kabla hapo wameyaondoa.
Inaendelea hapo anasoma msimamo huu unaashiria uasi ni kweli, ni kweli kwasababu .. kuna neno mabadiliko halafu elpsis sasa hapo napo kuna maneno yameondolewa. Kwahiyo kwenye baada ya mabadiliko pia nako yameondolewa. Je ni maneno gani na kwanini yaondolewe.
Kwahiyo tutaenda kukinukisha sanasana sasa kati ya kukinukisha na sanasana kuna elpsis na maneno yameondolewa. Hayo nayo ni maneno gani?
Tutaenda kukinukisha sanasana hapo napo kuna elpsis kwa maana ya maneno yameondolewa. Je yalikuwa na maana gani hayo maneno na kwanini hawajayaweka na hakuna ushahidi wowote kuhusu kwanini wametoa maneno hayo?
Part 476 itaendelea kwenye post inayofuata.
Repost.