utakuwa una funza kichwani kuamini kwamba changamoto za mwendokasi zinatokana na nani ni bosi wa mamlaka hiyo. the fact that it has to take the president to decide who runs the authority speaks volumes to the seriousness of the problem. this is a gimmick, don't fall for it.
Tundu Lissu is a patriotic son of our land.
He has shown us the way.
He has given us courage.
He has reaffirmed our collective demands for electoral justice.
His fight is our fight.
We are Tundu Lissu.
#IamTunduLissu
Ujumbe kutoka gerezani wa Mh. @TunduALissu
Jaji Hamidu Mwanga ni Jaji wa Samia, na kwasababu hiyo ni Jaji wa CCM na anafanya kazi ya CCM. Jaji Mwanga alikuwa kwenye Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya Jecha Salimu Jecha ambayo ilifuta uchaguzi wa Zanzibar wa 2015. Jaji wa namna hii tutatarajia aipende CHADEMA inayosema No reforms No election?????
Maamuzi yake yanathibitisha kauli yangu kwamba Majaji wengi ni Ma-CCM na wanafanya maamuzi kuipendeza CCM na yule anaeweza kuwapandisha madaraja kwenda Mahakama ya Rufani.
Kuhusu kuzuia shughuli za Chama; Chama ni wanachama, sio majengo, hata kama majengo ni muhimu lakini chama ni wanachama na wanachama waendelee na mapambano katika majukwaa yote yanayopatikana hasa katika mitandao ya kijamii isipokuwa katika jengo la Makao Makuu.
Wanachama wakumbuke historia ya mapambano ya aina hii. Chama cha ANC kilipigwa marufuku na serikali ya makaburu kwa miaka 30, viongozi wake wakuu ama walifungwa maisha Robben Island kama Mandela na wenzake au walikimbilia uhamishoni kama Oliver Tambo, Thabo Mbeki na wengine.
Hayo yote hayakuzima mapambano ya ukombozi kuendelea na hayakuiua ANC. Uamuzi wa Jaji Hamidu Mwanga hautazuia mapambano kuendelea wala kuiua CHADEMA.
ALUTA CONTINUA
-Admin