VIDEO:
Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) limemkemea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kwa kile ilichokiita kutumia vibaya madaraka yake kwa kuelezea sayansi zinazoweza kuwachanganya Watanzania hasa kwenye matumizi ya pombe.
Akizungumza katika kongamano la tano la jumuiya ya wanawake wa kanisa la AICT Mkoani Mara Askofu Mkuu wa kanisa hilo Mussa Magwesela amesema kauli hizo zinaweza kusababisha kanisa kutokuaminika katika kukemea mambo machafu.
Aidha askofu Magwesela ameitaka serikali kuendelea kuliamini kanisa katika kukemea vitendo vya ukatili, udhalilishaji, ushoga na mauaji ya watu wenye ualbino huku akiiasa jamii kuepuka vitendo hivyo kwa kuwa vitawasababishia kuchomwa katika moto wa milele.