Infantino claims he can't do anything about Referees, players, journalists and fans being banned from the World Cup because in every country there are Governments.
In 2023 Indonesia refused to let the Israeli U23 squad have visas
FIFA instantly moved the tournament to Argentina
Qatar said it doesn’t matter who you are or where you come from, you can come to the World Cup, just don’t drink alcohol at the stadium.
USA said you can’t come. Who you are or where you come from matters. We’ll decide who can and can’t participate. This isn’t a sport for everyone.
Madhara ya Propaganda!
Tatizo kubwa la kuendesha nchi kwa propaganda badala ya uhalisia ni kwamba propaganda inaweza kuchelewesha ukweli, lakini haiwezi kuubadilisha.
Kwa muda, propaganda inaweza kufanya watu waamini kwamba mambo yanaenda vizuri kuliko yalivyo. Lakini mwisho wa siku, wananchi hawaishi kwenye hotuba; wanaishi kwenye uhalisia.
Unaweza kuwaambia watu uchumi unakua kwa asilimia 10, lakini kama hawawezi kumudu chakula, kodi, umeme au ada za shule, wataamini mifuko yao kuliko matangazo ya serikali.
Unaweza kuwaambia watu haki za binadamu zinaheshimiwa, lakini kama wanaona watu wakikamatwa kiholela au kutekwa na kuogopa kutoa maoni yao, watayaamini macho yao kuliko taarifa rasmi.
Unaweza kuwaambia watu rushwa imepungua, lakini kama bado wanatoa rushwa kupata huduma, watayaamini maisha yao kuliko takwimu.
Ndiyo maana serikali zinazotegemea propaganda sana huanza kupoteza uwezo wa kujisahihisha.
Kwa nini?
Kwa sababu propaganda hujenga mazingira ambayo viongozi husikia wanachotaka kusikia badala ya kile wanachopaswa kusikia.
Taarifa mbaya zinafichwa.
Wakosoaji wananyamazishwa.
Takwimu zinapambwa.
Mafanikio yanakuzwa.
Mapungufu yanafichwa.
Matokeo yake ni kwamba serikali huanza kuishi ndani ya picha iliyojichorea yenyewe badala ya nchi halisi.
Hili ndilo lililotokea katika tawala nyingi duniani.
Katika dakika za mwisho za utawala wa Soviet Union, viongozi waliendelea kuambiwa kwamba mfumo ulikuwa imara wakati tayari ulikuwa unaanguka.
Katika Iraq ya Saddam Hussein, viongozi waliogopa kusema ukweli kwa sababu walitaka kusikia habari njema pekee.
Katika Zimbabwe ya Robert Mugabe, propaganda ziliendelea kuhubiri mafanikio wakati uchumi ulikuwa ukianguka.
Tatizo la propaganda si kwamba inadanganya wananchi pekee.
Tatizo kubwa zaidi ni kwamba huanza kuwadanganya hata viongozi wenyewe.
Kiongozi anapoanza kuamini propaganda zake mwenyewe, maamuzi mabaya huongezeka.
Rasilimali huwekezwa mahali pasipo sahihi.
Tahadhari za mapema hupuuzwa.
Migogoro huachwa ikue.
Na matatizo yanapotokea, huwa makubwa zaidi kwa sababu yalifichwa kwa muda mrefu.
Utawala bora unahitaji ukweli.
Propaganda huuliza:
“Wananchi wanapaswa kusikia nini?”
Uongozi bora huuliza:
“Ukweli ni nini?”
Propaganda hutafuta kuonekana mzuri.
Utawala bora hutafuta kufanya vizuri.
Propaganda hujenga picha.
Utawala bora hujenga taasisi.
Propaganda huishi kwa leo.
Mifumo imara hujenga kesho.
Ndiyo maana taifa lolote linalotaka maendeleo ya kudumu lazima lijenge utamaduni wa ukweli, uwazi na uwajibikaji. Kwa sababu ukweli unaweza kuumiza kwa muda, lakini propaganda huumiza taifa kwa muda mrefu zaidi.
Kama alivyoonya Dietrich Bonhoeffer, “Adui mkubwa wa jamii si uovu pekee, bali mazingira ambayo ukweli hauwezi kusemwa.” Taifa linapoanza kuogopa ukweli na kupenda propaganda, linaanza kupoteza uwezo wa kujirekebisha. Na taifa lisiloweza kujirekebisha huanza kujiandaa kwa mgogoro wake wenyewe.
Rev Peter Simon Msigwa.
Iringa
Tatizo kubwa la Tanzania leo si ukosefu wa wasuluhishi wa migogoro ya ndoa. Tatizo kubwa ni mifumo dhaifu ya utawala.
Wakati serikali inakabiliwa na tuhuma nzito za ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa uwajibikaji, wananchi walitarajia kuona viongozi wakuu wakijikita katika kujenga taasisi imara na kurekebisha mifumo inayozalisha matatizo hayo.
Ni jambo jema kiongozi kusikiliza matatizo ya wananchi. Lakini nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutatua kesi moja moja za watu.
Kiongozi anaweza kusuluhisha ndoa moja leo, lakini kama mfumo wa haki una matatizo, kesho kutakuwa na ndoa nyingine mia moja zenye migogoro.
Anaweza kusaidia mfanyabiashara mmoja leo, lakini kama mfumo wa rushwa haujabadilika, kesho wafanyabiashara elfu moja wataendelea kuteseka.
Anaweza kutatua mgogoro wa kiwanja kimoja leo, lakini kama taasisi za ardhi zinaendelea kuwa dhaifu, migogoro mingine elfu itaendelea kuzaliwa.
Tofauti kati ya mwanasiasa wa kawaida na mwanamageuzi ni kwamba mwanasiasa hushughulika na matokeo, lakini mwanamageuzi hushughulika na chanzo cha matatizo.
Rushwa si ugonjwa; ni dalili ya ugonjwa.
Ufisadi si tatizo la kwanza; ni matokeo ya tatizo kubwa zaidi.
Chanzo chake mara nyingi ni:
taasisi dhaifu,
ukosefu wa uwajibikaji,
ukosefu wa uwazi,
sheria kutotumika kwa usawa,
na mkusanyiko mkubwa wa madaraka sehemu moja.
Hapa ndipo tunapopata somo kubwa kutoka kwa Kanuni ya Jethro (Jethro Principle) katika Kutoka 18.
Musa alikuwa akihukumu kila kesi mwenyewe. Alisikiliza kila mgogoro, mkubwa na mdogo. Alikuwa akijaribu kuwa mahakama, polisi, msuluhishi na kiongozi kwa wakati mmoja.
Jethro alipofika alimwambia:
“Hili jambo unalolifanya si jema. Hakika utajichosha wewe na watu hawa walio pamoja nawe.”
Suluhisho la Jethro halikuwa kumsaidia Musa kusikiliza kesi nyingi zaidi.
Suluhisho lilikuwa kujenga mfumo.
Aliagiza wachaguliwe viongozi wa makumi, hamsini, mia na maelfu ili washughulikie mambo ya kawaida, huku Musa akibaki kushughulikia masuala makubwa ya kimkakati.
Kwa lugha ya kisasa, Jethro alikuwa anasema:
Kiongozi mkuu hafanikiwi kwa kufanya kila kitu mwenyewe. Hufanikiwa kwa kujenga taasisi zinazofanya kazi hata bila uwepo wake.
Tatizo la Afrika kwa ujumla si ukosefu wa viongozi wenye nguvu.
Tatizo ni ukosefu wa mifumo yenye nguvu.
Nchi nyingi zimejenga viongozi wakubwa kuliko taasisi zao.
Matokeo yake ni kwamba kila jambo linasubiri Rais, Waziri Mkuu, Waziri au Mkuu wa Mkoa.
Barabara inasubiri maelekezo ya juu.
Mgogoro wa ardhi unasubiri maelekezo ya juu.
Hata migogoro ya familia wakati mwingine inasubiri maelekezo ya juu.
Hiyo si dalili ya uongozi imara.
Ni dalili ya taasisi dhaifu.
Katika taifa lenye mifumo imara, mwananchi hapaswi kusafiri mamia ya kilomita kwenda kulalamikia Waziri Mkuu ili kupata haki yake.
Anapaswa kuipata haki hiyo katika ngazi ya kijiji, kata, wilaya au mahakama kupitia taasisi zinazofanya kazi kwa ufanisi.
Kazi ya viongozi wakuu wa taifa si kuwa wasuluhishi wa kila mgogoro.
Kazi yao ni kuhakikisha kuna mfumo unaozuia migogoro mingi kutokea na unaotatua migogoro inayotokea kwa haki na kwa haraka.
Wananchi hawahitaji tu viongozi wanaoweza kusuluhisha matatizo ya watu binafsi. Wanahitaji viongozi wanaoweza kujenga mifumo ambayo itafanya matatizo hayo yasitokee kwa kiwango kikubwa.
Historia haikumbuki viongozi waliotatua matatizo ya mtu mmoja mmoja. Historia huwakumbuka viongozi waliojenga taasisi imara, waliosimamia haki, na waliobadilisha mfumo kiasi kwamba hata baada ya wao kuondoka madarakani taifa linaendelea kusimama.
Kwa sababu mwisho wa siku, taifa haliendelezwi na uwezo wa viongozi wake kufanya kila kitu. Taifa huendelezwa na uwezo wa mifumo yake kufanya kazi hata viongozi hao wanapokuwa hawapo.
Ukimtukuza mtu kuliko mfumo, utapata mashujaa wachache na matatizo mengi.
Ukijenga mfumo kuliko mtu, utapata taifa imara na maendeleo ya kudumu.
🚨 EXPOSED: Samia Suluhu Hassan LIED straight to Putin and Russian media!
She boldly claimed ‘Tanzania is NOT under Western & European sanctions’ while begging for deals in Moscow.
LIES! EU froze €156M, US sanctioned her brutal police thugs for torture & election massacres, Washington reviewing ALL ties.
Samia is desperately shopping for Russian cover while her regime drowns in blood and isolation.
The whole world sees your hypocrisy, Madam Liar!
@KremlinRussia_E@mfa_russia@RT_com@SputnikInt@EU_Commission@StateDept@EUParl_EN
AIBU YA MWAKA HUKO RUSIA KWA MWENYE PhD 8
SWALI ALILOULIZWA SAMIA KWA MARAISI WA CCM NI MPAKA au NYERERE TU WANGETOBOA.
Samia ameulizwa swali na mwandishi wa Habari wa Russia, tena kwenye mkutano ambao uko chini ya control ya serikali au Putin. Swali limeulizwa: 'Sisi tunafanyaje maendeleo na ushirikiano wakati kuna vikwazo?' Wakati swali linaulizwa, unaona Putin anatabasamu kwa bashasha kubwa, maana hapo ndipo Putin alitaka kujua: 'Hapa tuna rafiki au msanii tu?'
Malengo ya lile swali hili ilikuwa ni Samia ongee akiwa kwenye ardhi ya Russia na kupeleka moto mkali kwa Marekani na Ulaya. Haya ni maswali ya kijasusi, si maswali ya moja kwa moja kujibiwa kienyeji kama alivyofanya, akaanza kulia kwamba ana uhusiano na Ulaya hakuna vikwazo.
Hahaha, Putin yeye hana la kumtisha na Ulaya au Marekani, alitaka sasa aone Samia akijitoa kwenye network na kuongea kama kiongozi wa Korea Kaskazini na kujipiga kifua kwamba sisi vikwazo siyo kitisho kwetu, tuko huru, bla bla, tunasimama wenyewe, hatutaki kuingiliwa.
Hayo ndiyo majibu Putin alikuwa anasikiliza, sababu kwa mazungumzo ya chumbani, Samia najiona mwamba kwamba yeye atishiki. Sasa walimtia pale kwenye ubao aongee tena hayo anayosema. Akashindwa, na mbaya zaidi, akabadilisha na lugha kabisa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili.
Kwa wenye akili kama ya Putin, washajua kwamba hapo hakuna mtu ni msanii tu anasaka pesa, Putin sio boya alisha mseti aseme mbele ya Dunia.
Swali lenyewe liliunganishwa kwenye angle ya Ukraine, kama angekuwa na akili kidogo kusoma chumba, angesoma kwamba hapo ni wakati wa kuchagua mchumba mmoja, Rusia au Magharibi, akaamua kutembelea vyombo vyote. Kitu ambacho hakimsaidi ni kwamba kuwa na Putin tu pale ni kimeo.
Putin kweli, malengo yake yametimia, wewe mwenye PhD 10 umeshindwa kuelewa walioulizwa nini. Anaruka akisema mimi sina vikwazo. Mwandishi wa Habari wa Urusi ametumwa na serikali ya Urusi, wanajua vikwazo vyanavyo, sasa unaambiwa na Urusi una vikwazo, wewe unamkatalia KGB? Wao wanafanyia kazi mambo ya mbele, wamesha confirm kwamba unapigwa vikwazo kila kona, unakana?
Kwa kifupi, Rusia walikua wanamwambia Samia: kwamba wewe una vikwazo tayari je tunasonga vipi mbele na wewe? Kama uwezi kukoma kwenye mazingira ya vikwazo hatuna cha kufanya na wewe, na Samia ameshindwa kuonyesha mkakati alionao ili kufanya ushirikiano akiwa na vikwazo.
Kwa Dunia ya sasa hakuna Kiongozi yeyote anayekwenda Rusia kwa sasa ambayo bado anapambana kuwa na mahusiano na Ulaya na Marekani, unapo chagua ushirika na Rusia unaachana na ushirikiano na Mataifa hayo mengine, haiwezekane ukalamba kotekote sababu hali ya sasa Dunia inakataa kutokana na Rusia kuwa kwenye mgogoro wa Kijeshi na hayo mataifa mengine.
Hivi inawezekana vipi Ulaya wakaachana mpaka na nishati ya Gas ya kutoka Rusia wananchi wao wakateseka, halafu Tanzania ikaenda Rusia kufanya biashara na Mrusi kisha Tanzania hiyo hiyo ikaenda Ulaya na Marekani kufaidia na misaada na biashara pia ? Huu ujinga mbona ni wa kiwango cha lami? Matarajio ya kila mtu ilikuwa ni hii safari ya maCCM huko Rusia ni kufunga ndoa na Rusia na kuachana na Magharibi yenye masharti mengi ya haki za binadamu na demokrasia kwamba hii ndio ilikuwa point ya safari .
Kwa hiyo Suala la vikwazo lilikuwa si la kukana; lilikuwa la kuelezea yeye, Samia, anapitisha vipi serikali ya CCM kwenye hivyo vikwazo au anakomaa vipi kwenye ushirikiano wake na Russia wakati huo akiwa na vikwazo hapo Putin angepima kama amepata mdau. Akili zimeganda, mnakomalia madaraka. Unakubali kwenda kuongea mbele ya media za nchi zinazosoma usichosema. Rusia ni majasusi wanajua vizuri Tayari ni suala la muda tu kina umma vikwazo vinakuja, sasa unawabishia
Rusia wanajua nini kilitokea Tanzania, Lakini wanajua mambo ambayo Samia amezungumza baada ya kufanya mauaji ( nimeweka video moja hapo chini) , Nchi kama Rusia unapokwenda wanakuchungulia kwa darubini , KGB wanafanyakazi yao vizuri kujua mgeni ni wa aina
Hii ndio kazi imepongezwa na viongozi wote wa ccm.
Bwana Kombo huyu Mwananchi alikua anarusha jiwe kwa Nani mpaka afanyiwe haya?
Kwanini Mtanzania avuliwe nguo na kubakizwa uchi wa mnyama?
Sheria gani inamruhusu askari kufanya hayo?
Hii video ndio sababu sitokaa kurudi tena kwenye umbea mpaka haki ipatikane Tz. I feel like nina deni kubwa la kuhakikisha hivi vifo vinapata haki na vinaleta haki kwenye nchi. This video ndio sababu I will never abandon the movement.
Kwa mara ya kwanza leo naposti full clip.
Video ya kwanza ndio original video. Video ya pili ndio video niliowapostia Watanzania, nilikata jina langu. I did this to a number of videos za Arusha. For some reason vijana wengi wa Arusha walikuwa wanasema “Dada Mange ona wanatuua” au “Mtumie Mange Kimambi aone”. Nitaachia na video zingine nilizokata jina langu.
The reason I’m posting this today ni sababu wauwaji wanalipa watu kusema kuwa hawa vijana walilipwa.
@SuluhuSamia kwanini hawa vijana hawakuita jina la waliowalipa waandamane? Instead wanaita jina la dada yao aliewapa elimu ya umuhimu wa kuandamana ili kudai haki kwenye nchi yao?????? Au niliwalipa mimi???
Vijana wa Tanzania naomba mjue, I’m in this fight mpaka haki ipatikane Tz au mpaka siku nakufa…… Hakuna kitu kingine nitafanya kwenye mitandao zaidi ya kudai haki juu ya vifo hivi….
BREAKING: VIDEO MPYA. NEW VIDEO EVIDENCE OF THE VIOLENCE THAT TANZANIANS ENDURED DURING THE INTERNET BLACKOUT UNDER SAMIA SULUHU ORDERS.
WATANZANIA AMBAO MLIKUWA MNAOGOPA KUACHIA VIDEO, PLEASE NITUMIENI ILI DUNIA IONE ILI TUPATE MSAADE WA NJE!!!!! WhatsApp +1 424 537 3057
Hii issue ni mbaya sana
Ina maana ujenzi wa huo uwanja hizo billion 400 wana kampuni tayari ndio maana wanashinikiza
Kwa maana nyingine wnataka kutupiga hii pesa kutupia kampuni la ujenzi , ku supply materials na mambo mengine
Uwanja unajengwa Mgumu kwa pesa yote hiyo? Na kwa nini unakwenda jengwa kwenye eneo ambalo liko karibu sana na mbuge kwa ndege kubwa zitasumbua wanyama, wakati Musoma kuna uwanja ambao wangeutanua kidogo tu na kuhakikisha barabara iko sawa kufika hapo Mgumu wala sio mbali kutoka Musoma
Kikwete alifirisi NSSF toka wakati huo hii taasisi haijapata nguvu tena,
Samia anafirisi PSSSF kwa kasi kubwa sana
Wazee wataanza kufa kwa kasi mbaya sana kwa kukosa kiinua mgongo
Samia kisingizio chake ni kwamba mbona wengine walifanya, ukiwa mkristo anasema unampiga vita sababu ya ukristo
Hivi kweli mmekubali nchi kuliwa sababu mtu anawaambia mambo ya jinsia yake, dini yake na uzanzibar?
#KatibaMpya
Kombo anasema tume heal na tumesahau!!! Kama vile waliua kuku!
Katibu mkuu wa ccm amepongeza hii kazi na kuita kazi iliyotukuka..
Samia mwenyewe amesema polisi walifanya kazi nzuri sana na kwa mda mfupi mno.
Nimemsikiliza mkuu wa mambo ya nje na zile barua zake 25, nimecheka kweli kama mazuri! mkuu wa mambo ya nje asiyejua historia ya nchi yake mpaka ategemee wa jalalani! Interesting ni kwamba baba yake alikuwa mwanasiana mkongwe huko kwao na right-hand man wa Mwalimu kwenye masuala ya siasa kwao, ungetegemea basi angalau angekuwa na interest ya kujifunza historia ya nchi yake!
Hakuna kitu kibaya kama hujui kama hujui na kibaya zaidi ni pale kutokujua huko kunapogeuka kuwa ujasiri wa kuwashawishi wengine kuwa nao hawajui.