BADALA YA KUTUNIA NGUVU KUBWA KUBAMBIKANA MA KESI YA UHAINI NGUVU HII TUNGETUMIA KULINDA RASLIMALI ZA TAIFA.
Ulinzi na usimamizi endelevu wa rasilimali za asili za Tanganyika ni suala la kufa na kupona.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zilizopitishwa na Bunge zinatambua mamlaka ya kudumu ya wananchi juu ya utajiri na rasilimali za asili. Hivyo basi, ni wajibu wa kila chombo cha dola na kila Mtanzania kuhakikisha kuwa rasilimali hizi haziuzwi, hazinyonywi, wala hazisimamiwi kwa njia inayodhuru taifa.
SHERIA NA ULINZI WA RASLIMALI ASILI.
Sheria mbili za mwaka 2017 ndizo ngao kuu za kulinda rasilimali za asili:
1. Sheria ya Umiliki wa Kudumu wa Rasilimali za Taifa, 2017 (Sheria Na. 5 ya 2017):
Inatamka kwamba rasilimali zote za taifa ni mali ya kudumu ya wananchi wa Tanzania na zinashikiliwa na Serikali kwa niaba yao.
sheria inataka mikataba yoyote inayohusu rasilimali za taifa kuhakikisha faida kubwa inabaki kwa Watanzania.
Inatoa masharti kwamba migogoro yote kuhusu rasilimali za asili lazima isikilizwe ndani ya Mahakama za Tanzania na siyo mbele ya mabaraza ya usuluhishi ya nje.
2. Sheria ya Mapitio na Majadiliano Upya ya Masharti Kandamizi, 2017 (Sheria Na. 6 ya 2017):
Inalipa Bunge mamlaka ya kupitia na kujadili upya mikataba yenye masharti kandamizi, ya kinyonyaji au yenye kwenda kinyume na maslahi ya taifa. Je tunalo Bunge la namna hii?
Sheria inataka kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji katika mazungumzo, usimamizi na utekelezaji wa mikataba inayohusu rasilimali za asili.Hivi hili la Makaa ya Mawe liliwahi kujadiliwa au kutangazwa wapi na nani aliyezuia Serikali Kununua Hisa husika?
Kusimamia kwa uthabiti utekelezaji wa Sheria Na. 5 na Na. 6 ya mwaka 2017 kama kinga ya mwisho ya kisheria dhidi ya unyonyaji na uporaji wa rasilimali ndiyo kingekuwa kipaumbele chetu
Utajiri wa asili ndiyo uti wa mgongo wa uhuru wa Tanganyika kuulinda si hiari bali ni jukumu la kikatiba, kisheria na kizalendo.
BAK MWABUKUSI.
Nilimsikiliza kwa Umakini Bisho Gwajima.
Alitoa fact na hoja zilizo dhahiri.Inahitajika ujasiri wa kipepo au kishetani kupinga ukweli ule.
Ajibiwe kwa hoja siyo Vijembe.
Yeyote asiye muelewa ni ama ndiye mtekaji Mkuu ,Wakala wa utekaji au mnufaika wa Utekaji kwa njia ya moja kwa moja au ile isiyo ya moja kwa moja.
CHA MUHIMU SASA TUJIUKIZE TUNATOKAJE HAPA...
Nafikiri Nchi hii inaongozwa na watu wa ajabu sana โฆ
Taratibu za kisheria za kusafiri nje ya Nchi ni zipi?
Taratibu ni kuwa na Passport yako .
Taratibu ni kuwa na VISA ya Nchi unayokwenda.
Na amekua akipa wapi bila kufuata taratibu?
Polisi polisi eleza hizo taratibu za kisheria ambazo Amani amekua akivunja na amefanya hivyo lini na lini?
Hivi hawa watu wanaweza kuwa viongozi wa Nchi hii?
Eleweni tu kwamba hakuna wa kurudisha mapambano ya kudai mabadiliko nyuma.
Tutawashinda.