Mungu tupe kibali cha kuuona uovu wetu ili tuweze kuudhibiti, mapungufu yetu ili tuweze kujijenga na Zaidi tupe uwezo wa kuweza kuuchimba mgodi wa dhahabu uliopo ndani yetu, maana bado tunajiogopa na hatujamini katika ukuu, nguvu na vipawa ulivyo tujalia ndani yetu
Nafikiri hiki ndicho Kipindi tasnia ya Burudani imepata uwakilishi mkubwa kwenye ngazi za maamuzi.
Bungeni - Babu Tale,Baba Levo, Sanga, Dotto Bahemu, Kijah Yunus, Keisha.
Serikali kuu - Naibu Waziri Mwana FA/DC Nikk wa Pili /DC Mchopanga
Serikali za Mitaa - Shetta, Dogo Janja.
Naitakia kila la kheri Timu yetu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 20 (Tanzanite Queens) inapoanza safari ya kulitumikia na kuliheshimisha Taifa letu katika mashindano ya Kombe la Dunia la 2026 yanayoanza leo nchini Poland.
Ushiriki wenu katika mashindano hayo makubwa duniani ni heshima na fahari kubwa kwa nchi yetu. Aidha, ni uthibitisho wa uwezo, vipaji na juhudi za mabinti zenu, na pia ni chachu ya kuhamasisha na kukuza ushiriki wa wanawake katika michezo.
Tunawatakia kila la kheri. Taifa lenu lipo pamoja nanyi.
Tabia zetu nikubwa kuliko mipango yetu, kabla ya kuweka mipango yetu kwanza tuchunge na kuchunguza tabia zetu, bila kufanya hivyo mipango yetu itaishia kuliwa na tabia zetu
Ukichagua kupambana kimaisha upige hatua hiyo njia ni ngumu, ukikata tamaa na kupoteza matumaini na kurudi nyuma hiyo njia pia ni ngumu, njia yoyote utakayo chagua Maisha sio rahisi, so no excuse
Leo jijini Dar es Salaam nimeungana na viongozi wengine wa Afrika kufungua Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika, ambapo Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji. Jukwaa hilo, linaloadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, limekuwa sehemu muhimu ya kuunganisha mitaji, miradi na wataalamu ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani Afrika.
Katika mkutano huo nimeeleza kuwa, Tanzania inashirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu, ikiwemo barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Hatua hii inachochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa kupunguza gharama za usafirishaji, kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kutoa ajira na kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha usafirishaji.
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kimazingira duniani, nimesisitiza umuhimu wa Afrika kuimarisha miundombinu inayohimili mabadiliko hayo na kuunganisha nchi zetu ili kuendelea kukuza biashara, uwekezaji na uongezaji thamani wa rasilimali zetu.
Edward Jenner mgunduzi wa chanjo ya ndui 1796 iliyo okoa mamilioni ya Maisha ya watu duniani lakini pia ndiyo ilikua chanjo ya kwanza ya kinga na kufungua milango ya chanjo nyingine zoote. Kifupi huyu ni baba wa immunology.