A prolific Swahili News Anchor with a nose for news/ presenter/political guru /News editor/video editor/news reporter and a seasoned journalist . @radiomaisha
Mtu mmoja amefariki kutokana na korona huku watu watano zaidi wakithibitishwa leo kuambukizwa virusi vya korona na kufikisha idadi ya waliombukizwa nchini kuwa 184.
#HabariZaSasa
Kiongozi wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ameendela kuwasihi wananchi kuhakikisha kwamba wanafuata maagizo ya serikali kuzuika maambukizi ya virusi vya korona nchini
#HabariZaSasa
Kisanga kimeshuhudiwa katika Bunge la Kitaifa wakati wabunge waliposhinikiza kuondoka kwa Mbunge wa Eldas, Adan Keynan wakidai kwamba alikuwa amewasili nchini kutoka London hivyo kustahili kuwa karantini kwa kipindi cha siku 14.
#HabariZaSasa
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza Machi 21 kuwa siku ya maombi ya kitaifa kwa ajili ya maambukizi ya Virusi vya Korona nchini.
Kufikia sasa watu wanne wamethibitishwa kuambukizwa Korona nchini.
#HabariZaSasa
Mhudumu mmoja wa teksi ametengwa katika Hospitali ya Mukuru Health Centre baada ya kufika huko akihofia kuwa na maambukizi ya Virusi vya Korona.
#HabariZaSasa
Wakristo nchini wamehimizwa kuliombea taifa wakati huu linapokabiliwa na maambukizi ya Virusi vya Korona. Kasisi wa Kanisa Katoliki la Maralal, Virgili Pante amewahimiza Wakiristo pia kufuata maagizo yote yanayotolewa.
#HabariZaSasa
Shughuli za kawaida zimesitishwa katika Shirika la Kutoa Huduma za Vijana, NYS huku wanafunzi wakiagizwa kutoendelea na utaratibu wa kawaida wa masomo katika juhudi za kukabili maambukizi ya Virusi vya Korona.
#HabariZaSasa
Mwanamume anayeshukiwa kuwa na Virusi vya Korona anaendelea kutengwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Londiani kwenye Kaunti ya Kericho.
#HabariZaSasa
Walimu Wakuu wa Shule za Upili nchini KESSHA ambaye pia ndiye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Machakos, Kahi Indimuli Kahi ameipongeza serikali kufuatia agizo la kufunga kwa shule ili kuzuia maambukizi ya Korona.
#HabariZaSasa
Kampuni ya Ndege ya Jambojet imesitisha safari za ndege kuelekea mataifa jirani ya Uganda na Rwanda. Hatua hii ni miongoni mwa za hivi punde zinazoathiri sekta ya usafiri wa angani.
#HabariZaSasa
Polisi mjini Mombasa wanamsaka mwanamke aliyeonekana akimwadhibu mjukuu wake mwenye umri wa miaka minane kwa kumtishia kumrusha kutoka kwa dirisha kwenye jengo la orofa nne.
#HabariZaSasa
Shughuli za uchukuzi zimetatizika katika Barabara Kuu ya Nairobi-Kisumu baada ya wanafunzi wa Chuo cha Kiufundi Kisumu kuandamana wakikashifu hatua ya usimamizi wa chuo hicho kuongeza karo.
#HabariZaSasa