"Je, umeikosa Pepo, au umepewa habari kwamba hutakubaliwa?"
Tuliza moyo wako, kwani kila kitu kisichokuwa Pepo hakina thamani mbele yake.
Yaani, usihuzunike kwa mambo ya dunia; lengo kubwa la Muumini ni kupata radhi za Allah na kuingia Peponi.
📔 Elimu tukufu zaidi ni elimu ya Tawhiyd.
❍ Allah Ta'ala amesema:
«﴿ شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴾
"Allah Anashuhudia kwamba hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Na Malaika pamoja na wenye elimu pia wanashuhudia hivyo, huku Akiisimamia haki. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu, Mwenye hekima."
Surat Al 'Imran aya ya 18
🎓 Al-'Allaamah 'Abdur-Rahmaan As-Sa'diy رحمه الله amesema katika Tafsiri yake:
«"Katika aya hii kuna dalili kwamba jambo tukufu zaidi ni elimu ya Tawhiyd; kwa sababu Allah Amejishuhudia Mwenyewe juu yake, na Akawafanya viumbe Wake maalumu (Malaika na wenye elimu) kuwa mashahidi wake."»
📚 Taysur al-Karīm ar-Rahman (1/124).
Si jambo la busara kupuuza maneno au vitendo vinavyokuumiza kwa ajili ya kumlinda mtu fulani au kwa kuogopa kumpoteza.
Wakati mwingine kumpoteza mtu anayekuletea madhara huwa ni hatua ya kwanza ya kupona. Mtu anayejua thamani yake hujilinda na hujiepusha na maumivu mengi yasiyo ya lazima.
Hadithi ya Mtume ﷺ
«قال رسول الله ﷺ:
«حُرِّمَ عَلَى النَّارِ كُلُّ هَيِّنٍ لَيِّنٍ سَهْلٍ قَرِيبٍ مِنَ النَّاسِ»
(رواه الترمذي)»
Mtume wa Allah ﷺ amesema:
"Ameharamishwa kuingia Motoni kila mtu aliye mnyenyekevu, mpole, mwepesi (katika muamala), na aliye karibu na watu."
📚Imepokewa na Al-Tirmidhiy
Maana ya Sifa Hizi
1. هَيِّن (Hayyin):
Ni mtu mwenye unyenyekevu, utulivu na heshima, asiye na kiburi wala majivuno.
2. لَيِّن (Layyin):
Ni mtu mpole na mwanana katika maneno, matendo na muamala wake na watu.
3. سَهْل (Sahl):
Ni mtu mwepesi katika muamala, asiyeleta ugumu kwa watu, mwenye tabia njema na anayependa kurahisisha mambo.
4. قَرِيبٌ مِنَ النَّاسِ
(Qaribun mina an-Nas):
Ni mtu anayependana na watu, anayefikika kwa urahisi, mwenye ukarimu wa tabia na asiyejitenga nao kwa kiburi.
Anasema Mtumeﷺ
أكثرو الصلاة عليَّ يوم الجمعة وليلة الجمعة، فمن صلى عليَّ صلاة صلى الله عليه عشراً
Kithirisheni Kuniswalia Siku Ya Ijumaa [Mchana Wake] Na Usiku Wa Ijumaaa, Yule Atayeniswalia [Mara Moja], Allah Atamswalia Mara 10
[حسن لغيره]
[السنن الكبرى للبيهقي (٥٩٩٤)[
Hadithi ya Mtume ﷺ
«قال رسول الله ﷺ:
«إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَ عَلَيْكُمْ عُقُوقَ الأُمَّهَاتِ»
(رواه البخاري)»
Mtume wa Allah ﷺ amesema:
«"Hakika Allah Amekuharamishieni kuwaasi mama zenu."»
📚Imepokewa na Al-Bukhariy
Maana ya 'Uquuq (عقوق):
Ni kumfanyia mzazi ubaya, kumpunguzia haki yake, kutomtii katika mambo ya kheri, au kutomfanyia ihsani na wema unaomstahiki.
Kwa nini Mama ametajwa?
Ingawa kuwaasi wazazi wote wawili ni haramu, hadithi imemtaja mama mahsusi kutokana na ukubwa wa haki yake na juhudi kubwa anazozitoa katika ujauzito, kujifungua na malezi.
Hivyo, Uislamu umehimiza kwa msisitizo mkubwa kumtii, kumheshimu na kumfanyia wema.
✨Hadithi ya Mtume ﷺ
Kutoka kwa Abdullah bin Abbas رضي الله عنهما amesema:
Nilimsikia Mtume wa Allah ﷺ akisema:
"Lau mwana wa Adam angekuwa na mali kiasi cha bonde moja, bila shaka angependa awe na lingine mfano wake.
Na hakuna kitakachoyajaza macho ya mwana wa Adam isipokuwa udongo. Na Allah Anampokea toba yule anayetubu."
📚 Sahih Al-Bukhari (6437).
📜 Katika hadithi hii kuna dalili kwamba: Mwanadamu ataendelea kuwa na tamaa ya dunia na kutamani kuongezewa mali mpaka kufa, isipokuwa yule ambaye Allah Amemuwezesha kuwa na kuridhika (qana'ah) na kujitenga na tamaa za dunia (zuhd).
Al-Hasan Al-Basri رحمه الله amesema:
"Kila umma una sanamu wanayoabudu, na sanamu ya umma huu ni dinari na dirhamu."
📚 Al-Adab Ash-Shar'iyyah (3/297).
🌍 Isambazeni, kwani kusambaza elimu ni miongoni mwa mambo makubwa ya kujikurubisha kwa Allah.
1. Kuisha Kwa Wakati Kiasi Ambacho Akichukua Mara Tatu Wakati Wa Swala Utaisha, Itamlazimu Kutawadha Mara Mojamoja
2. Maji Machache
3. Kuwa Na Kiu, Ili Maji Mengine Atumie Kuyanywa Na Hali Hii Itakuwa Ni Haramu Kwa Mtu Kuchukua Udhwu Mara Tatutatu
4. Kupitwa Na Jama'ah
[Faida Ya Siku]
Katika Kutia Udhwu Ni Sunnah Kutawadha Viungo Mara Tatu Tatu, Na Hii Ndio Bora, Pia Ni Sunnah Mara Mbilimbili Na Ni Wajibu Kutia Udhwu Mara Moja...
Lakin Kuna Nyakati Au Hali Ambazo Zitambidi Mtu Kutawadha Mara Moja, Hali Hizo Amezitaja Al-Khatwib Ash-Shibinī
#KHILAFAH Hupatikana kwa Kutimiza Masharti ya Allah.
Waislamu wengi leo wanatamani kurejea kwa Khilafah na nguvu ya Ummah. Hilo ni jambo jema, lakini ni lazima litafutwe kwa njia aliyoiweka Allah, si kwa 'hisia' wala 'matamanio'.
Allah ameahidi khilafah kwa kusema katika Suratun-Nūr (24:55):
"Allah amewaahidi wale miongoni mwenu walioamini na wakatenda mema kwamba hakika Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya waliokuwa kabla yao, na Atawamakinishia dini yao Aliyowaridhia, na Atawabadilishia baada ya hofu yao wawe na amani. Wawe wananiabudu Mimi wala hawanishirikishi na chochote..."
Tunapoitazama aya hii kwa makini, tunaona kuwa Allah hakuanza kwa kuahidi Khilafah, bali alianza kwa kutaja masharti ya kuipata:
Imani ya kweli.
Matendo mema.
Kumwabudu Allah Pekee bila kumshirikisha na chochote.
Baada ya hapo ndipo Allah akaahidi mambo matatu makubwa:
Kuwapa Khilafah na utawala katika ardhi.
Kuimakinisha dini yao.
Kuwabadilishia hofu kuwa amani.
Hivyo, Khilafah si jambo linalopatikana kwa harakati za kisiasa pekee, maandamano, au kaulimbiu za kuutaka utawala wa Kiislamu.
Ni ahadi ya Allah, na ahadi za Allah hazipatikani isipokuwa kwa kutimiza masharti Yake.
Mtume ﷺ alikaa miaka kumi na tatu Makkah akiwajenga Maswahaba juu ya Tawhīd, Imani na utakaso wa nafsi, kabla Allah hajawapa dola Madinah. Huo ndio ulikuwa mwenendo wa Mitume na ndio njia ya ushindi.
Kwa hiyo, mwenye kutaka Khilafah ya kweli aanzie pale alipoanzia Mtume ﷺ: kusahihisha Aqīdah, kueneza Tawhīd, kufuata Sunnah na kutenda mema.
Hapo ndipo Ummah utastahiki ahadi ya Allah ya ushindi, utawala na amani.
Allahu A'lam
Mtume Muhammad ﷺ amesema..⏬
Mwenye kunidhaminia (kunihakikishia) kile kilicho kati ya taya zake (yaani ulimi wake) na kile kilicho kati ya miguu yake (yaani atajilinda na zinaa na atahifadhi tupu yake), basi mimi ninamdhaminia Pepo.
Maana yake ni kwamba mwenye kuudhibiti ulimi wake na kuhifadhi tupu yake na maasi, kwa idhini ya Allah atakuwa na sababu kubwa ya kuingia Peponi.
[Allah Hamuangamizi Mja Kwa Dhambi Aliyoifanya Mara Ya Kwanza]
Anasema Anas bin Mālik [Allah Amridhie]:
أتي عمر بشاب قد سرق،فقال: والله ما سرقت قبلها قط، فقال عمر:كذبت والله، ما كان الله ليسلم عبدا عند أول ذنب
Aliletewa Umar bnul Khatwāb Kijana Ambaye Kaiiba, Akasema [Yule Kijana]; Namuapia Allah Sijawahi Kuiba Hapo Kabla [Hii Ndo Mara Yangu Ya Kwanza],
Akasema Umar: Namuapia Allah Unaongopa, Hakuwa Allah Ni Mwenye Kumwangamiza Mja Katika Dhambi Aliyoifanya Mara Ya Kwanza
[صحيح]
[كتاب الزهد لأبي داود السجستاني (٥٦)]
Unapo Mchagua Mtu wa kuanza nae Maisha usiangalie tu Jinsi anavyo kufanya Ujiskie Vizuri angalia Jinsi anavyo ongea nawewe jinsi Mambo yanavyo kua Magumu 📌
[Kauli Ya Allah Na Mtume Wake Haiachwi Kwa Kauli Ya Yeyote Yule Awe Katika Watu]
Anasema Shaykh 'Abdul'Aziz bin 'Abdillah bin Baaz [Allah Amrehemu]:
"Amehimiza Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake] Kunako Jambo La Ndoa [Kuoa/Kuolewa], Kama Ambavyo Kitabu Cha Allah [Qur'an] Kimehimiza Jambo Hilo La Ndoa, Ama Kauli Ya Kuwa Ndoa Inafaa Kuachwa Au Ni Sheria Kuiacha Au Mfano Wake, Hii Ni Katika Kauli Mbovu,
Hata Kama Watafanya [Wataacha Kuoa] Baadhi Ya Watu, Na Kama Itaisihi Kuwa Ibn Jarir At-Twabarī Hakuwa Ni Mwenye Kuoa, Au Ikasihi Kuwa Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah Hakuwa Ni Mwenye Kuoa, Huenda Wao Walikuwa Na Udhuru, Lakin Sio Hoja Kwenye Jambo Hili,
Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake], Kwa Hakika Amekwisha Bainisha Jambo Hili Na Kitu Ambacho Amekibainisha Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake] Na Akalibainisha Allah Haifai Kwa Yeyote Yule Kubali Maneno Yenye Kwenda Kinyume Na Jambo Hilo, Hata Awe Nan,
Bali Ni Wajibu [Kwa Waislaam] Kuchukua Maneno Ya Allah Na Mtume Wake, Kwa Sababu Hao [Ambao Hawakuoa] Huenda Walikuwa Na Udhuru, Na Vilevile Sio Hoja Kwa Kile Chenye Kwenda Kinyume Na Sheria Ya Allah"
[دليل الزوجين (ص٢٥)]
[Abū Bakar Swidiq- 'Abdillah bin 'Uthmān bin 'Āmir bin 'Amrū bin Ka'ab Al-Qurashī-Radhi Za Allah Ziwe Juu Yake]
Anasema Bakar bin 'Abdillah [Allah Amrehemu]:
إن أبا بكر لم يفضل الناس بأنه كان أكثرهم صلاة و صوما، إنما فضلهم بشيء كان في قلبه
Hakika Ya Abu Bakar Swidiq [Allah Amridhie] Watu [Maswahaba] Walimfanya Kuwa Mbora [Kuliko Wao] Kwa Kule Kuwa Alikuwa Ni Mwingi Wa Swalah Na Funga Kuliko Wao,
[Hapana], Hakika Si Vinginevyo Walimfanya Bora Kwa Kitu Ambacho Kilikuwa Katika Moyo Wake [Imaani]
[صحيح]
]كتاب الزهد لأبي داود السجستاني (٣٧)]
[Qur'an Imeshushwa Ili Isomwe, Sio Kuninginizwa Kwenye Magari, Madukani Na Mfano Wake]
Anasema Shaykh Muhammad bin Swālh Al-'Uthaymin [ Allah Amrehemu]:
"Asili Katika Uandishi Wa Qur'an Katika Makaratasi, Na Katika Vipande Vya Mbao Ni Kufaa, Lakini Kuininginiza Katika Kuta Za Majumbani [Au Madukani] Halikuthibiti Hilo Kwa Wema Waliotangulia Allah Awarehem, Wala Sio Kwa Mtume [Swala Na Salaam Ziwe Juu Yake] Wala Maswahaba Zake Wala Tabi'ina,
Na Wala Sifahamu Kwa Uhakika Ni Lini Bid'ah Hii Ilianza, Na Hii Kwa Uhakika Bid'ah, Kwa Sababu Qur'an Hakika Si Vinginevyo Ilishuka Ili Isomwe Ni Sio Ininginizwe Kwenye Kuta Na Maeneo Yasiyokuwa Hayo"
[فتاوى نور على الدرب (١/١٧٤)]
[Dunia Ina Masiku Matatu, Yako Ni Leo]
Anasema Al-Hassan Al-Baswrī [Allah Amrehem]:
الدنيا ثلاثة أيام، أم أمس فقد ذهب بما فيه، وأم غدا فلعلك أن لا تدركه، فاليوم لك فاعمل فيه
Dunia Iko Na Masiku Matatu, Ama Jana Kwa Hakika Imeshaondoka Na Yale Iliyokuwa Nayo, Ama Kesho Huenda Usiwe Ni Mwenye Kuidiriki [Kuifika],
Na Siku Ya Leo Ndo Ya Kwako, Bas Fanya [Matendo Mema] Ndani Yake
[كتاب الزهد الكبير للبيهقي (٤٧٧)]
👉🏾 Tujitaidi Tuwe Ni Kufanya Matendo Mema Leo, Kusubir Kesho Ambayo Hatuna Uhakika Wa Kuifika Ni Kuipoteza Siku Yetu Hii Ya Leo