"Fanya uwezavyo katika maisha yako na haswa katika watu wako wa karibu uwe na walau mtu mmoja anayeweza kukuuliza maswali magumu, machungu na usiyoyapenda." ~
"Mambo unayoyaona madogo madogo katika maisha ndio mambo yote katika maisha. Ukisema usubirie makubwa yaje, hatujui yatafika lini, na wakati unayasubiria, maisha hayasimami kukusubiria. Furaha ya maisha iko kwenye hayo madogo madogo”
"Wengi wanaojitafuta wanaiga wengi waliojipata sababu hakuna anayependa kuishi kwa shida. Tatizo ni wengi waliojipata hawana vingi vizuri vya kuigwa na wengi wenye vizuri vya kuigwa wanaficha uhalisia wa jinsi walivyojipata. Jitafute kivyako vyako." ~
"Nidhamu ya maisha inahusisha kuchagua na kuheshimu mrengo wa maisha na kuuishi mrengo huo bila kuyumba. Inahusisha ratiba zako, machaguo yako, kujipangia vipaumbele, bajeti, ukomo wa anasa na starehe. Usipokuwa na mrengo utayumba kimaamuzi juu ya mwelekeo wa maisha yako."
Changamoto za kimaisha, kama magonjwa, Migogoro, kupoteza kazi, biashara kuyumba, usidhani vinatakiwa kuwatokea watu flani pekee, au ukafurahia sababu huwapendi au una tofauti nao.
It can happen to anyone, hata wewe.
Tutakiane kheri kwenye mapito yetu.
"Furaha kama ilivyo Huzuni ni misimu inayopishana katika maisha yetu. Furahia vya kutosha wakati wa msimu wa furaha uwe na akiba na kumbukumbu ya kutosha ya furaha ya kukuliwaza na kukuvusha msimu wa huzuni."
"Pesa haikosi washauri. Ukiipata, utapata washauri wengi ambao hukuwaona wakati unazitafuta. Watakuletea mipango mizuri ya pesa wakati ama wenyewe hawana pesa au hawako tayari kujaribisha mipango hiyo mizuri na pesa zao. Waogope."
"Riziki na fursa ni kama basi la abiria. Kila fursa na kila riziki inakupeleka katika uelekeo fulani, inakukutanisha na watu fulani, inakupitisha katika hatari fulani na kukupa mafanikio ya aina fulani. Usidandie bila ya kusoma kibao."
@SikilizaTogolan "Katika maisha yako tofautisha kati ya fadhila (priviledge) na haki (right). Haki ni stahili, fadhila ni tunu. Unaweza kuidai haki lakini huwezi kuidai fadhila. Epuka kuizoea fadhila, maana ikikuzoea itakugeuza Mfungwa wa Nadhiri."
"Kama unapokwenda katika maisha ni mbali kuliko ulipotoka, basi mahasidi uliokutana nao ni wachache kuliko utakaokutana nao mbele. Visasi na nongwa dhidi ya uliowavuka vitakuchelewesha tu kufika. Wekeza nguvu kujiandaa na wajao."
"Kabla ya kuchukua hatua kutekeleza nia au uamuzi wowote, jenga tabia ya kuweka swali mwishoni,' HALAFU?' Ndipo utapogundua kuwa baadhi ya dhamira na maamuzi yako ni matokeo ya hasira, mhemko au hisia za wakati huo tu."
When you believe, it doesn’t mean the road ahead is smooth all the way. Far from it. Expect the Almighty to test you if you’re true to your word. Remember, faith is not the belief that He will do what you want, it is the confidence in knowing that He will do what’s best for you.
@SikilizaTogolan "Si kila anayekuudhi au kukuchokoza ni wa kugombana nae. Wengine wameumizwa na kujeruhiwa watokako wanatafuta pa kumalizia hasira zao au kupangusia lawama zao. Wakwepe.Gombana na mtu tu ikilazimu na kama una safari naye katika maisha yako."
@SikilizaTogolan "Ni rahisi kudhani matatizo aliyonayo mtu mwenye uwezo zaidi yako ni madogo kuliko tatizo lako kubwa. Uyaonayo madogo kwake yaweza kuwa ndio makubwa kwake. Ukimlilia shida na akakuambia hawezi kukusaidia, usimkasirikie."
@SikilizaTogolan "Usidharau jukumu au kazi yoyote. Kila upewapo jukumu au kazi, iwe ndogo au kubwa, yenye maslahi au isiyo na maslahi, wewe ifanye kwa uwezo wako wote maana huwezi jua ni ipi itakayokujenga na kukubariki." ~
@SikilizaTogolan "Usihadaiwe na umoja na viapo wakati wa kula njama. Ukishiriki au kushirikishwa jambo lolote haramu usimtegemee mtu kunusuru nafsi yako. Mambo yakishaharibika kila mmoja huwa na wajibu wa kuokoa nafsi yake." ~
"Uzee wako utakuonyesha usahihi wa maamuzi yako ya ujanani ikiwemo ndoa, idadi ya watoto, malezi, mahusiano, kipato na uwekezaji, na machaguo yako mengine ya maisha. Kuwa makini na maamuzi yako ya ujana." ~