@Roma_Mkatoliki Inawezekana, lakin tujipe time tusome mwenendo wa mchezo wao, mimi naona bado mapema sanaa kama wakicheza mchezo serious utawaathiri pakubea wao wenyewe kabla ya kufika 2030
Huwezi kutarajia fikra za standard ya juu kwa gharama za kiwango cha chini. Huwezi kuokoa mabilioni kwa kuogopa kuwekeza kiasi chenye uzito wa kimkakati katika kutafuta washauri wa kimataifa. Tatizo hapa si fedha ni upeo wa kufikiri.
Milioni kumi si bajeti ya kuunda dira ya usafiri wa jiji, hiyo ni pesa ya ushauri wa masuala ya “wikiendi wapi Dar kuna bamba?” Siyo ramani ya mageuzi ya mfumo wa usafiri wa jiji lenye mamilioni ya watu na linalobeba uchumi wa taifa.
Tatizo la foleni katika Dar es Salaam linachoma mabilioni ya shilingi kila siku. Linateketeza muda wa uzalishaji, linachafua mazingira na kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi, na linadhoofisha mahusiano ya familia. Ni jeraha la uchumi na mzigo mzito kwa maisha ya jamii.
Kama milioni kumi zinaonekana kuwa “pesa kubwa ya ushauri” kwenye meza ya maamuzi kwa ajili ya kutafuta suluhisho la foleni Dar, basi changamoto si foleni pekee bali ni kiwango cha fikra za uongozi na upana wa maono.
Huenda kabla ya kuondoa msongamano barabarani, tunapaswa kuondoa msongamano wa fikra finyu vichwani. Changamoto kubwa zinahitaji mawazo makubwa. Think big.
NB : Watu watembee kwa miguu Dar es salaam. Foleni zote zitakwisha kabisa. Pls naombeni Milioni kumi zangu.
Ukitaka kujua kiwango cha ujinga na uwezo mdogo kwa hawa watu sikiliza wanachosema…
Yaani huyu ni Waziri!!!! Kwamba wizara nzima, serikali yote mwaka 2026 miaka 65 baada ya Uhuru hawajui namna ya kutatua tatizo la foleni kwenye mji mmoja tu Dar?
Unawezaje kuwa na watu kama hawa, wanaua watu ili wabaki madarakani, hawana hata plan ya kuondoa matatizo ya watu?
Waziri mzima hajui hata namna ya kuondoa foleni tu!!! Na sio huyu tu, huyu anasema ni wao wote hawajui hata namna ya kutatua matatizo, kilimo, maji, Nishati, uchumi,Elimu , Afya nk!!!!! Ccm ni janga kwa Nchi.
Narudia tena kusema, mtu yoyote anayekuja na kauli za kusema
🗣️
“KUTOFAUTIANA MTAZAMO SIO UADUI”
Au sijui eti
🗣️
“USILAZIMISHE TUFANANE MTAZAMO NA MAONI”
Mtu huyo ni hana akili na hajui anachoongea!!
Yapo masuala tunapaswa woteeeee kuwa na mtazamo mmoja na maoni ya kufanana!!
MASUALA KUHUSU UHAI WA WATU NA HAKI YA KUISHI!!
Yani sisi tunapinga mauaji then ww unatuambia hatupaswi kufanana mitazamo, means wewe huyapingi mauaji? Unataka yaendelee?
Unataka utekaji usipingwe? Unataka tutofautiane mtazamo kuhusu kupinga utekaji? Wewe ni mjinga kabisa!!
Yapo mambo yanapingwa na kila taasisi duniani, so yanapaswa kufanana mtazamo na sio kila mtu awe na mtazamo wake!!
Mauaji/Haki ya kuishi!!
Hili linapingwa na waislamu/wakristo/makabila yote/Katiba ya nchi/Sheria za nchi/Tamaduni/Mila/Mungu/Yesu/Mtume!!
Wote hao wana mtazamo mmoja kuhusu hilo, then wewe uje useme kutofautiana mtazamo sio uadui!!
WEWE NI ADUI TU COZ UKO KINYUME NA KILA TAASISI DUNIANI!
Siku wapinzani wakiwa watawala wakaingia ikulu, amini kwamba hawa watawala ndio hawataweza kabisa kuwa wapinzani!!
Yaani sioni anayeziweza siasa za upinzani pale, sio wanasiasa wao wala wafuasi!!
Kwanza wengi watahama na kurudi kwa watawala!!
Siyo kila jambo linaweza kubadilika unapolikabili, lakini hakuna jambo linaloweza kubadilika bila kulikabili kwanza.Ujasiri wako sio tu kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani bali ni mindset transformation juu ya thamani ya utu na haki kwa vizazi na vizazi. Haupaswi kuwa jela hata kidogo. Nafikiri we are not doing enough kama wananchi.
Mdude Mpaluka Nyagali Polisi makao makuu waliunda mpaka Kamati kuchunguza mpaka sasa kimyaa japo afisa wao alitajwa bayana.
Mzee Kibao uchunguzi unaendelea,Soka na wenzake Mahakama ikaamuru Polisi wa chunguze mpaka leo kimyaa labada bado wanachunguza amri ya mahakama ,
soka na wenzake uchunguzi unaendelea?! Banjo katekwa na kuuwawa eneo lenye vifaa saidizi na kuzungukwa na ulinzi pale Arusha Uchunguzi unaendelea?!
Humphrey Polepole tunasikia mpaka baadhi ya Maafisa walirudi kuvunja gari lake na kuondoka na nyaraka...uchunguzi unaendelea
Namna pekee na sahihi ya kupata majawabu kuhusu utendaji wa polisi na vitendo vya utekaji ni kulichunguza Jeshi la Polisi.
Uchunguzi huru,Jumuishi na wakimataifa utategua kitenda wili cha mtekaji na muwezeshaji wa utekaji.
HAKI,UKWELI NA UWAJIBIKIJA UTALIPONYA TAIFA....siyo maombi ya kidini ya kisanii wala maridhiano ya jumla jumla na ya hadaa .
Zamu hii hatutakubali tena kupelekwa machinjoni kama kondoo wa kafara.
BAK MWABUKUSI.
@Baradhuli2@miss___yanga Kwahyo mliua watu ili mje mridhiane na wafu et?
Mlibembelezwa sanaa kabla ya uchaguzi mrekebishe mambo yakae sawa mkatia pamba masikioni et baada ya kutimiza adhma yenu ndo mnataka maridhiano!
Watafuteni,Soka,mdude,polepole, Chaula na wote mlioteka na kuwaua 29oct. mridhiane nao
WATANZANIA SISI NI WASHINDI NDANI YA MASAA 19 TUMEMCHANGIA JOVIN MILLION 10.
Jovini Kaaya ni mkazi wa Kimara Wilaya ya Ubungo Dar, Jovin amekuwa akimbeba Baraka kila alipofika mahakamani kwenye kesi ya uhaini, Jovini alionyesha moyo wa kipekee na kuvutia hisia za wengi, Baraka na Jovin waliachiliwa siku ya Jumatano.
MCHANGO HUU ULIKUWA NI SEHEMU YA MAANDAMANO YA HAKI NA KUONYESHA NGUVU YA UMMA.
Vijana wengi wanaweza kuyumbishwa kwa sababu ya pesa na mahitaji mbalimbali na tukakana hata imani yetu nilikuwa naangalia kwenye mtandao mmoja wale vijana wanaosema vijana Wakatoliki wamshtaki Kitima, Kitima ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania"
"Sasa eti vijana Wakatoliki wanamshtaki kwa Papa kwanza wanajua mlango wa Papa wanaingilia wapi? Papa utamuona wapi? lakini unaona ni vijana ambao wanatafuta umaarufu na kukana kabisa imani yao eti kwasababu ya kutaka uchawa ni ulevi fulani tu unaofanya vijana wanapoteza imani yao"- Askofu Eusebio Kyando kutoka Jimbo Katoliki Njombe
Tunaposema HAKI NI MSINGI WA AMANI hii kwa tafsiri ya kawaida ni kwamba "HUWEZI KUJENGA NYUMBA HEWANI".
Kwamaana kwamba lazima ujenge MSINGI kisha nyumba ifuate. Huwezi kujenga nyumba HEWANI lazima uanze na MSINGI.
KANISA KATOLIKI LINANAENDELEA KUPIGA PANAPOUMA
TUTAKUWEPO🫵😎
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga mkoani Kagera, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amesema kuna watu na makundi katika jamii ya leo yanayotumia nguvu, risasi na mabomu ya machozi kwa sababu ya kushindwa hoja, akifananisha tabia hiyo na akina Herode waliokataa kumpokea Yesu Kristo, Mfalme wa Amani.
Akizungumza katika Homilia yake, Askofu Rweyongeza amesema watu wanaoshindwa katika hoja, tafakari, midahalo na maridhiano mara nyingi hukimbilia matumizi ya nguvu ili kunyamazisha sauti za wanaotumia hoja na fikra.
Amesema kundi la kwanza la watu wasiompokea Yesu ni akina Herode, akiwataja kuwa ni watu wenye ubinafsi, uchu wa madaraka na ukatili, ambao hawapendi kushauriwa, kuonywa wala kusemwa, na badala yake hutumia nguvu pale wanaposhindwa hoja.
Askofu huyo amesema kundi la pili ni Mafarisayo, aliowataja kuwa ni wanafiki wanaotumia dini kama kifuniko cha kufanikisha ajenda binafsi, huku wakijifanya wacha Mungu lakini kwa vitendo wakijihusisha na vitendo vya ufisadi, unyonyaji na uharibifu wa taasisi za dini.
Ameongeza kuwa kundi la tatu ni la Yuda Iskariote, watu wanaomsaliti Yesu kwa busu, yaani wanaoonekana watakatifu kwa nje lakini ndani wakitafuta namna ya kunasa, kuharibu au kunufaika binafsi kupitia mali, sadaka na rasilimali za Kanisa.
Katika homilia yake, Askofu Rweyongeza amesema kundi la nne ni la akina Pilato, watu wanaoujua ukweli lakini huchagua kunawa mikono na kukaa kimya, wakiruhusu dhuluma, uonevu na mauaji ya haki kufanyika bila kuchukua msimamo wa wazi.
Ameeleza kuwa kundi la tano ni la wale aliowafananisha na Wayahudi waliomsulubisha Yesu, akiwataja kuwa ni watu wanaodhalilisha, kuumiza, kupora mali za waathirika, kuwanyonya wanyonge na hata kuwanyima yatima haki zao baada ya vifo vya wazazi wao.
Askofu Rweyongeza amesema makundi hayo bado yapo katika jamii ya leo na yanaendelea kutokumpokea Yesu kwa sura mbalimbali, licha ya kusherehekea Krismasi na kutambua kuzaliwa kwake.
Hata hivyo, amesema bado wapo watu wanaompokea Yesu kwa matendo yao, kwa kuishi katika haki, amani, maridhiano na kulinda utu wa binadamu, jambo ambalo amesema ndilo msingi wa ujumbe wa Krismasi.
Unang’ang’ania madaraka, unaua watu, unazuia wapinzani wako kushindana na wewe, unateka watu, unapoteza na kuua kikatili kama. Alivyofanyiwa mzee Kibao.
Unafanya yote hayo ili iweje, Kama maji tu yamewashinda miaka 64 iliyopita?
Sisi ni Nchi ya tatu kwa vyanzo vingi bora vya maji safi na baridi Duniani. Nchi ambayo mvua zinanyesha kila mwaka.
Asilimia 60 ya madawa yanayonunuliwa kwenye hospital zetu ni kwasababu ya magonjwa yanatokana na kutumia maji machafu.
Kwahiyo ukiwapa watu maji safi na salama ya bomba, utakua umeokoa 60% ya bajeti ya dawa zielekezwe kwenye mambo mengine. Pia utakua umeokoa maisha ya watu wengi sana.
Miaka 64 bado eti tuna wizara ya maji na watu wanatembea Nchi nzima, kuahidi kwamba tutaleta maji..
Ndio maana watanzania wanataka uchaguzi huru na haki waweke watu wanaoweza kuondoa kero hizi, lakini poa hao watu wakishindwa Watanzania wawe na uwezo wa kuwaondoa na kuweka wengine.
Unatumia mabilioni ya shiling kununua silaha, kulipana posho, kuua na kutisha watu kulinda madaraka uliyojipa mwenyewe bila ridhaa ya watu.
Ungewapa watu vitu wanavyohitaji wao wenyewe wangekutetea, matendo yako na uongozi wako ungekutetea sio silaha wala polisi.