3/3 Ikumbukwe kuwa Duniani Kwa Ujumla Nchi zinazotoa Adhabu ya Kifo kwa Wala Rushwa ni China, Vietnam, Iran , Korea ya Kaskazini, Thailand na Indonesia japo Kwa Thailand na Indonesia utekelezaji wake umekuwa wa nadra sana ukilinganisha na Nchi hizo nyingine tajwa hapo juu.
#SheriaAfrica🌍
Niger imepitisha Sheria mpya inayotoa Adhabu ya Kifungo cha Maisha au Kifo kwa Wala rushwa.
Chini ya sheria hiyo, Mtu yeyote atakaetiwa hatiani kwa kufuja fedha za umma kiasi dola 350,000/TZS milioni 900 au zaidi, anaweza kuhukumiwa Kifungo cha Maisha Jela➡️➡️
2/3 Sheria hiyo inaendelea kutamka kwamba wale watakaofuja au kufanya ubadhirifu wa zaidi ya takriban dola milioni 1.7/TZS Bilioni 4.4 wanaweza kukabiliwa na adhabu ya Kifo. Kwa Africa ni Niger na Burkina Faso pekee zimeweka Adhabu ya Kifo ili Kukabiliana na Rushwa. ➡️➡️
#SheriaThoughts⚖️🇹🇿
Kwa Mujibu wa Maamuzi katika kesi ya Bahati Boniphace Kazuzu V. Ruth Alex Bura (HC, DSM, 2021), Mahakama Kuu iliamua kwamba Mali/Zawadi yoyote anayopewa mwanandoa kutoka kwa Mchepuko wake itahesabiwa kuwa ni Mali ya Wanandoa Wote (Matrimonial Property).
#SheriaThoughts⚖️🇹🇿
Kuelekea Weekend muhimu kuwakumbusha Wadau wa Vileo/Pombe. Tambueni kuwa Sheria ya Vileo [CAP 77] inafanya Kuwa Kosa kwa Mfanya biashara Yoyote wa Vileo/Pombe Kumuuzia Mtu Kileo/Pombe wakati tayari amekwishalewa. ADHABU: KIFUNGO JELA MWAKA 1 AU FAINI AU VYOTE.
#SheriaThoughts⚖️🇹🇿
Kisheria Mume na Mke wana uwezo wa Kuibiana. Pale Mke/mume Anapochukua kitu cha Mwenza wake (mfano fedha wakati wa kufua nguo/au mume kuchomoa noti kwenye mkoba wa mkewe) bila idhini yake atahesabika kuwa mwizi kama wezi Wengine. ADHABU: KIFUNGO JELA MIAKA 7.
#GeoPolitics🌍
Hatimae Makubaliano ya Awali Yamefikiwa Kati ya Marekani na Iran kuhusu Usitishwaji Rasmi wa Vita na Kuweka Mkakati wa siku 60 wa Kumaliza Masuala Mengine yaliyobaki.DIPLOMASIA IMECHUKUA NAFASI, DUNIA IMESHUSHA PUMZI..!!
2/2 Pia Mke anaweza kutumia pesa za mume wake zozote zilizo mikononi mwake au kubadilisha mali ya Mume inayohamishika kuwa pesa na Kutumia hizo pesa kwa Mahitaji Muhimu kwa ajili yake na watoto wa ndoa hiyo yanayolingana na uwezo na Mtindo wa Maisha wa Mume. Kifungu cha 64, LMA.
#SheriaThoughts⚖️🇹🇿
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa ya 1971,wajibu wa kutoa kutunza familia ni wa Mwanaume na ikiwa mume Anakimbia wajibu huo basi Mke anaweza kukopa ili kukidhi Mahitaji yake binafsi ya msingi na ya familia kwa Jina la Mume wake na Mume atawajibika Kulipa Mkopo huo.
#SheriaThoughts⚖️🇹🇿
NI KOSA kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kwa Mfanyakazi kutumia muda wa kazi kufanya mambo binafsi (kuchat au kuongea ongea na simu),kusinzia/kulala ofisini. ADHABU NI KIFUNGO JELA MIEZI MITATU AU FAINI AU VYOTE.
2/2 IKumbukwe Wahouth wa Yemen ni moja kati ya ushirika wa ncha ya Upinzani (axis of resistance) hasa dhidi ya Israel na Marekani ambao kiongozi wake ni Iran ambaye Wamarekani na Israel humuita kama kichwa cha pweza huku mikia yake ikiwa ni Hezbollah, Hamas, Wahouth n.k.
#GeoPolitics🌍
WAHOUTH WATISHIA MELI ZA ISRAEL ENEO LA BAHARI NYEKUNDU: Hali ya mashaka inaendelea baada ya Wahouth kutangaza kushambulia meli zozote zinazohusiana na Israel na kwamba tayari wameshaishambulia Israel ikiwa ni hatua ya kuiunga Mkono Lebanon.
#GeoPolitics🌍
ISRAEL YAJIBU MASHAMBULIZI NDANI YA IRAN: Mapema alfajiri kwa Saa za Iran, Jeshi la Anga la Israel limeripotiwa kufanya mashambulizi kujibu mapigo katika maeneo Mbalimbali ya Iran ikiwemo Tehran,Isfahan, Tabriz na Karaj. Milipuko kadhaa ilisikika katika miji hiyo.
3/3 Iran pia wametishia Kushambulia kambi za Marekani ikiwa watashambuliwa. Dalili zinaonyesha kuwa Israel wanaweza kujibu kwa kiasi fulani na Trump anapaswa kumzuia Netanyahu na Netanyahu ana shauku ya kuendelea na vita.Iran nao wanaonyesha kuwa tayari.MUDA UTAONGEA VYEMA ZAIDI.
#GeoPolitics🌍
IRAN YASHAMBULIA ISRAEL Baada ya Siku zaidi ya 60 za makubaliano ya Kusimama kwa Vita baina ya Marekani, Israel na Iran..Iran imeishambulia Israel kwa makombora ikiwa ni kulipiza kisasi kufuatia Israel kushambulia maeneo ya Kusini mwa Lebanon. CHANGAMOTO MPYA...!!
2/3 Trump amesisitiza na kuiambia Iran kwa kuwa wameshajibu mapigo kwa Kuishambulia Israel basi warejee mezani na wasaini makubaliano ya Amani.Israel pia wanadai wameyadungua makombora yote ya Iran na hakuna madhara.Swali ni Je, Israel watajibu kwa Kuishambulia Iran au watapuuza?
#FikraSheria⚖️🇹🇿
BAADA YA NDOA WANANDOA HAWAPASWI KUDAI TALAKA MPAKA MIAKA MIWILI IPITE KWA MUJIBU WA SHERIA YA NDOA. Namna pekee ni Kuomba Kibali Maalum (court's leave) kutoka Mahakamani na lazima Usibitishe unapitia Mateso Mazito ili Kukubaliwa Vinginevyo Mnatakiwa Kuvumiliana.
#FikraSheria⚖️🇹🇿
Kwa Mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, Mwanaume Pekee ndio anauwezo wa Kufanya Kosa la Ubakaji na hivyo Mwanamke Kisheria hachukuliwi kuwa na uwezo wa Kufanya Kosa la Ubakaji na hivyo hawezi kushitakiwa kwa Kosa Hili. ADHABU YAKE NI MIAKA 30 JELA.
2/2 Kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka (1971) na pia Sheria ya Kanuni ya Adhabu CAP 16, Ifahamike mke akikimbia jukumu hili na kumtelekeza mume wake kwa sababu ya ugonjwa au umri hilo ni KOSA LA JINAI NA ANAWEZA KUFUNGWA JELA KIFUNGO KISICHOZIDI MIAKA MITANO AU FAINI AU VYOTE.
#FikraSheria⚖️🇹🇿
Imezoeleka kwamba wajibu wa kutunza familia (mke na watoto) ni wa Mume/Baba.Lakini pia muhimu Kutambua kwamba pale Baba/Mume anapokuwa katika hali duni kiafya au kwa Sababu ya umri basi mke wake anapaswa kuwajibika kumuhudumia katika mahitaji yake yote ya msingi.