MKWELI,MPENDA HAKI ,MTU WA MUNGU ,ASIYEYUMBUSHWA NA MALI ZA DUNIA , POSITIVE MINDSET ALWAYS,najivunia Sana kuwa muumini wa TUNDU LISSU ❤️🙏
#FREETUNDULISSU#FREETUNDULISSU
…. Lissu ni Alama ya nguvu, msimamo thabiti na kujitoa kwa moyo wote kwa ajili ya wengine.
Mtu anayewapenda na kuwatumikia watu wake kuliko anavyojipenda mwenyewe.
Hakika huyu mzee, ni roho ya kimalaika inayotembea miongoni mwa watu.
Muachilieni Huru.
Tundu A.M Lissu alikamatwa akiwa Mbinga, Ruvuma Aprili 9, 2025. Tangu tarehe hiyo ya kukamatwa (Aprili 9, 2025) hadi leo (Mei 20, 2026), zimepita siku 406.
Februari 24, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Ndogo ya Dar es Salaam) iliahirisha kesi hiyo kwa muda usiojulikana (sine die). Shauri la msingi likasimama.
Hatua hii ilikuja baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha shauri la mapitio/rufaa katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania kupinga uamuzi mdogo wa Mahakama Kuu.
Tangu upande wa Jamhuri ukimbilie Mahakama ya Rufaa na kesi ya msingi kusimamishwa (Februari 24, 2026) hadi leo (Mei 20, 2026), jumla zimepita siku 85.
Tunawauliza Serikali, hamtaki kuendelea na kesi yenu dhidi ya Tundu Lissu? Ushahidi wenu hautoshelezi? Vielelezo vya kuthibitisha kesi yanu vimeyeyuka?
Tunawauliza @judiciarytz, hamtaki kesi dhidi ya Tundu Lissu iendelee? Kwanini tarehe haipangwi baada ya siku 85 kupita? Majaji wa mahakama ya rufaa hawapo?
Kama hamtaki kuendelea na kesi kwa njia za mahakama, muachieni huru Tundu A.M Lissu. Kama mnataka kuendelea na kesi yenu, pangeni tarehe haraka sana.
Vinginevyo, mnaulazimisha UMMA kusimama na kumdai Tundu A.M Lissu. CHADEMA tunamtaka kiongozi wa chama chetu, uraiani. Tunasisitiza, #FreeTunduLissu.
Tafadhali sana, muachieni Eng David Djumbe mara moja. Djumbe ni msaidizi wa Tundu Lissu; na zipo taarifa za majaribio ya kumteka tangu mwaka jana. Nimesikitika kufahamu ametekwa jana usiku.
Free David Djumbe Now!
Tundu Lissu si mhalifu, ni sauti ya wananchi wanaodai haki na demokrasia. Kumweka gerezani ni kuinyamazisha Tanzania. Tunadai aachiwe huru sasa!!
#Katibampya#Freetundulissu
Wamemteka David Djumbe, Msaidizi binafsi wa Tundu Lissu.
Nimezungumza na mke wake usiku huu, wamemteka akiwa karibu kabisa na nyumbani kutoka mihangaikoni, wameondoka na yeye pamoja na Gari yake.
Ikumbukwe ametekwa siku moja tu baada ya kurudi nchini.
TUSAIDIANE KUPAZA SAUTI.
Giza limekuwa refu mno, na kila sekunde anayokaa ndani ni pigo kubwa kwa mioyo yetu. Sauti ya haki haiwezi kufungwa milele kwenye kuta nne za baridi za Ukonga. Tunatamani kumuona akitembea kwa amani, akitabasamu na kurudi kwenye mikono ya familia na mamilioni ya Watanzania wanaomwombea. Mwachieni Mheshimiwa Tundu Lissu, uonevu sasa basi! 🕊️💔"
#FreeTunduLissu #BringBackOurLeader #HakiZaBinadamu