@McinikaWaLamar Gawio halitegemei umekaa na hisa miaka mingapi; kinachojalisha ni kununua kabla ya tarehe ya mgao. Unaweza pata gawio hata ndani ya miezi michache kama timing ni sahihi.
"Penye makutano ya watu na taarifa ndipo panapokaa rizki nyingi. Katika mahangaiko yako hakikisha mara kwa mara unakuwemo au unazungukia maeneo hayo. Ukizengea zengea hapo, ama utapata mtu au watu watakaokufungulia fursa, au utapata taarifa muhimu kuhusu fursa itakayokufaa."
"Kila mtu ana mapungufu yake na vilema vyake. Kinachofanya tusione mapungufu na vilema vya watu wengine ni sababu wanao watu wanaowafanya tuwaone wamekamilika kwa kuwavumilia mapungufu yao ama kuyasitiri. Muhimu uwajue wanaokukamilisha maishani na waenzi waendelee kukusitiri."
Bado tuna shida mahala sisi VIJANA . Inaonekana bado ngumu kukubali ule msemo
1: " Hii KEKI ni kubwa sana kila mtu atakata kipande chake na bado itabaki "
2: " Kwani kuna shida wote tukishinda / Kufanikiwa " ?
Upatikanaji wa hizi hela unafanya watu kuchukiana/ kuharibiana
@MayengoDr@NMBTanzania Duuh ngoja nitawacheki tena walinambia maybe naweza kufungua account yao inaitwa Dhahabu initial amount 100k ukitaka kutoa ni kuanzia one year na kuendelea
MAN TO MAN
Kukata tamaa ni anasa ambayo wanaume dhaifu huichagua.
Hakuna anayejali visingizio vyako. Hakuna atakayebeba mzigo wako. Ukiacha njiani, mtu mwingine atachukua maisha ambayo yangeweza kuwa yako.
Ukweli wa maisha ni kwamba dunia haiwapi nafasi wanaume wanaolalamika bali wanaopambana. Simama, jikaze, na endelea kupigania maisha unayotaka.
WANAUME tunakuwa bora zaidi pale tunapojiboresha kihisia, kifedha na kiafya. Kwa hiyo Linda sana afya yako ya akili, imarisha afya yako ya mwili, na pambana kuboresha hali yako ya kifedha hata kama kipato ni kidogo Hapo ndipo nguvu ya mwanaume halisi na mpambanaji anapoonekana. 💪