Uwanja mpya wa michezo wa Arusha (Samia Suluhu Hassan Stadium)
Eneo ulipo: Olomoti, Arusha
Ukubwa: Mita 105 kwa Mita 68
Uwezo: Watu 30,000
Ujenzi ulipofikia: 42% (Juni 1, 2025)
Ukipata Nafasi Tazama Picha Hizi Za Wapiga Picha Wanafanya Mambo Ya Ajabu Ili Wapate Picha Kali
Wengine wakiweka maisha hatarini kwa ajili ya shot kali
Kwa wapiga picha, passion ndiyo kila kitu.
Watavumilia lolote ili wapate kile wanachokiona akilini.
Fungua Thread 📸🧵
Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana.
Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wanaochuja Wagombea wa uchaguzi watende haki na wapime kwa umakini na kuangalia wale wanaofaa ili kuepuka kupitisha Wagombea ambao wanakosa sifa na kuendana na yale ambayo CCM inayataka.
Akiongea wakati wa kufunga Mkutano Mkuu leo May 30,2025, Rais Samia amesema “Niwaombe au sijui niagize vikao vinavyokwenda kuchuja Wagombea wakatende haki, wakatende haki, anayefaa aambiwe anafaa, asiyefaa tuseme huyu ana kasoro mbili tatu hatufai kwa huko mbele tunakokwenda, tukitoa mwanya Ndugu zangu, tukipitisha wanaotafuta tu na Mie niwemo ndio tunapata wale wanaokwenda huko, Chama kinakuwa Gwajimanize”
“Kwahiyo kwa vyovyote tusigwajimanize Chama chetu Magwajima tuyaache nje, hamna kuoneana aibu wala aya”
“Unajua kule Zanzibar kuna Mtu aliimba mcheza ngoma sio yake lazima ataharibu, akasema hawi sawa na wenzake anakuwa Majuzubu, Majuzubu ni Mtu ambaye hazimo hazimo hivi, kwahiyo ukicheza ngoma sio yako utaharibu na utajulikana lazima utasema Mimi sie jaman ndio haya yanayotoke, kwahiyo twendeni tukachuje kwa ustadi mkubwa”
#MillardAyoUPDATES
@SuluhuSamia Hii Barabara tunaomba mtuwekee rami ni Barabara fupi mno inayounganisha watu wa kutoka Dar na mikoa ya Kaskazini hususan watu wanotoka Arusha, Moshi, Tanga Kupitia Chalinze, Msolwa Mdaula Ubena Zomozi Ngerengere Jeshini Unanyoosha moja kwa moja mpaka mvuha kisaki.
@SuluhuSamia Pia Barabara kubwa inayopita magari mengi mnoo makubwa hususani ya mizigo inayoenda kwenye mradi ya bwawa la Mwalimu Nyerere na Mabasi ya Abiria yanayoenda kwenye miji ya Dutumi mpaka kisaki na magari ya watalii yanayoenda kwenye mbuga ya Mwalimu Nyerere...
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua ilani ya Chama hicho kwa mwaka 2025/30 ambayo itatumika kukinadi Chamaa hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi October 2025.
Rais Samia amezindua Ilani hiyo kwenye Mkutano Mkuu Jijini Dodoma leo ambapo kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM na Waziri wa Mipango Prof. Kitila Mkumbo amesema katika kulinda mafanikio makubwa yaliopatikana wakati wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 na katika kukuza uchumi jumuishi na kuimarisha ustawi wa Watu wote, Serikali imetakiwa kuchochea mapinduzi ya uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani utakaojengwa katika misingi wa kuongeza thamani rasilimali zinazozalishwa nchini.
Prof. Kitila amesema hayo wakati akiwasilisha muhtasari wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Mwaka 2025/30 ambapo amesema “Kipaumbele kingine ni kuongeza fursa za ajira kwa Vijana, kuongeza kipato kwa Wananchi na kupunguza umasikini, Kuboresha maisha ya Watu na ustawi wa jamii, kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kukuza na kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za kiuchumi na kijamii”
“Kipaumbele kingine ni kudumisha demokrasia na utawala bora, kuendelea kudumisha amani, utulivu na usalama, Kudumisha utamaduni wa taifa, na kukuza sanaa na michezo pamoja na
Kuongeza kasi ya maendeleo vijijini”
#MillardAyoUPDATES