Baadhi ya Picha wakati Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa akipokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania https://t.co/Lfh4KXcozL Phillipo Mpango alipowasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere akitokea Vatican ambapo alipewa hadhi ya Ukardinali na Papa.
Heri ya miaka 73 ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete. Ahsante kwa utumishi wako kwa umma wa zaidi ya miaka 50 kwenye Chama Cha Mapinduzi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na baadaye kama Rais wa nchi yetu. Nakutakia afya njema na wakati mwema unapokumbuka siku hii.
POLISI JAMII YAANZA KULETA MATOKEO CHANYA - SONGWE
Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Theopista Mallya Oktoba 06, 2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kununua tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya shule ya sekondari ya
Nimekumbuka hapa kipindi naishi home kwa ma mkubwa Ukonga kuna siku tulirudi home alfajiri na bro tumetoka batani tukakuta watu na viti tukajua msiba(tukajiuliza nani tena tuko kwa fensi turuke) kumbe jumuiya iko home๐๐๐
TANZIA: Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amefiwa na mke wake Lady Cathy Ferguson ambaye ameaga Dunia akiwa na umri wa miaka 84 na kuacha watoto watatu, wajukuu 12 na kitukuu mmoja.
Katika taarifa yake ya leo Septemba 6, 2023 Manchester United imesema "Kila mmoja ndani ya Manchester United anatuma salamu za rambirambi kwa Sir Alex Ferguson na familia yake kwa kuondokewa na Lady Cathy.โ
"Kama ishara ya heshima, wachezaji wetu watavaa kitambaa cheusi wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Brentford." Imesema taarifa hiyo.
Bendera katika uwanja wa Old Trafford zimeshushwa nusu mlingoti huku timu za Wanawake na wanaume za klabu hiyo zitakazocheza mwishoni mwa Juma zitavaa vitambaa vyeusi kama ishara ya kuomboleza.
Sir Alex Ferguson alistaafu mwaka 2013 baada ya kuiongoza United kwa zaidi ya miaka 26 na kusema kutumia muda mwingi na Cathy na familia yake ni moja ya sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo.
#KitengeSports
CCM imewafanya watanzania wafurahie umaskini na kuwachukia watu waliofanikiwa. CCM imewafanya watanzania wajione ni marafiki wa karibu na umaskini. CCM inawaita maskini wanyonge ili kuwasahaulisha umaskini wao. Tanzania ina rasilimali zinazotosha kuondoa umaskini wa kila raia.