#TajiriLaKihaya
Ujue Serikali Nyingi Huwa inatumia kanuni ya ‘TENGA UTAWALE’
DIVIDE AND RULE…
Hii hurahisisha saana Utawala wao… na kutuweka busy na mambo yasio na muhimu wao wakiendelea kula mema ya nchi…
Tumejitahidi kwa kiasi chake kuDeal na Mambo ya Wasanii na Miziki yao…
Tumejitahidi kwa kiasi chake Kudeal na Mambo ya Simba na YANGA… mamipira..
Vile vile Naomba Saana Tujitahidi Kudeal na UDINI…
UDINI ndio silaha kubwa zaidi kuzidi zote… MAANA inashika Imani za watu- na waafrika wengi Huwaambii kitu kuhusu Dini…
Kama ambavyo kwenye Simba na Yanga Tumedeal na Viongozi wao, kwenye miziki tumedeal na Wasanii na kuacha kuwafuatilia ila MASHABIKI tumebaki kuwa wamoja … let the same Apply to Maswala ya DINI…
Masanja Mkandamizaji,Mwamposa,KKKT na wengineo Wakiharibu Tunadeal nao na Sio Wakristo wote wala wafuasi wao…
BAKWATA wakionekana wameramba Asali - tudeal nao wao… viongozi hao na wala sio waislamu wote au Masheikh wote…
Tutaacha mambo ya muhimu na kudeal na vitu ambavyo havifai mwisho wa siku Tunapoteza FOCUS.
Kama MUISLAMU nawaambia BAKWATA sio Taasisi ndogo kama tunavyoichukulia- Dar es salaam,Pwani,Tanga,Dodoma,Singida,
Tabora,Zanzibar NK- misikiti ya Bakwata ni asilimia 98% ya misikiti yote mnayoiona…Mikoa yote mikubwa na wilaya zote Tanzania nzima misikiti mikubwa ya IJUMAA ni ya Taasisi za BAKWATA.
Kiufupi asilimia 90% ya waislamu NCHI nzima viongozi wao ni BAKWATA na wanawafuata kweli kweli… mfano mzuri tu angalia - sikukuu za iddi… wengi huwafuata BAKWATA na wanaoswali siku tofauti ni wachache mno- hata kama zote zitaangukia weekend.
Ninataka kusema nini… tujichunge saana Tusipoteze FOCUS yetu mwisho wa siku tukapoteza nguvu na muda wetu kwenye maswala ya DINI…
Kama ambavyo BAKWATA walituamrisha TUFUNGE Jumatatu siku ambayo Raisi alikua anaapishwa na TUKAKAUSHA hakuna Aliefunga- tukaendelea na mambo yetu…
Tuendelee vivyo hivyo… maana Hatukuwatukana wala kuwavunjia heshima…
Hakuna ambae atapigana na Dini akashinda… hata msemaje hakuna muislamu ambae atahama awe mkatoliki na vivyo hivyo hakuna mkatoliki atahama awe muislamu…
Tuendelee kupigania tunachokiamini bila Kuvunjiana Heshima kwenye Dini… ADUI wetu ni mmoja tu… na atafurahia saana tukiingia kwenye huu mchezo wa UDINI.
Viongozi wakiongea ‘Pumba’ zao tuwakaushie infact hata Airtime hio ya kuwajadili tusiwape… lets FOCUS na mambo ya muhimu- Positive vibes only!
Hakuna kipindi inapaswa tuwe wamoja kama hiki…
Hakuna MUISLAMU KAMILI atafurahia unapowatukana MASHEIKH ZAO - hata mm sifurahii mnapowatusi masheikh hawana Elimu… mara sijui wanakula kitimoto… matusi ambayo hayana Tija kutafuta likes na engagement za kipuuzi.
Tofauti na mitazamo yetu kwenye siasa kuwa Tofauti…hawa ni Masheikh zetu kwenye Imani… ni waalimu wetu wa madrasa ni viongozi wetu wa Kiroho…
Lets maintain our FOCUS…
tukianza kujigawa kwenye UDINI… kuna wengi kimbilio lao litakua DINI KWANZA…and it will be worse!
Now Tunataka KATIBA MPYA, Tume ya UCHAGUZI IVUNJWE , waliouwa ndugu zetu WAWAJIBISHWE, Haki ipatikane kwa wote walioathirika, vijana wetu waliopotezwa wapatikane wakiwa Hai au miili yao, wafungwa wa Kisiasa wote waachiwe huru bila masharti, Kesi zote za CHADEMA mahakamani zitupiliwe mbali na waachwe waendelee na kazi zao!
Ikiwezekana UCHAGUZI MKUU URUDIWE…. Hata kama ni gharama tupo tayari kukaa miaka mitano bila maendeleo yoyote- ila viongozi tuwachague sisi kihalali💯
Lets maintain our FOCUS…