Natoa salamu zangu za pole kwa Mh. Dkt. @SuluhuSamia kufuatia msiba wa kufiwa na mume wake.
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Kama Qur’an Tukufu inavyosema:
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ
"Kila nafsi itaonja mauti."
(Qur’an 3:185)
@SuluhuSamia Katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi, namuomba Mwenyezi Mungu akupe subira, nguvu, utulivu wa moyo na faraja. Mwenyezi Mungu amsamehe marehemu, amrehemu, amjaalie makazi mema Peponi, na awape familia yote subira na nguvu katika kipindi hiki cha majaribu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) tarehe 28 Februari, 2026 Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) tarehe 28 Februari, 2026 Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel: Ikulu Tanzania na Tovuti: https://t.co/wmldPXYfck
_________
#MaendeleoEndelevu
#TabasamuLaUtu
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga katika kikao na Watendaji wa Wizara ya Maji wakiongozwa na Waziri wake, Mhe. Jumaa Aweso leo Februari 12, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Februari, 2026 kabla ya kuondoka nchini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).
_________
#MaendeleoEndelevu
#DiplomasiaYaKiuchumi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Bole, Jijini Addis Ababa Ethiopia, tarehe 12 Februari, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokelewa na Waziri wa Kazi na Ukuzaji wa Ujuzi wa Ethiopia Mheshimiwa Muferihat Kamil Ahmed.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TabasamuLaUtu
#maendeleoendelevu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Abubakari Asenga, wamepatiwa mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya utafiti ya REPOA, leo tarehe 12 Februari, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mashimba Ndaki, katika kikao na Watendaji kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, leo Februari 12, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mhe. Edwin Swalle, katika kikao na watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiongozwa na Naibu Waziri wake, Mhe. Regina Qwaray.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly katika kikao na Watendaji wa Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Februari 12, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Hawa Chakoma Mchafu katika kikao na Watendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) leo Februari 12, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Husna Sekiboko, wamepatiwa mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yaliyoongozwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma.
Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako (Mb), imefanya kikao kazi cha kwanza leo tarehe 12 Januari,2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe wametoa mafunzo kwa Wabunge waliochaguliwa kushiriki katika nafasi za Uwakilishi katika Taasisi mbalimbali za Kikanda na Kimataifa.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Abdallah Chikota katika kikao na Watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) leo Februari 12, 2026 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.