BIASHARA YA KUUZA KESI NDIYO BIASHARA MPYA..!
Kuna wakati nikiwa Meya halmashauri ya manispaa ya Kinondoni nilikuwa naona kila ifikapo mwisho wa mwezi naletewa taarifa ya Manispaa kushindwa kesi kutoka kitengo cha sheria.
1.Machale yakanicheza nikaomba kitengo cha sheria kiniandikie taarifa ya kesi zote tulizo shitakiwa na tulizoshitaki na zije kuwasilishwa katika kikao cha kamati ya fedha na uongozi.
2.Nikaandika barua kwenda TAMISEMI,TAKUKURU na MKOANI kuomba wanasheria waziada wa Kupitia majalada ya kesi zote,
4.Nilijibiwa vizuri na kupewa ushirikiano kwa kupewa wanasheria wa kuisaidia halmashauri ya manispaa ya Kinondoni wapatao watano,Wawili kutoka TAMISEMI
3.Baadae timu ya Wanasheria kutoka TAMISEMI, MKOANI,na KATUKURU ikaleta taarifa yake baada ya kupitia kesi zote katika kikao cha kamati ya fedha na uongozi.
4.Matokeo ya ile taarifa yalikuwa ni ya kuhuzunisha sana,baadhi ya kesi zilikuwa zinasikilizwa "experte" upande mmoja bila uwepo wa Wanasheria wa halmashauri ya manispaa ya Kinondoni.
5.Baadhi ya kesi Majaji wa Mahakama ya rufaa,Mahakama kuu na Mahakimu walikuwa wana "doubt" tilia shaka uwezo wa Mawakili wetu wa Halmashauri wawapo mahakamani katika uwasilishaji wa hoja zao.
6.Baadhi ya kesi tulikuwa tunakata rufaa nje ya muda kwa makusudi kumpa mdai wetu unafuu au ushindi kwa makusudi.
7.Nikathibitisha mali na pesa za serikali ni kama shamba la bibi,hakunaga mwenye uchungu nazo wajanja wachache walikuwa wanajipatia pesa nyingi kupitia fidia za kushindwa kesi.
8.Baadhi ya kesi maarufu zilizo uzwa kizembe sababu ya Kukosa uwakilishi Mahakamani na Kushindwa kwa uzembe ni
1.kesi ya Uwekezaji wa Jengo la Makazi ya zaidi ya familia moja ya biashara (Oysterbay Villa apartments).
2.Manispaa ya Kinondoni Vs Q consult (Manji).
3.Mkataba wa Jengo la uwekezaji la biashara stendi ya Makumbusho.
9.Baadhi ya kesi nililazimika kuunganisha nguvu mimi na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni wakati ule Ally Hapi kwenda wenyewe kukataia rufaa kwa Masajili wa Mahakama yarufaa
( hapo napo kuna Jambo zito sana nililiona nitazungumza siku nyingine).
10.Namna ya Kudhibiti upigaji au biashara ya kuuza kesi zipo mbili
1.Kuzuia Watu wachache kufanya maamuzi yatakayosababishia hasara serikali.
(kuzuia kutengeneza mazingira ya kesi)
2.Kesi zinapokuwa zimefunguliwa,Wanasheria wanaowakilisha kesi kuundiwa timu mchanganyiko kutoka idara mbalimbali za serikali
(kuzuia wanaosababisha kesi kuendesha kesi)
MAAJABU KATIKA HIZI KESI ZA SERIKALI TUNAZOSHINDWA
1.Tangu nianze kusikia serikali kushindwa kesi za kimataifa hatujawahi kusikia Waliosababisha kesi kuchukuliwa hatua.
2.Tangu tusikie mali za serikali (ndege) kukamatwa hatujawahi kuona serikali ikipangua ofisi ya Mwanasheria mkuu kama sehemu ya kuwawajijibisha.
3.Hatujawahi kusikia zabuni ya Mawakili wa Kimataifa na njia wanazopatikana kukodiwa na serikali ktk Mahakama za kimataifa.
4.Timu ya Wanasheria wetu ni ile ile kwa miaka 6,kwa kesi zote hawabadilishwi pamoja na kushindwa kesi kila siku.
inamaa kocha huoni sababu ya kubadili kikosi chako pamoja kufungwa kila siku..?
Hii ni biashara ya watu,na njia mpya ya kupata pesa kirahisi sana.
Kwa bahati mbaya sana Idara ya usalama wa Taifa (TISS) wapo bize sana na siasa tu,kuliko maslahi ya nchi.
Au huenda hawasikilizwi na wamekata tamaa au wamekosa uzalendo au na wao ni sehemu ya mfumo ulio oza wa kupiga dili na kujali maslahi yao binafsi.
Boniface Jacob
Ex mayor Kinondoni & Ubungo.
Mtikila Mtikila Mtikila.......!
Nakuagiza wewe na Vikosi vyako kuangaza maeneo yaote ya Pwani ya bahari ya hindi juu na Chini wakati natua ENEO LA VITA..
Elekeza askari wako wasitawanyike wakati mimi na Vikosi vyangu tumerudi Kuongeza nguvu.
Operesheni hii itaisha January mosi OVER.
Labda hapo katikati mambo yaharibike sana😂😂😂
‼️🚨Hanang #Tanzania 🚨
kazi bado kubwa ya uokoaji
Kuna nyumba Katesh karibu na soko zimezingirwa na matope na watu wanashindwa kutoka tokea siku ya tukio wameomba tupaze sauti!
Gendabi mvua iliyonyesha imeharibu mfumo wa maji - hawana maji!
Huduma inayotolewa bado haitoshi!
Wapendwa habari! Msaada, kwa yeyote anayemfahamu Dr Makia, alikuwa Daktari Muhimbili. Mama huyu alininusuru na kifo kwa kusimamia upasuaji wangu mwaka 2009. Nilipoteza mawasiliano naye, nafsi yangu haitulii, ninahitaji kumpata japo nimshukuru. Kwa anayemfahamu DM please👏
Nimewasilisha malalamiko yangu dhidi ya Mh.Gekul kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Maadili ya viongozi wa Umma Sura. No.398( R.E 2020) kifungu cha 25(1) kinachotoa fursa kwa mtu yeyote kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya kiongozi wa Umma juu ya uvunjifu wa sheria ya Maadili.
Biswalo anapewa UJAJI. Feleshi anapewa AG. Kilangi anapewa UBALOZI. Juma Anaendelea UJAJI Mkuu kwa Mkataba.
Hawa watu walikuwa kwenye FOREFRONT ya kusupport udikteta wa Magufuli na wanaendelea kula KODI.
Mpoki anachukuliwa HAKI ya kufanya kazi yake BINAFSI!
It’s disgraceful.
Ni muhimu kukumbuka kwamba: @MpaleMpoki ni:
1. Wakili kiongozi kwenye kesi ya Loliondo.
2. Wakili kiongozi kwenye kesi ya Bandari.
3. Wakili kiongozi kwenye kesi ya @Mwabuk2Boniface
4. Alikuwa wakili kiongozi kwenye kesi ya kupita bila kupingwa.
@MariaSTsehai@lifeofmshaba
Mnatengeneza precedent mbaya sana. Jambazi au mwizi anaweza kuuwawa akiwa kwenye tukio la uhalifu kama hakuna uwezekano wa kumdhibiti.
Mhalifu akidhibitiwa na raia na kufikishwa katika mikono ya polisi hatutakiwi kusikia amefariki kwa mateso au kipigo cha polisi. Haitakiwi kabisa.
Polisi inapaswa kuwa sehemu salama hata kwa mtuhumiwa wa uhalifu kukimbilia akiamini kwamba atakuwa salama hadi mahakama imtie hatiani.
Kwamba hatuamini sheria zetu za makosa ya jinai? Sheria zimeeleza vizuri makosa yote ya jinai, hukumu na adhabu zake. Tuzifuate na kuzitumia hizo sheria.
Kama hatuamini katika hizo sheria kwamba zinatoa adhabu ndogo kwa wahalifu, tunaweza kuwatumia hawa wabunge waliopo, kuweka adhabu kali zaidi.
Umemsikiliza mkuu wa mkoa wa DSM leo? Ile ni kauli mbaya sana, kauli ile ikitumiwa na polisi DSM, niamini mimi, ndugu yako atauwawa na utalia sana.
MMM simtetei jambazi au mwizi yeyote, lakini nafahamu athari za kuruhusu polisi kuwapiga watu risasi na kuwauwa kwa sababu zozote za uhalifu.
Kuna vijana wengi sana Mburahati, Mabibo, Manzese wameuwawa kwa kupigwa solar-tape mdomoni na puani tena wakiwa katika mikono ya polisi.
Malalamiko hayo ninayo mengi sana. Wazazi wao wanapigiwa simu baada ya watoto wao kukamatwa, wakachukue maiti zao mochwari. Tusiende huko.
Sirari, Tarime, April 2018, Chacha Suguta alikamatwa na polisi akiwa Bar. Akiwa ndani ya gari la polisi wakizunguka naye, alichomwa kisu akafariki.
Chacha Suguta alikamatwa BAR usiku, askari wakaondoka nae, akiwa mzima. Asubuhi anakutwa Mortuary ya hospitali ya wilaya ya Tarime.
Mwili wa Chacha Suguta ukiwa MAITI una majeraha ya visu. Mwili ukafanyiwa postmortem mbele ya ndugu zake, daktari akathibisha jeraha la kisu
Unajiuliza, Chacha Suguta akiwa amefungwa pingu, ndani ya gari la polisi au hata kituo cha polisi, kwanini mwili wake ukutwe na jeraha la kisu?
MMM au BoniYai au Mbowe hawawezi kuuwawa kwa namna hiyo, umma utapiga kelele. Lakini ndugu zenu huko mtaani watafanywa hivyo na mtalia sana
Polisi watawaua ndugu zenu kwa kusema ni wahalifu tena wakiwa wamekamatwa wazima na tutakuwa tunatengeneza dola hatari la kipolisi. Msishangilie.
Tusiruhusu polisi kujichukulia sheria mkononi. Polisi wakifika hatua hiyo, watarasimisha utaratibu wa kuwatoa wahalifu mahabusu kwenda kuwaua.
Katika jamii zetu tumeweka utaratibu wa ulinzi shirikishi, kuna hadi askari kata, tuweke utaratibu mzuri kuwataja wahalifu katika mikutano ya umma
Tuhudhuria mikutano ya vitongoji, vijiji, mtaa, kata. Tushirikiane kuwataja wahalifu, wakamatwe, wafikishwe polisi, washtakiwe mahakama.
Kamwe, chonde-chonde, tusikubali na tusiruhusu nchi yetu kuwa dola la polisi kwamba wanaweza kumuua mtuhumiwa wakiwa naye mkononi.
Unaweza kushangilia hao wengine kuuwawa katika mikono ya polisi kwa sababu siyo ndugu zako, lakini siku wakimuua mtoto wako au baba yako UTASEMA.
Wapo wengi wanakamatwa na wanalazimisha kukiri tuhuma kwa mateso makali. Mtuhumiwa, anawafia mikononi, wanampeleka mochwari.
Unaweza usinielewe kirahisi. Sitetei wahalifu au wezi au majambazi. Hapana. Nasema tusiruhusu polisi kuwaua wahalifu wakiwa wamedhibitiwa tayari.
MMM, Martin Maranja Masese
Siku ya tarehe 13 Dec 19, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu raia wa China, Liang Hu kulipa FIDIA ya TZS 50 milioni kwa kosa la kuua tembo 511 wenye thamani ya TZS 7 billioni. Mahakama ilimtoza mtuhumiwa FAINI ya TZS 300,000 au kifungo cha MIEZI 5 jela. Hii ni baada ya mtuhumiwa KUKIRI kosa kwa DPP (Plea Bargaining).
Mahakama hiyo hiyo, ikamhukumu MTANZANIA aitwaye Haika Mgao (26) kifungo cha MIAKA 60 jela kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na kiboko yenye thamani ya TZS 69.5 million.
TAKUKURU, mnatakiwa kufanya UCHUNGUZI katika mazingira kama haya. DPP & Hakimu wote wachunguzwe kwa sababu mahakama imepewa mamlaka ya KUKATAA 'PleaBargain' ambayo ina WALAKINI (magumashi)! Lakini Hakimu hakufanya hivyo.
Inakuwaje DPP anaingia "Plea Bargaining" kwenye mali ya Umma yenye thamani ya TZS 7B! Halafu anatumia nguvu zote kumfunga mtz kwa mali ya TZS 69 M? Ina maana DPP hakuwa na ushahidi wa kutosha kwa mchina lakini akawa na ushahidi wa kutosha kwa mtanzania?
Haya mambo ili yaishi ni lazima tuyazungumze.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe: Tundu Lissu (@TunduALissu ) leo ametembelea Nairobi Hospital kuwasalimia Madakatari na Wauguzi walishiriki kumtibu baada ya kushambuliwa kwa bundiki na risasi kumpata sehemu mbalimbali za mwili September 2017. Mungu awabariki sana hawa wataalamu.
BARUA YA WAZI KWA MHE. RAIS @SuluhuSamia
Mhe. Rais, naamini una uzima wa kutosha asubuhi ya leo. Ukiiangalia video hii kwa haraka haraka utawaona “wahuni” na “watu wasiokuwa na maadili” wakifanya biashara ya “ukahaba.” Lakini ukiangalia kwa umakini, hautowaona wahuni, utaona kundi kubwa la watanzania maskini wanaoishi maisha ya tabu na mateso. Ukiangalia kwa umakini zaidi, utawaona wapiga kura wako ambao umaskini umewalazimisha leo waonekane kama wadhambi kuliko watanzania wote.
Mhe. Rais, kinachofanywa na Mkuu wa Mkoa hapa wala sio kukamata “makahaba” na “kufungia madanguro,” kinachofanyika ni kumdhalilisha maskini kwa sababu ya umaskini wake. Nasema hivi kwa sababu wenzao wanaofanyia “ukahaba” kwenye guest houses za elfu thelathini kule Sinza kuhudumia wateja wa tabaka la kati au wale wanaofanyia kwenye mahoteli yaliyopo ufukweni wakihudumia wateja wa tabaka la wenye nacho, wao hawabughudhiwi. Kwa hiyo hawa kwenye video wanaadhibiwa kwa sababu umaskini wao unaonekana wazi na unawakera viongozi.
Mhe. Rais, usinielewe vibaya. Sipingi kinachofanywa na Mhe. Mkuu wa Mkoa, ila najiuliza, kwa nini viongozi mnakerwa na muonekano wa maisha ya watu wenu lakini hamkerwi na mambo yanayosababisha hawa watu waishi maisha haya? Kwa mujibu wa taasisi ya UNAIDS, Tanzania kuna zaidi ya wanawake 150,000 wanaojihusisha na biashara ya ukahaba. Wametoka wapi wote hawa? Wala usiumize kichwa sana Mhe. Rais, nitakukumbusha. Hawa ndio wale vijana waliomaliza kidato cha nne wakarudi nyumbani bila maarifa yoyote yenye tija. Ndio wale ambao NECTA wanasemaga “asilimia 75% wamepata Division Four na Zero.” Wengine ndio wale waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira na elimu waliyopewa haijawaandaa kujiajiri, waende wapi? Walio pambana sana ndio wale wamekuwa waendesha bodaboda na wengine mama ntilie, hizo ndio zimekuwa kazi za ndoto zao.
Mhe. Rais, kama hawa wangeweza kupewa mafunzo mbadala, kukuzwa na kuendeleza vipaji vyao, na kukopeshwa mitaji, labda leo wasingekuwa wanatweza utu wao kwa kiwango hiki. Hata hivyo zile fedha za kufanyia haya ndio serikali yako imeamua iwanunulie viongozi magari ya kifahari; iwaongezee wabunge mishahara kimono; na hivi karibuni itawagawia wake wa viongozi ambao tayari wanaogelea kwenye utajiri. Fedha nyingine ndio zile zimepigwa kwa mabilioni kwenye report ya kamati ya kudumu ya bunge hesabu za serikali (PAC). Hizi ndio fedha zinazotumika kutengeneza wale vijana mashuhuri unaowaona kule Israel, Singapore, China, Finland, etc. Hawana uchawi wowote Mhe. Rais, wameamua kujali tu.
Nihitimishe Mhe. Rais, hawa maskini ambao leo wanasambazwa kwenye media kama object of mockery kwa taifa hawakuchagua kufanya haya. Nikuone basi, tunapoenda kuwanyanyasa kwa umaskini wao, basi angalau hata tuwatunzie utu wao kwa kuficha sura zao. Kuwapa adhabu ya public shame juu ya mzigo wa umaskini wanaoubeba ni sawa na kuwaua angali bado wapo hai. Na la mwisho, Mhe. Rais, ikikupendeza, basi mwambie mkuu wa Mkoa anapowaambia waondoke na waache kufanya wanachokifanya, basi awaambie pia waende wapi na wakafanye nini kama mbadala wa hiki.
Nakushuru sana kwa muda wako.
Wako
Onesmo Mushi
Mama amefungwa miaka 22 Kwa kukutwa na nyama ya swala, aliyeua tembo anahukumiwa miezi 5 na faini ya 300K ! Tembo mmoja ni sawa na Swala wangapi ? Sheria zetu zinabagua ?
Mzee Christopher Ole-Sendeka anapotumia mbinu za wanasiasa uchwara.
Na Mwl, John Pambalu
Katika kipindi cha hivi karibuni wiki iliyopita taifa limekumbwa na ufisadi wa kutisha. Ma-Trillion ya shilingi yamechotwa na kuibwa na mafisadi ambao kwa kadiri ya hali ilivyo inajidhihirisha kuwa serikalini ya Mhe. Rais Samia iko ICU katika uwezo wa kuyakabili majizi ya mali za nchi, kwani ripoti ya CAG imeendelea kudhihirisha kuwa nchi inapepetea kama karanga.
Katika sakata hilo mnamo siku ya tarehe 04.11.2021 Bunge lilipitia ripoti ya CAG na mbunge Ole-Sendeka akijifanya mwenye uchungu kupitiliza alisema ifikapo juma tatu ya tarehe 6.11.2023 basi angewataja wezi na mafisadi wote, tena akionyesha kuwa angeanza na wake wa IPTL. Leo ni jumatano ya tarehe 08.11.2023 hajataja hata kifaranga cha mafisadi sembuse ma papa???.
ninaomba nimnukuu, “Mimi nigekuwa Waziri miezi sita hii hakuna ambaye angebaki aliyetuhumiwa kwenye wizara yangu, lakini nataka niwaambie wako watu wamefisadi kuanzia IPTL leo wako Serikalini”alisema na kuongeza
“Pamoja na maazimio ya bunge, ni leo tu nanyamaza, kesho kutwa (Jumatatu) katika mjadala mwingine nitataja nani wako nyuma ya IPTL, nani yupo nyuma ya ufisadi wa SGR ambayo manunuzi yametugharimu hasara,”amesema Ole Sendeka.
Amesema kwa ufisadi uliofanyika, pesa zingetolewa, kwenye miradi ya maendeleo Zanzibar ingepata gawio la zaidi ya Sh bilioni 300
Ukimsikiliza between lines utagundua mambo makuu mawili..
Kwanza, anataka uwaziri. Anathibitisha hilo kwa kusema kuwa, "mimi ningekuwa waziri". Kama hiyo haitoshi anatega chambo kwa mteuaji wa mawaziri Mzanzibari Rais Samia.
Anasema, "pesa zingetolewa, kwenye miradi ya maendeleo Zanzibar ingepata gawio la zaidi ya Sh bilioni 300". Unafikiri ameitaja Zanzibar kimakosa. Iko hivi kule Butimba nyumbani kwetu tukitaka kutega samaki unaenda kwenye tope, unafukua utapata minyoo tunaita "chambo". Unakuweka kwenye ndoano kisha unarusha mtoni au ziwani, utaona samaki anakula chambo kwa kuwa anakipenda kumbe kwenye chambo kuna chuma kinaitwa ndoano hapo ndipo mwisho wa ujanja wake.
Olesendeka anatumia chambo (Zanzibar) kumnasa samaki (Rais Samia) kwa kuwa anajua kuwa Rais Samia anaipenda Zanzibar, anaona akiutaja ufisadi na kuunasibisha na Zanzibar anajua ngoma itatiki. Mzee anatumia mbinu kali sana kuliko hawa ma chawa wa kizazi kipya.
Pili. Ole-Sendeka anataja siku ya kuwataja mafisadi, na leo zimepita siku mbili hakuna aliyemtaja. hii inamaana kuu mbili.
Kwanza, Sendeka anatumia mbinu za wanasiasa wasiokuwa waaadilifu ambao wanapiga tochi kuonyesha upande alipojificha muhalifu ili aonyesha anania njema. Halafu gizani anawafuata na kuwaambia msiponipoza nitawataja kweli. Wanasiasa wengi wenye ukosefu wa uadilifu hujipatia fedha nyingi kwa mafisadi kwa kuwafanya mafisadi waamini kuwa wadipochukua hatua ya kumpoza mwenye mdomo wataumbuka. Binafsi sina imani kuwa Sendeka atawataja mafisadi.
Pili, kuna uwezekano kuwa ama anawajua mafisadi ila amehofia usalama wake (ni mwanasiasa muoga) au hana kabisa huo ushahidi ana deshi tu aonekane anawajua. Ni vile tu Tanzania tumefubdishwa kutumia lugha zenye staha hasa kwa wazee wetu lakini ingelikuwa South Afrika Julius Malema angesema hawajui mafisadi huyu, hana ushahidi wowote asingeishia hapo angezema ni Ndanda head tu.
Wanasiasa aina ya Ole-Sendeka hawapaswi kuaminika katika nchi hata kidogo. Wabunge wanapaswa kuwa watu wa kwanza kulisaidia taifa pindi linapofisadiwa. kitendo cha yeye kushindwa kuwataja wezi na ikiwa kweli anawajua alistahili yeye kushtakiwa kwa kusaidia kushamiri kwa ufisadi katika taifa.
Ninamuomba Mungu nikiwa mkubwa nisiwe kama Ole-sendeka maana hana faida kwa lolote katia taifa linalotafunwa na kikundi kidogo cha watu ilihali mamilioni ya watu wakitokomea katika lindi la umasikini wa kupindukia.
Wasalaam
John Pambalu
[email protected]
Mwanza-Tanzania
08.11.2023