Tarehe 30 Desemba 2006, asubuhi ya Sikukuu ya Eid, Saddam Hussein alisimamishwa juu ya jukwaa la kifo.
Alivaa koti la rangi nyeusi, suruali ya kijeshi, na shati jeupe. Alikuwa mtulivu, lakini macho yake yalionyesha dharau.
Saddam alifungwa mikono yake kwa nyuma huku miguu yake ikifungwa minyororo.
Saddam alipandishwa kwenye jukwaa tayari kwa kunyongwa, alipokuwa akipanda kwenye jukwaa mmoja wa walinzi alisikika akisema "Nenda Motoni" na kumfanya al-Faroun awaonye watu kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kusema chochote.
Wakati kamba ya kunyongwa ilipofungwa shingoni mwake, aliangaliana na waliokuwepo, huku akikariri maneno ya kidini..... Subiri
Ilikuwa ni Desemba 13, 2003. Usiku ulishashika hatamu katika kijiji cha Ad-Dawr, kilicho karibu na Tikrit, Iraq.
Kundi la askari wa Marekani waliokuwa wakifanya operesheni ya siri walifika katika eneo ambalo walihisi kuwa mtu aliyekuwa akitafutwa zaidi duniani angeweza kujificha.
Wakiwa na bunduki zenye miangaza mikali, walizunguka shamba dogo la mitende. Chini ya mti mmoja, kulikuwa na shimo lenye mfuniko wa mbao.
Walipolifungua, walimkuta mtu aliyekuwa amechoka, mwenye ndevu ndefu zilizokuwa zimejaa vumbi na macho yaliyokuwa yamepoteza matumaini.
Hakuwa mwingine bali Saddam Hussein, mtu aliyewahi kuitawala Iraq kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 24.
Huyu ndiye Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti, mtu aliyewahi kuwa mfalme asiye na taji wa Iraq, lakini mwisho wake ulikuwa wa fedheha na udhalilishaji wa hali ya juu.
Thread 🧵 ⬇️
Ila Lissu ni kichwa sana aisee Kama usipoelewa hapa basi una matatizo ya akili Kaeleza kuhusu zanzibar inavyonyonya bara hadi mwili ukachoka https://t.co/23C30ZFgBR
Siku zote za msiba wa Magufuli, Kinana, KIPARA na Nape hawakufika lilipo jeneza la Magufuli. Akiwa hai walimuita mshamba na amechanganyikiwa. Baada ya miaka miwili kupita, leo, sielewi kimemsibu nini Kinana hadi kwenda katika kaburi la Magufuli, Chato. Unafiki wa MaCCM…